Singida dengu inalimwa sana kwenye aridhi ya MBUGA
Changamoto kubwa ya zao hili ni TIMING ya kulima
Dengu haitaki nvua nyingi, inatakiwa nvua ikikata tu aridhi ikiwa bado ina unyevu nyevu ndio unalima na kupanda dengu
Unaweza kulima ukidhani mvua imekata na mvua ikirudi hata mshindo mmoja tu mbuga ikalowana vya kutosha inakula kwako
Au mvua inaweza kukata mapema ukadhani itarudi na unyevu nyevu ukaisha shambani na mvua isirudi hapo pia imekula kwako
Mara nyingi Singida mvua zikianza kukaribia kukata unaingiza trekta au ngombe na unalima kwanza bila kupanda ili kulainisha shamba.... halafu ukiwa na uhakika mvua imekwenda unaingia tena kulima na kupanda, hapo mbuga inakua laini na mazao yataota vizuri
Dengu mara nyingi haina shida wala haiitaji palizi, labda ishambuliwe na wadudu ndio utahitaji kupulizia dawa
Na ulimaji wa Singida bado ni ule wa kupanda kwa kumwagia mbegu shambani kisha ndio unalima
Hapa inahitajika kama debe 2 hadi 4(ndoo mbili za lita 20) kama mbegu kwa eka moja(wastani miguu sabi kwa sabini)
Mavuno inategema na timing yakulima, aina ya mbegu, kiasi cha mbegu ulichotumia na kama zao liliahambuliwa na wadudu
Wastani ni gunia kuanzia 3 hadi 5 kwa eka moja
Uzuri wa dengu bei yake huwa inacheza kuanzia 200k kwenda juu kulingana na mwaka na mahitaji ya wanunuzi kutoka nje