Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?

Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?

Chadema is a very weak party.

Mtu dhaifu mara nyingi anapenda sana visa.

Mtu mwenye nguvu hupenda amani na ni rahisi kusamehe.

Uimara wa Chama ni pamoja na kuonesha busara katika maamuzi yake.

Ccm huwa inawafukuza na huwasamehe na kuwarejesha wanachama wake waliokengeuka.

Ila madhaifu chadema hayana huo ubavu.

Yana gubu kama mashangingi ya kiswahili .
 
Kwanza, maelezo yako mengi huonyesha kuwa CHADEMA ina viongozi, wanachama na wafuasi wasiojitambua, wanaojisikia sana, wasiosikia mawazo mbadala, wabishi na wasio na mikakati ya maana. Na hiyo ni kero kubwa sana kwako. Umetoa tishio la karma kwao mara kwa mara.
Mkuu Drifter ,CHADEMA ina viongozi, wanachama na wafuasi wasiojitambua, wanaojisikia sana, wasiosikia mawazo mbadala, wabishi na wasio na mikakati ya maana, hii ni uongo?. Chadema imewahi kuwa na mikakati gani ya kuingia Ikulu?.

Hili ya karma kuitandika, Chadema, sio tishio ni real!. Kwa vile unaweza kunisoma naamini kabisa unaiona karma inavyo itafuna Chadema, and take it from me, mkifanikiwa kuwatimua hawa 19 bila kuwatimua kwa haki, believe me, the karma consequences will be devastating!. Mlipo mtimua Zitto, niliwashauri Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"... unajua ni nini kiliwakuta wahusika wakuu wote wa kadhia hii, mmoja baada ya mwingine?. Mimi nakijua!, watu mkiambiwa wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii, mnabisha!.

Tena hizo karma, ni cha mtoto, nimewashauri Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu karma yake itakuwa very devastating!.

P
 
Pili unawaaminisha kuwa “njia ya kwenda Ikulu” na kuondoa CCM i wazi kwao endapo watashirikiana na wapinzani wengine including some dubious characters.
Mkuu Drifter, kuna vitu vinaitwa facts and fallacies, ili kupata mafanikio, kuna mambo unaweza kufanya mwenyewe na ukafanikiwa, na kuna mambo huwezi kufanya mwenyewe ukafanikiwa no matter how good you are!. Haya yanahitaji team work!. Hivyo it's a fact kuwa Chadema peke yake haiwezi kuing'oa CCM na kuingia Ikulu, ni lazima ishirikiane na wengine hata kama some ni dubious!. Na ndia maana hapa Kwa Hili! Hongera Sana Chadema, Hongera Mhe. Mbowe!, Sasa Muwege Mnasikilizaga Ushauri!

P
 
Pia wakimezea na kusamehe baadhi ya maovu hata uvunjifu wa katiba na ukiukaji wa sheria unaofanywa na dola.
Mkuu Drifter , ili kufanikiwa sometimes there is some give and take, sometimes one has to make some sacrifices, sometimes in order to win, you have to lose or a win win situation, ikiwemo kumezea na kusamehe baadhi ya maovu hata ya uvunjifu wa katiba na ukiukwaji wa sheria unaofanywa na dola!, angalia hapa niliuliza nini Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee? na kwa kuwasaidia wavivu wa kufungua links
View: https://youtu.be/A_YPEHtM9WM?si=cZxp-SqoWsQlkAlj
Sihitaji kugusia kuhusu illegality ya masuala ya hao wabunge 19 waliofutwa uanachama na CDM wala illegality ya kesi ya ugaidi na
“msamaha” kwa Mbowe. Mitazamo yako ni questionable.
Naomba kuheshimu msimamo wako on illegality na mimi pia nimefanya reciprocity
P
 
Sote pamoja na wewe tunajua kuwa CCM haina mpango wa kuruhusu uchaguzi huru na wa haki.
Mkuu Drifter , usichanganye CCM na serikali, CCM ni chama cha siasa na kutafakari kutawala milele!, hivyo CCM kitafanya kila liwezekanalo kuendelea kutawala, hili nimelisema humu mara kibao
-"CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!

CCM ni chama tuu, sio mwenye mali, mwenye mali ni Mtanzania ameipa CCM ridhaa ya kututawala, hivyo mwenye mali akiamua CCM basi, CCM inawekwa kando!.

Kama mwenye mali anataka uchaguzi Mkuu huru na wa haki, anapaswa kumueleza yule mtumishi wetu, Rais wa JMT, kuwa 2025 tunataka uchaguzi Mkuu huru na wa haki utakaotumia sheria za haki za uchaguzi, na kusimamiwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.

Katika salamu zangu za kuuaga mwaka 2022, kuukaribisha 2023 niliuliza Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu? nikagundua sisi Watanzania ni maneno matupu vitendo sufuri!.

Hiki ndicho na mimi ninakwenda kuwasaidia Watanzania 2024.
P
 
Hizo bla bla kuhusu mkakati wa CDM kuingia Ikulu hazina mantiki yoyote. Kinachoonekana dhahiri ni janja ya kutaka kushusha kiwango cha brand ya CDM.
Hapa naomba to reserve my comments
Mienendo ya vyama vingine vya upinzani na viongozi wake inajulikana. Pendekezo la ushirikiano linaacha maswali.
We need a united front. Sometimes ili uweze kushinda vita ni lazima ushirikiane na adui yako against a common enemy!.
Hii kukubaliana moja kwa moja na mambo ya ovyo yanayofanywa na serikali ndio mwanzo wa viongozi wa CDM kuonekana “wamelambishwa asali”. Hata “maridhiano” wengi hatuyafurahii ingawa tunayaelewa kiasi fulani.
Kuna msemo wa kizungu unasema when you are in a difficult situation caught in between the two devils, choose the lesser!,
Ni ukweli wa wazi kabisa tena wa mchana kweupe, Chadema imelambishwa asali!, nusu mkate ni asali tuu!, tuliwaeleza humu, Siasa za Kijungu Jiko, Penye Uzia, Penyeza Rupia!. Hakuna Mkate Mgumu Mbele ya Chai!, Hata Uwe Mgumu Vipi, Mbele ya Chai/Rupia, Lazima Utalainika!
P
 
Kilicho dhahiri pia ni kuwa dola inachokoza kijanja (provoke) wapinzani ili wahamaki ipate fursa ya kuwagonga kwa kisingizio cha kulinda amani. Zile kamati na mahubiri mtiririko ya amani majukwaani na kwenye nyumba za ibada ni maandalizi ya kimkakati. Hatuna illusion kuwa eti CCM inaweza kuondoka madarakani kwa kura (vikaratasi) wala katiba (kijitabu). Hivyo tunaposoma mada za kuhimiza CDM ikubaliane na “nusu shari” ili iishi hata kwenda Ikulu tunajiuliza dhamira ya mwandishi ni ipi hasa?
I reserve my comments
Kitu pekee unachoweza kuisikitikia (CDM), kama kweli unajali, ni mtihani mgumu ilio nao wa kuingia kwenye uchaguzi mkuu katika mazingira yasiyokubalika kabisa. You may wish to put a word on that.
Kwa hili mimi siisikitikii Chadema bali naisikitikia nchi yangu Tanzania, na kuwasikitikia Watanzania, enzi za JPM, nilikuwa nikiwa na langu jambo ambalo nataka lifanyike, unamlengeshea Magufuli, kimtindo kwa kumlia timing, anaingia King utaona tuu linafanyoka!, toka Maza ametimba, hili la sheria ya uchaguzi, tume huru na Shirikishi ya uchaguzi na creating
a level playIng field, nimelianzishia mabandiko zaidi ya 10, Maza kimya!, ndio juzi kati wametuletea kiini macho, cha mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya!. Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili?. Ni Mvinyo wa Zamani, Kwenye Chupa Mpya?. Why Ubatili Huu?!.
P
 
Mwisho kabisa sina shaka unajua vizuri sana kuwa mabandiko marefu yenye cross-references kibao ndio kile kinachoitwa “stringing people along”. Tutaendelea kukusoma hadi tufike huko unakotupeleka. Have a good day, Sir.
Mkuu Drifter , asante endelea kunisoma, ila faida yangu mimi ya ziada, ni zaidi ya kutumia silaha ya kalamu, kuandika magazetini na mitandaoni na silaha ya sauti kwa kutangaza kwenye Redio na TV kupitia vipindi vyangu, bado nina silaha ya maangamizi makubwa, WMD, hivyo hatua yangu ya kwanza ni amsha amsha, maana nilikuja kugundua sisi Watanzania ni maneno maneno matupu lakini vitendo sufuri!, Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Hivyo mwaka huu wote wa 2024 ni mwaka wa amsha amsha, na mwaka 2025 ni mwaka wa vitendo, na kisipoeleweka, ni kubutua tuu WMD!.

Mungu Ibariki Tanzania
P
 
Andiko nzuri my Adv.Mayala, ila HAKUNA mgogoro ndani ya CHADEMA, huo mgogoro unaouna wewe kama mwandishi, issue hii CHADEMA walishatoa uamuzi wake na uamuzi ule ulikua kuwafukuza uanachama wale watuhumiwa, kwa shinikizo la chama dola wakaenda mahakamani na hukumu imetoka, case hii imefungwa, na tuelewe kuwa kujiunga na chama cha kisiasa ni hiari ila ni muhimu katiba ya chama hicho kuiheshimu.Tanzania yangu inahitaji kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Hao wabunge wanawauma nin mzee waacheni
 
Wanabodi

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa, Chadema ni chama cha Kitaifa hivyo haya yanayoendelea ndani ya Chadema katika huu mgogoro wake na wabunge wake 19 wa viti maalum, una athari za Kitaifa zenye maslahi kwa taifa. Hoja yangu ya leo ni hii ,"kuna watu wana macho lakini hawaoni!, na wana masikio lakini hawasikii!". Swali ni je Chadema wana macho na yanaona?. Je wana masikio na yanasikia?. Kwenye hili la Wabunge 19, je Chadema wawasamehe wabarikiwe, au waendelee kukomaa nao mpaka kieleweke hata kama ni kulaaniwa?.

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili, kwa inspirational kutoka andiko la Kaka yangu/mdogo wangu na bosi wangu kule TEF, Deodatus Balile.

Balile ameandika bandiko hili akiwa safarini jijini New Delhi nchni India.
C&P ya Balile

Mwisho wa kunukuu

Chief @⁨Balile⁩ , nikiwa New Delhi nilijifunza imani ya Hinduism kuhusu kitu kinachoitwa karma, hivyo ushauri wako kwa Chadema, utawaepushia Chadema karma ya mambo
mabaya waliowatenda hawa wadada 19 ambao mimi nawaita ni mashujaa, hivyo huu ni ushauri mzuri, wa hekima na busara sana kwa Chadema wenye maslahi kwa Chadema na maslahi kwa taifa only if Chadema wana macho ya kuona na wanaona, na wana masikio ya kusikia na wanasikia, kwasababu kuna watu wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii.

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anakabiliwa na kesi ya ugaidi, nilipandisha makala mfufulizo za Kilio cha Haki, nikiangazia haki jinai.
Kwenye sala yetu ya Baba Yetu, kuna mstari "Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea" hivyo tulimpongeza rais Samia kwa kauli hii baada ya Freeman Mbowe kuombewa msamaha
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Baada tuu ya bandiko hili, haukupita muda hatimaye Freeman Mbowe alisamehewa na kesi ya Mbowe ilifutwa!,

Sisi wa kupongeza tukapongeza
Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Sasa kuna ugumu gani Chadema kuwasamehe hawa wabunge wake 19?.

Hili sakata la wabunge hawa toka lilipoanza, mimi nimekuwa very open, objective and very transparent
Na nikashauri Chadema



Katika Salaam zangu kwa mwaka mpya, Mahali ni pazuri ndugu wanapokaa, wakipata vema na kupendana. Tulikotoka ni kugumu, tunakokwenda ni kurahisi, kuzuri! Heri ya Mwaka Mpya wahusika wote

Japo kwa jicho la juu juu, hao 19, wanaonekana kama wameshinda kesi yao mahakamani but in reality ni wameshindwa na hili nililisema The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! kwasababu katiba ya Chadema ina kipengele kilicho kinyume cha katiba, mwanachama wa Chadema akifungua shauri lolote mahakani, akishindwa kesi ni amejifukuzisha, hivyo Mahakama tayari imeishabariki kufukuzwa kwao, salama yao ni kusamehewa tuu!.

Kwa vile mimi namfahamu Freeman Mbowe kuliko Chadema wengi, Mbowe ni muungwana, Mbowe ni mtu wa shukrani, na baada ya kikao cha CC kuwatimua, Freeman Mbowe aliingia huruma na kufukuzwa kwao, akawasamehe, akawaita Nairobi, akawasamehe, akawashauri waombe msamaha, ili wayamalize, wakamgomea!.

It's high time Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Aikael Mbowe, kuitumia kofia yake ya Uenyekiti wa Chadema kwa kuitekeleza kwa vitendo sala ya Baba Yetu, kwa mtindo wa reciprocity kama yeye alivyosamehewa bila kuomba msamaha, sasa ni zamu ya na yeye kusamehe tuu bila kuombwa msamaha?., au Chadema iendelee kukomaa nao ili kuwaonyesha, kuwakomoa na kuwanyorosha?.

Tena na mimi kwa vile ubavu wangu ni pande za Kaskazi, na mimi nimeunga tela hija za migombani.

Merry Christmas

Paskali.
Kaka,mbona km unabariki udharimu wa kipumbavu kwenye jamii ya wastaarabu?
Mtu alikuwa mahabusu mpaka usiku,kulivyokucha anaapishwa sebuleni na baadae kutinga Bungeni,kwako ina maana gani?

Wateuzi wa hao COVID-19 wakathibitisha kuwa hawahaja husika popote toka hatua za awali ndani ya chama chao ila walishuhudia kupitia vyombo vya habari,wewe huoni km kuna rushwa hapa iwe ni ya madaraka ama namna nyingine?

Hivi kwa akili yako kesi ya ugaidi ina msamaha ikiwa imethibitishwa na mahakama?

Je,kwako kusamehewa kwa hao kuna maana ipi tofauti na kuruhusu upumbavu na uhuni kuendelea kwenye jamii inayojinadi kuwa ya kidemokrasi?

Je,ingelikuwa ni Chadema ndio wanawalipa watu wasiokuwa na uhalali wa kulipwa mamilioni ya fedha ilihali watumishi wanaidai serikali malimbikizo ya mishahara yao wewe na chama chako mngelikuwa mnachekelea tu?

Mimi si mwachama wa chama chochote cha kisiasa wala cha ushirika lkn pamoja na makosa mengi ambayo chama chako kimekuwa kikitufanyia Watanganyika mawili makubwa ni Uchafuzi mkuu na kuwalipa COVID-19 fedha zetu.
 
Mkuu Drifter , asante endelea kunisoma, ila faida yangu mimi ya ziada, ni zaidi ya kutumia silaha ya kalamu, kuandika magazetini na mitandaoni na silaha ya sauti kwa kutangaza kwenye Redio na TV kupitia vipindi vyangu, bado nina silaha ya maangamizi makubwa, WMD, hivyo hatua yangu ya kwanza ni amsha amsha, maana nilikuja kugundua sisi Watanzania ni maneno maneno matupu lakini vitendo sufuri!, Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Hivyo mwaka huu wote wa 2024 ni mwaka wa amsha amsha, na mwaka 2025 ni mwaka wa vitendo, na kisipoeleweka, ni kubutua tuu WMD!.

Mungu Ibariki Tanzania
P
We pimbi. tu
unajikanyakanyaga hueleweki unasimamia nini unasema unapenda haki
Lakini unaogopa kukemea upande flani usiotenda haki
 
Mkuu Drifter ,CHADEMA ina viongozi, wanachama na wafuasi wasiojitambua, wanaojisikia sana, wasiosikia mawazo mbadala, wabishi na wasio na mikakati ya maana, hii ni uongo?. Chadema imewahi kuwa na mikakati gani ya kuingia Ikulu?.

Hili ya karma kuitandika, Chadema, sio tishio ni real!. Kwa vile unaweza kunisoma naamini kabisa unaiona karma inavyo itafuna Chadema, and take it from me, mkifanikiwa kuwatimua hawa 19 bila kuwatimua kwa haki, believe me, the karma consequences will be devastating!. Mlipo mtimua Zitto, niliwashauri Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"... unajua ni nini kiliwakuta wahusika wakuu wote wa kadhia hii, mmoja baada ya mwingine?. Mimi nakijua!, watu mkiambiwa wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii, mnabisha!.

Tena hizo karma, ni cha mtoto, nimewashauri Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu karma yake itakuwa very devastating!.

P

Hawa covid 19 ni wasaliti wa chama hivyo kuwarudisha chamani ni kukiua chama kwani hawa walitumiwa na ccm kufanya vile walivyofanya ; hivyo kuwarudisha tena ni kuwaleta vibaraka wa ccm kuja kukidhoofisha chama!
Unaposema kuwatimua kwa haki una maana gani? Hawa wamekiuka miiko ya chama in other words these 19 women are traitors whose only punishment is EXPULSION!! Uamuzi wowote tofauti na kuwafukuza ndio utakuwa mwisho wa hicho chama!
Mbowe anatafuta njia ya kuwarudisha lakini ni kwa maslahi yake na sio kwa maslahi ya Chadema!!
 
Unaposema kuwatimua kwa haki una maana gani?
Mkuu Bulesi , there you are.
Katiba ya Chadema imeweka utaratibu wa kuwatimua wanachama wake, nimekuwekea katiba ya Chadema ya 2006, hapo chini , kwanini CC ya Chadema imewatimua kinyume cha utaratibu wa kwenye katiba yao?.

Kuwatimua kwa haki ni kuwatimua kwa mujibu wa katiba ya Chadema.

Hata mtu anayehukumiwa kunyonywa, adhabu hiyo inatekelezwa kwa utaratibu.
  1. Baada ya hukumu ya kunyongwa, mtuhumiwa atahamishiwa gereza la kunyongea kwa Tanzania ni Gereza la Isanga.
  2. Huko gerezani, huwekwa chumba cha peke yake, na hafanyi kazi yoyote zaidi ya kula na kulala.
  3. Mfungwa huyo hupatiwa huduma za ushauri nasaha kumuandaa kwa kifo.
  4. Pia hupatiwa huduma za kiroho kwa mujibu wa imani ya dini yake ili kumuandaa kwenda kukutana na muumba wake.
  5. Nakala ya hukumu hupelekwa Ikulu kutayarishiwa Death Warrant ambayo lazima Rais wa nchi aisaini ndipo adhabu hiyo hutekelezwa.
  6. Rais akiisha saini death warrant, itaonyesha mfungwa huyo atanyongwa lini, wapi na saa ngapi.
  7. Ndugu wa mfungwa huarifiwa, kuwapa fursa ya kuja kumuaga kabla ya kunyongwa.
  8. Ndugu wa aliyemua hujulishwa kama watapenda kushuhudia.
  9. Siku ya kunyongwa hufanyiwa usafi, shaving, new dress, heavy breakfast.
  10. Kabla ya kunyongwa daktari humpima kujiridhisha yuko fit kiafya, akikutwa na ugonjwa wowote, hata homa tuu, au mafua, adhabu haitekelezwi, anapaswa kutibiwa kwanza apone ndipo anyongwe.
  11. Akikutwa fit, hupewa fursa ya kuaga ndugu zake na kutoa neno lolote la mwisho.
  12. Viongozi wa dini yake humsalia sala ya mwisho, kama ni Mkristo Mkatoliki hupakwa mafuta ya krisma.
  13. Ndipo hunyongwa na kama ni Muislamu hunyongwa kwa kutizamishwa kibla.
  14. Baada ya kunyongwa, daktari hiitwa kuthibitisha amekufa.
  15. Familia hukabidhiwa mwili kwenda kuuzika.
Huo ni utaratibu.
Kumfutia mwanachama uanachama wake ndio capital punishment kwenye chama lazima ufunyike kwa uangalifu na umakini kwa mujibu wa katiba ya Chadema. Kwanini haukufanyika?.
Kwa faida ya wasio na uwezo wa kuisoma katiba, nimewawekea hivyo vifungu hapa

Kwa Vile Kamati Kuu ya Chadema Imewaita Kina Halima Mdee ili Iwahoji, na Wamegomea Mwito, Naomba Kuwaletea Vifungu vya Mamlaka ya Nidhamu Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema.

6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za kinidhamu:-
6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama Uongozi na Vikao vya Tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa Tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.
6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza: (haya ni masherti ya vikao vya nidhamu)
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu ya maandishi katika muda usiopungua wiki mbili. (Mashitaka ni kwa maandishi na Majibu ni kwa maandishi na sio kuitana kienyeji enyeji)

(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
(d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa ( kwenye issue ya kina Halima Mdee, kulikuwa na uharaka huu?.) isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa Ibara ya 5.4 ya Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.
6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.
6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au
6.5.9 Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha maamuzi.

Sasa kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa kama nilivyo zianisha hapo juu, jee zilifuatwa?
  • Kwa nini CC ya Chadema, inawaita watu kihuni huni tuu, bila kuandaa hati ya mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
  • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
  • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
  • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, kugomea wito huo wa kienyeji wa kufika mbele ya Kangaroo court iitwayo CC ya Chadema ambapo CC hiyo inapokaa kama a Kangaroo court, kazi yake huwa ni moja tuu, kuchinja bila kueleleza Kibla!. Ukichinja bila kuelekeza Kibla, kunahesabika ni kunyonga. Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!.

Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!

Paskali
 

Attachments

Central committee ya Chadema ina mamlaka ya kutoa uamuzi kwa niaba ya vikao vya chini yake! Hivyo sikubaliani na wewe kuwa walikiuka utaratibu kwani kuna mambo mengine yanahitaji kuamriwa kwa haraka kutokana na unyeti wake; under those emergency conditions , the highest organ can make decisions ili mambo yasiharibike!!
 
Central committee ya Chadema ina mamlaka ya kutoa uamuzi kwa niaba ya vikao vya chini yake! Hivyo sikubaliani na wewe kuwa walikiuka utaratibu kwani kuna mambo mengine yanahitaji kuamriwa kwa haraka kutokana na unyeti wake; under those emergency conditions , the highest organ can make decisions ili mambo yasiharibike!!
Mkuu Bulesi, kwanza nikupongeze tena kwa objectivity yako, kwasababu ni wachache sana humu wanaozijua emergency powers za CC ya Chadema to overrides the roles of Baraza Kuu na Mkutano Mkuu in case of emergency.

Nimekupongeza kwasababu kwanza hizi emergency powers za CC ya Chadema, hazikuwepo kwenye katiba ya Chadema ya 2006 wakati wanamtimua Zitto. Hivyo Zitto Kabwe hakutimuliwa kwa haki na wahusika wakuu wote wameisha kula karma zao according to their roles.

Baada ya utimuaji haramu wa Zitto ndipo Mkutano Mkuu wa Chadema ukafanya mabadiliko madogo ya katiba na kukasimu mamlaka ya kusimamisha mwanachama yoyote incase of emergency.

Ila pia kuna kanuni za application ya hizo emergency powers, there has to be a serious emergency situation that needs urgency action, ukichelewa kuchukua hatua, will worsen the situation!.

In this case
1. Appointment letter kutoka Chadema imekwenda NEC kuwateua.
2. Barua za uteuzi kutoka NEC kwenda bungeni zimepelekwa.
3. Bunge limewapokea limewaapisha hivyo tayari ni wabunge halali,

Kuna emergency gani hapa to warrant and justify the use ofvemergency powers za CC ya Chadema?. The harm was already done, ukiwatimua kwa haraka, unakuwa umezuia nini?. Ukisubiri na kutumia the normal process ungeharibu nini?.

Tukubali tukatae, Chadema kuna udhaifu mkubwa kwenye kufuata katiba yake, na nilisema The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia!

Mimi ni Mzee wa masauti na karma, naendelea kusisitiza tiba salama ya kulimaliza hili kwa amani ni Chadema is left with only two options
1. Ifanye a due process of doing things right kwa kuwatimua kwa haki kwa mujibu wa katiba ya Chadema
Or
Wawasamehe.
Wakristo walioko Chadema ile sala ya Baba Yetu sijui huwa wanaisali kwa mazoea tuu kama wimbo but they don't mean what they pray?!

P
 
Watu hawamwelewi Pascal Mayalla kwa hoja

Pascal kwa utaalamu kidogo anakabiliwa na hali (si ugonjwa) unaoitwa ''temporary amnesia'' yaani kupoteza kumbukumbu kwa muda ndiyo maana anakumbuka ya Kitila, Zitto , Mwinyigamba n.k. waulize Wasukuma !
Mkuu Nguruvi3, with due respect, kufuatia huu ugonjwa wa temporary amnesia, due to ile ajali yangu, naomba kwa heshima na taadhima, nisijibu hoja zako kwa sasa, kwa sababu hii amnesia yenyewe ni temporary tuu, ikiisha na kumbukumbu kunirudia, nitakuja kukujibu, ila kiukweli hili la amnesia, linanifikirisha sana!.

P
 
Mkuu Nguruvi3, with due respect, kufuatia huu ugonjwa wa temporary amnesia, due to ile ajali yangu, naomba kwa heshima na taadhima, nisijibu hoja zako kwa sasa, kwa sababu hii amnesia yenyewe ni temporary, ikiisha kumbukumbu zikinirudia, nitakuja kukujibu ila kiukweli hili linanifikirisha sana!.

P
Mkuu usichukulie kwa namna tofauti, So sorry ikiwa nimekukwaza lakini intention haikuwa mbaya. Nafuta bandiko na pole
 
Back
Top Bottom