Uchaguzi 2020 Wana Mbeya Tumekukataa Mh. Tulia

Uchaguzi 2020 Wana Mbeya Tumekukataa Mh. Tulia

Hii nimeichota sehemu...

TULIA HATOSHI, NI KIRUSI KINACHOIGAWA CCM MBEYA

Mh. Tulia Ackson kazungukwa na watu wa ovyo. Kwanza ana haraka sana. Kitendo hiki kinawakera Mbeya tofauti na yeye na watu wake wanavyodhani.

Sawa anaweza kuwa mgeni kisiasa. Lakini hawezi kuwa mgeni wa hulka za wana Mbeya. Spidi yake inachefua kuliko kuvutia.

Amepania kubeba bendera ya CCM Mbeya mjini 2020. Lakini harakati zake zinapingana na ukweli halisi. CCM tukichanga karata vibaya 2020 tutasaga meno. Hili halihitaji mnajimu wa nyota.

Anataka kura za watu anaojitenga nao. Magari na ving'ora, misafara na mapikipiki ya nini Mbeya? Watu unaotaka wakupe kura zao hutaki wakukaribie. Unawaogopa wapiga kura wako?

Tulia hatakiwi hata kupandisha vioo vya gari akiwa Mbeya. Siasa ya Mbeya ni ngumu sana kwa sababu watu wanajielewa.

Hata askari anaowatumia hawalipwi posho. Na yeye hawapozi hata na maji ya kunywa. Utasema ni kazi yao kulinda viongozi. Lakini tambua pale anataka kuwawakilisha mpaka hao polisi.

Siasa hufanya kiongozi awe mtumwa wa wapiga kura. Tulia anataka wapiga kura wawe watumwa wake. Ni ngumu kumuuza 2020.

Tunajua anataka Uspika. Lakini Mbeya ya sasa inahitaji uwakilishi wa Mbunge mwenye mashiko. CCM tusimamishe mtu anayeuzika.

La sivyo hatuwezi kupambana na Chadema ya Mbeya yenye Sugu, kwa kumtumia Tulia. Tunajidanganya wana CCM, hilo litakuwa zoezi gumu kuliko lile la 2015.

Mh.Tulia ameigawa CCM. Kuna CCM 'Team Sugu' wa kimya kimya. Anamharibia hata Mh. Rais kwa kujinasibu kuwa kamtuma. Mbeya hawapendi kuburuzwa na hawataki mtu aliyetumwa, au tumesahau ya Bruno Mpangala?

Tulia hana muunganiko (connection) na Mbeya Jiji. Hata nyumba ya kuishi kaanza kujenga hivi sasa ili kuhalalisha achagulike. Tujue kwamba Mbeya sio wajinga. Hawawezi kuacha kumchagua Sugu, kwa sababu ya mgombea anayewaza Uspika. Tutachemka.

Lazima chama kiwe na watu wanaouzika. Wenye mashiko ndani ya Mbeya. Tukiwa vichwa ngumu kwa kushupaza shingo zetu. Sugu atarudi bungeni kwa kura nyingi zaidi kuliko rekodi yake ya 2015.

Ndimi mwana CCM,
Edwin Mwakanyamale,
Forest Mbeya.
Ikiwa mwaka 2020 kutakua na wawakilishi wa mamba bungeni basi mchagueni tu huyo bibi maana anafaa zaidi kuwakilisha mamba kwa muonekano wake!
 
Due to her arrogance of higher level she will fail miserably,she is doing everything possible as deputy Speaker to please Mr President to have mercy on her to clinch Mbeya town Constituency but that is never easy coz mbeya is cosmopolitan city with knowledgeable educated people, not brainwashed as she might think,better this Woman humble herself and respect all people regardless of their political affiliation,
Prides comes before fall
 
Sisi tunasimama na Tulia . Naona kama uchaguzi unachelewa Dr Tulia achukue jimbo
 
Due to her arrogance of higher level she will fail miserably,she is doing everything possible as deputy Speaker to please Mr President to have mercy on her to clinch Mbeya town Constituency but that is never easy coz mbeya is cosmopolitan city with knowledgeable educated people, not brainwashed as she might think,better this Woman humble herself and respect all people regardless of their political affiliation,
Prides comes before fall

Jitahidi kuandika Kiswahili mwana ukiandika kingereza unaboronga Adjective juu ya adjective
 
Hivi si ninasikia Ameandaa timu ya kuhonga elfu 30 maeilayani ili Watu wafanye maandamano ya kumuunga? Ananunua utu. Wamepita chunya na Mbalali wakiwaomba watu wajifanye yeye ndiye figure ya Mbeya. Kuna kijana nasikia anania ya kugombea Mbeya anamtia presha huyu dada. Vipi mumeshamrudishia billion 4 zake?
 
Mbunge aliyesajiliwa dirisha dogo kama Le Profeseli
Kama liprofrseli macho kodooo[emoji116]
Macho%20kodo.jpeg
 
HUYO TULIA AENDE AKAGOMBEE KWAO TUKUYU MBEYA MJINI TULISHAGA WAKATAA WANYAKYUSA WANA VIDOMO DOMO SANAHALAFU NI AIBU KUONGOZWA NA MWANAMKE MJI MKUBWA KAMA MBEYA,AKAONGOZE WENZAKE WA MWAKALELI HUKO TUKUYU SIO MBEYA
 
Kama mkitaka maendeleo mbeya nendeni na Tulia coz anaushawishi mkubwa kwenye serikali hii ya awamu ya Tano, ila kama no ushabiki basi zichangeni karata deny vintage.
Umeongea point kubwa kabisa
 
Ukiona mtu anaacha hoja za msingi anaongelea small issues ujue umeishiwa eti mwanamke.. kumbe ht katika familia yenu unamdharau mama yako kwasababu mwanamke, eti mji mkubwa huu utalinganisha na bunge mbona ni naibu spika,
 
Alete maendeleo kwa mlango wa nyuma kwani wapigakura watakuwa wanamuinamisha maendeleo yanatokea nyuma?
mm nakapenda kamama kale, kanajitolea sana hata kama kanataka kugombea mm naweza kukapa kalete maendeleo hata kwa mlango wa nyuma tu
 
Sio kweli kuwa na ushawishi ni kigezo kwa serikali hii.Dar walipiga chini ccm pamoja na kura za uraisi.lakini kuna miradi luluki ya maendeleo na mkuu wa mkoa ametamka hadharani juu ya hilo kwahiyo tupunguze upotoshaji.yeyote atayepitishwa na chama chake ni sahihi.
Kama mkitaka maendeleo mbeya nendeni na Tulia coz anaushawishi mkubwa kwenye serikali hii ya awamu ya Tano, ila kama no ushabiki basi zichangeni karata deny vintage.
 
huyo labda awe mbunge wa ikulu maisha yake yote ila kwenye sanduku la kura hapiti.
Mkuu usisahau kitu kimoja. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM hahitaji kushinda uchaguzi ili kutangazwa kuwa mshindi. Kuna DED mmoja aliniambia wale wabunge wa upinzani waliotangazwa kushinda ilikuwa hivyo kwa ajili ya sababu mbili - moja angalau kuonyesha upinzani nao wanashinda hasa sehemu ambazo ilikuwa wazi upinzani wana nguvu zaidi, pili ni kwa kuwa CCM hawakuwa wanamuona mgombea wao kuwa atawasaida sana akiwa mbunge.

Kwa hiyo suala la Tulia kugombea ubunge ni formality tu, matokeao tayari yanajulikana; Sugu atapata kura zaidi lakini Tulia atapata Ubunge.
 
Ushawishi anao ndiyo kakarabati shule kongwe loleza kaomba fedha zimeongezwa loleza na iyunga: Kakarabati kituo cha afya Mwanjelwa serikali imeongeza fedha zaidi alimuomba waziri mkuu siku ya ziara akakubali
Kaomba wamachingabwatumie eneo la Airport Rais kakubali
 
Mkuu usisahau kitu kimoja. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM hahitaji kushinda uchaguzi ili kutangazwa kuwa mshindi. Kuna DED mmoja aliniambia wale wabunge wa upinzani waliotangazwa kushinda ilikuwa hivyo kwa ajili ya sababu mbili - moja angalau kuonyesha upinzani nao wanashinda hasa sehemu ambazo ilikuwa wazi upinzani wana nguvu zaidi, pili ni kwa kuwa CCM hawakuwa wanamuona mgombea wao kuwa atawasaida sana akiwa mbunge.

Kwa hiyo suala la Tulia kugombea ubunge ni formality tu, matokeao tayari yanajulikana; Sugu atapata kura zaidi lakini Tulia atapata Ubunge.
means hata ikitumika figisu atabaki kuwa mbunge wa Ikulu kwasabab order ya hiyo figisu inatoka Ikulu.

Then huyo DED kwa swala la Mbeya kakuongopea au hajui tu kuwa SUGU alipata kura nyingi kuliko mbunge yoyote hapa Tanzania, unaanza wapi kumkata mtu wa namna hii??
 
Back
Top Bottom