Wana-Simba, mwaka huu ndiyo umeisha; tusubiri usajili wa mwakani

Wana-Simba, mwaka huu ndiyo umeisha; tusubiri usajili wa mwakani

Mwaka huu ni mwendo wa kupapaswa tu, nyumba kipigo, ugenini kichapo.
 
Najua nitaitwa majina yoote hapa, "shabiki maandazi, hujui mpira wewe, ushawahi kucheza mpira?unachangia sh ngapi"

Kwa kweli ikitokea simba ikachukua ubingwa wa ligi basi itakuwa miujiza mikubwa sana na kufika robo fainali ya CAF itabidi ifanywe sherehe kubwa sana.

Aiseee, eiiish , uuuuuwiiiiiii draw au kufungwa siyo sababu ni kwamba team inachezaje? Israel mwenda kichwa chake kimejaa makamasi , he is a thick head, hivi mna hakika anajua hata kusoma na kuandika yule jamaa?

Hapo kuna watu wanaona bora duchu aendelee kuwepo kwa mkopo ila huyu mwenda aendelee kula mshahar a wa bure hapo sitaki kuongelea suala la NAMBA 6 NA NAMBA 9 ambalo kwa mwaka mzima walikosa wachezaji barani afrika wa kusajili.

Oh GOD
Mkuu ulitaka namba 9 gani tena ilihali mzungu Geogevic yupo.

Kama namba 6 mbona yupo Akpan.
 
Usajili wa maana Simba uliondoka na mwamba HANSPOPE (RIP). Akitumwa kwenda kumsajili mchezaji pesa aliyopewa ikiwa pungufu anaongeza ya kwake ya mfukoni. Morison alisajiliwa Simba na HANSPOPE kutoka Yanga miezi kadhaa kabla ya usajili rasmi muda wote huo akipewa kila kitu na Pope. Walichokifanya Babra na Magori anayeenda Uganda mara mbili mbili kuomba apunguziwe bei ya Manzoki utafikiri Manzoki ni tenga la maembe wakati Simba ina mamilioni kama sio mabilioni ya udhamini kutoka makampuni mbali mbali sio kuleta utani kwenye mambo "serious".

Simba ilikuwa na jicho la mwewe kwenye usajili kwa kuona mafundi hasa wa mpira kuanzia kwa Adebayor, Sylla, Aziz Ki, Manzoki, Ngomo lakini mwisho wa siku wote hao hata mmoja hajasajiliwa Simba pamoja na mahaba mazito walioonyesha wazi mitandaoni Manzoki na Adebayor kwa Simba. Ukiangalia Simba ya sasa hivi kwenye usajili haina tofauti na Asernal ya mzee Wenger kwani alikuwa na uwezo wa kufuatilia wachezaji wengi bora duniani lakini sasa linapokuja suala la uhamisho analeta ubahili matokeo yake wachezaji wanaenda timu nyingine.
 
hata siku ya yanga alimchosha sana inonga kwenda kupokea vipasi njiwa vyake, yaani hata ukimuangalia usoni ni kama akili hazijatimia vizuri kufanya maamuzi kwa haraka hawezi kabisa mipira ya kutoa kurusha yeye anatoa backpass na siku zote pass zake ni njiw huwa zinakomea njiani
Ana makosa Ila sio kwamba kichwani hazijatimia.
 
Dogo kukaba hajui, kupandisha timu kwake ni mtihani, kucheza pasi hajui yani sijui yupo pale Simba Sc kutimiza majukumu gani tu.

Cha kushangaza eti ndio backup tegemezi ya Kapombe, daaaah..! Hapo Simba Sc akiumia Zimbwe na Kapombe ujue hakuna team tena.
Karia yupo, wakiumia hao mechi za Simba zitaghairishwa mpaka wapone.
 
Dogo kukaba hajui, kupandisha timu kwake ni mtihani, kucheza pasi hajui yani sijui yupo pale Simba Sc kutimiza majukumu gani tu.

Cha kushangaza eti ndio backup tegemezi ya Kapombe, daaaah..! Hapo Simba Sc akiumia Zimbwe na Kapombe ujue hakuna team tena.
unazungumzia Kapombe na Zimbwe waliochoka! Zimbwe bado ana maluweluwe ya tobo la Aziz Ki na lile goli alilosababisha Taifa Stars!!
Inonga nae majanga tu promo kibao Mayele akaipasua Simba goli mbili safi mbele yake!! Beki za Simba zote uchochoro tu!
 
Back
Top Bottom