Wana-Simba, mwaka huu ndiyo umeisha; tusubiri usajili wa mwakani

Mwaka huu ni mwendo wa kupapaswa tu, nyumba kipigo, ugenini kichapo.
 
Mkuu ulitaka namba 9 gani tena ilihali mzungu Geogevic yupo.

Kama namba 6 mbona yupo Akpan.
 
Usajili wa maana Simba uliondoka na mwamba HANSPOPE (RIP). Akitumwa kwenda kumsajili mchezaji pesa aliyopewa ikiwa pungufu anaongeza ya kwake ya mfukoni. Morison alisajiliwa Simba na HANSPOPE kutoka Yanga miezi kadhaa kabla ya usajili rasmi muda wote huo akipewa kila kitu na Pope. Walichokifanya Babra na Magori anayeenda Uganda mara mbili mbili kuomba apunguziwe bei ya Manzoki utafikiri Manzoki ni tenga la maembe wakati Simba ina mamilioni kama sio mabilioni ya udhamini kutoka makampuni mbali mbali sio kuleta utani kwenye mambo "serious".

Simba ilikuwa na jicho la mwewe kwenye usajili kwa kuona mafundi hasa wa mpira kuanzia kwa Adebayor, Sylla, Aziz Ki, Manzoki, Ngomo lakini mwisho wa siku wote hao hata mmoja hajasajiliwa Simba pamoja na mahaba mazito walioonyesha wazi mitandaoni Manzoki na Adebayor kwa Simba. Ukiangalia Simba ya sasa hivi kwenye usajili haina tofauti na Asernal ya mzee Wenger kwani alikuwa na uwezo wa kufuatilia wachezaji wengi bora duniani lakini sasa linapokuja suala la uhamisho analeta ubahili matokeo yake wachezaji wanaenda timu nyingine.
 
Ana makosa Ila sio kwamba kichwani hazijatimia.
 
Karia yupo, wakiumia hao mechi za Simba zitaghairishwa mpaka wapone.
 
unazungumzia Kapombe na Zimbwe waliochoka! Zimbwe bado ana maluweluwe ya tobo la Aziz Ki na lile goli alilosababisha Taifa Stars!!
Inonga nae majanga tu promo kibao Mayele akaipasua Simba goli mbili safi mbele yake!! Beki za Simba zote uchochoro tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…