Mleta mada usisahau kusifia kiwango bora kabisa cha beki namba 2 wa As Vita Djuma Shabani
Huyu jamaa kwenye michuano ya CHAN aliwapeleka puta sana mabeki wa Libya mpaka Congo ikapata goli dakika za lala salama
Hvyo kiuwezo kamzidi mbali Tshabalala, na kwenye mpira team work ndio kila kitu,, ndo maana Miquissone ilimlazimu awe anashuka chini kumuongezea nguvu Tshabalala
Cha msingi tu ni kumkumbusha Tshabalala kwamba hao ndio aina ya mabeki au winger atakaokutana nao ktk hii michuano, sio wale aliowazoea wa Mwadui au Ihefu ambao hata kutuliza mpira hawajui,,, hvyo Tshabalala aongeze umakini zaidi