Wana Simba SC tutaje wachezaji tunaoona hawatufai msimu ujao

Hakuna ubishi kocha ndio mwamuzi.. haya ni maoni yetu mashabiki wala sio sheria.
Waliopo bongo wanajadili ya Liverpool a/u Man u utawaambiaje??
Uwanjani tunaingi na Jezi tunanunua.. tulia kama hayakuhusu
Mkuu kwa mfumo wa simba sahivi kocha anatoa tu mapendekezo but kuna kamati maalumu ambayo ndo inatafakari na kutoa maamuzi ya mwisho....kwa taasisi kubwa kama simba huwezi kumwachia tu eti kocha ndo awe kila kitu kwenye swala kubwa kama ilo...mi napendelea kuona boss wetu moodewji akishirikiana na wataalamu wachache wa mpira atakaowachagua ndo wanakuwa waamuzi wa mwisho...jamaa ana ipenda sana simba na anawekeza hela nyingi so moja kwa moja hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye usajili wakati kawekeza pesa nyingi
 
Kumbuka hata sisi tunaenda viwanjani na tunaona viwango vyao
 
Tamaa mmezidi mkuu! Kwasi na Salamba tuliwataka, kwa kuwa mna mawe mkawadaka! Mmeshauwa vipaji vyao sasa hamuwataki!
Viwango wanavyo, ila kwa simba inayotaka kutwaa taji LA Africa, viwango vyao vimeshuka
 
Jamaa hapo juu hajui washabiki wana nguvu gani kwenye timu...
Lakini ukweli benchi la ufundi, bosi na wataalam wengine lazima washirikiane.. Kuboresha timu.
 
Makocha siku zote wanasema wanataka nani kwenye team iwe ni kiungo, beki, mshambuliaji, kipa

Na hata kuwataja kwa majina kabisa kama amewaona tayari katika team alizokutana nazo

Kazi ya watoa fedha ni kutimiza mahitaji ya mwalimu aliyoyatoa
 
Mkuu mwalimu anatoa mapendekezo but mwisho wa siku kamati maalumu ndo inaamua....hiyohiyo kamati ndo wenye maamuzi ya mwisho...hata kocha mwenyewe yupo chini ya iyo kamati so inaweza kumuona hata yeye hafai ikamuondoa na kutafuta kocha mwingine....kwenye kipindi cha usajili ni kipindi ambacho hata kocha mwenyewe hajui hatima yake..anaweza temwa kama wanavyotemwa wachezaji mfumo siku zote huwa hivyo
 
Ajibu na Gadiel kutoka timu gani?? Acha kuota.. Hakuna Mchezaji atakayeondoka Yanga kama Zahera anamuhitaji.. Eti Kabunda baba yake kavuja jasho na damu Yanga.. mwenyekiti Yanga Kasema timu inaenda Germany kwa marafiki zake mjipange
 
Timu itaenda ujerumani kwa kuchangishana hizo bukubuku mnazokusanya kwenye mabakuli???mkuu simba ikitaka kumsajili mchezaji yoyote yanga inamchukua tu bila ubishi wowote...mchezaji gani anayependa kuchezea timu ambayo inachangishana bukubuku ndo alipwe mshahara...najua roho inakuuma na nafsi haitaki kukubaliana na ukweli but yanga mpo kwenye hali mbaya...wakina kakolanya wenyewe wameona bora wapoteze msimu bila timu kuliko kuendelea kushinda njaa pale Yanga
 
Ajibu na Gadiel kutoka timu gani?? Acha kuota.. Hakuna Mchezaji atakayeondoka Yanga kama Zahera anamuhitaji.. Eti Kabunda baba yake kavuja jasho na damu Yanga.. mwenyekiti Yanga Kasema timu inaenda Germany kwa marafiki zake mjipange
hahaaa yaani team inapelekwa Germany kwa marafiki wa mwenyeki

Yanga mmeishiwa
 
Bora ww umewaelimisha maana wengi naona kale kajina ka Rage kamewapendeza sana
 
Hakuna ubishi kocha ndio mwamuzi.. haya ni maoni yetu mashabiki wala sio sheria.
Waliopo bongo wanajadili ya Liverpool a/u Man u utawaambiaje??
Uwanjani tunaingi na Jezi tunanunua.. tulia kama hayakuhusu
Jitafakari kama unatosha kupendekeza hayo kisa tu unaingia uwanjani na kununua jezi za klabu...poor Tanzania football fans ....
 
Huyo Gadiel nae ni walewale vibeki vifupi fupi hivi haviaminiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…