Wacheji wa Simba wa kimataifa ninaowaona wana madhara wakiwa uwanjani
1. CC Chama
Anafunga magoli, aongeze bidii, hana kasi, afanye mazoezi ya kukimbia kwa kasi.
2. Okwi
Anafunga magoli ajifue zaidi,
Aongeze pumzi za dakika zote 90 mchezoni. kama anaanza kukata pumzi mapema.
3. Kagere
Anafunga magoli, aongeze bidi ya mazoezi, uzito unamnyemelea ajifue zaidi.
4. Gyan
Bado mdogo, anauwezo mzuri wa kukaba na kumiliki mpira na hata kupiga chenga, kama atajiamini atakuwa mzuri zaidi msimu ujao.
5. Niyonzima ..!
Anaweza ila ana mbwembwe nyingi zisizo na maana, hafungi magoli, hasongi mbele sana anapenda kuzungukazunguka na mpira,
angekuwa siriaz angekuwa bora zaidi, hakabi, hana madhara. inampasa kujirekebisha sana.
6. Kotei ..!
Huyu ni kiraka na anakaba sana, anaweza fikiriwa kama hakuna mbadala mwingine.
7. Juuko ..!
Kama ataacha kucheza rafu anaweza fikiriwa tena ila aongeze bidii, huwa wakati mwingine anajisahau uwanjani.
8. Kwasi ..!
Kiwango chake kimeshuka ghafla, hafiti sana kwenye mipango ya baadae ya Simba.
9. Zana ..!
Ni mchezaji mzuri ila naona anatatizo la Umri mkubwa kuweza kukabiriana na mikiki ya mechi za kimataifa, hakabi vizuri, hana kasi kuendela na kasi ya ukabaji. Anaweza kuondoka.
10. Wawa ..!
Ni mchezaji mzuri ila umri umemtupa mkono.
Anaweza kucheza timu yenye malengo ya kushinda ligi ya ndani. Kimataifa hawezi kushindana na kasi ya akina Kampamba na Makusu.
Ova.