Wana Simba SC tutaje wachezaji tunaoona hawatufai msimu ujao

Wana Simba SC tutaje wachezaji tunaoona hawatufai msimu ujao

Nakumbuka Tambwe alidaka mpira akawechini akafunga.. Kambuzi akasema peleka mpira kati.. aahaa aahaa.
Mpira mchezo mgumu sheria zake zinatungwa na Waingereza. . Hivyo mediocre hawezi kuelewa.. Handball na ball to hand
 
Simba wanatakiwa wawe makini sana kwenye usajili. Wasilete mchezo wa mazoea kwenye kufanya usajili maana ndicho kilichotugharimu kwenye champion legue. Ila kama wana lengo la kutawala vizuri kimataifa mwakani basi waangalie kwa jicho la 3 katika usajili.
 
Mkuu kadi hadi sasa kwa taarifa nilizonazo tunazo watu si chini ya 12000 hadi 15000 hivi...kati ya hao unakuta wanaolipia kadi zao kila mwaka ni watu 500 hadi 1000 unategemea timu itaendelea vipi hapo mzeee???? ok wewe unakadi sawa,,kadi yako mara ya mwisho kulipia ilikuwa lini?kama sio kwenye mkutano wa juzi ???
Mkuu watapinga tu lakin hoja zako zimesimama sana ,na nimegundua wewe ni mshabiki maumivu haswa yaani mpira unakukata maini!
Big up ngoja na mm nifanye mchalato wa kadi nailipia 10yrs
 
Simba ni sehemu salama ya kuua vipaji vya wachezaji! Daah yaan jembe kama Mbonde ndio lishapotea! Kwasi, Mo, Salamba, Mlipili ..........Then mbabaishaji kama Manula eti anacheza!
Kama hafai timu ya taifa anafanya nn,
 
Mikaia utazani mnachangia hata Shillingi 100.
Wakati mpaka mwanaume acheke half wa kiume mshangilie.
 
Wacheji wa Simba wa kimataifa ninaowaona wana madhara wakiwa uwanjani

1. CC Chama
Anafunga magoli, aongeze bidii, hana kasi, afanye mazoezi ya kukimbia kwa kasi.

2. Okwi
Anafunga magoli ajifue zaidi,
Aongeze pumzi za dakika zote 90 mchezoni. kama anaanza kukata pumzi mapema.

3. Kagere
Anafunga magoli, aongeze bidi ya mazoezi, uzito unamnyemelea ajifue zaidi.

4. Gyan
Bado mdogo, anauwezo mzuri wa kukaba na kumiliki mpira na hata kupiga chenga, kama atajiamini atakuwa mzuri zaidi msimu ujao.

5. Niyonzima ..!
Anaweza ila ana mbwembwe nyingi zisizo na maana, hafungi magoli, hasongi mbele sana anapenda kuzungukazunguka na mpira,
angekuwa siriaz angekuwa bora zaidi, hakabi, hana madhara. inampasa kujirekebisha sana.

6. Kotei ..!
Huyu ni kiraka na anakaba sana, anaweza fikiriwa kama hakuna mbadala mwingine.

7. Juuko ..!
Kama ataacha kucheza rafu anaweza fikiriwa tena ila aongeze bidii, huwa wakati mwingine anajisahau uwanjani.

8. Kwasi ..!
Kiwango chake kimeshuka ghafla, hafiti sana kwenye mipango ya baadae ya Simba.

9. Zana ..!
Ni mchezaji mzuri ila naona anatatizo la Umri mkubwa kuweza kukabiriana na mikiki ya mechi za kimataifa, hakabi vizuri, hana kasi kuendela na kasi ya ukabaji. Anaweza kuondoka.

10. Wawa ..!
Ni mchezaji mzuri ila umri umemtupa mkono.
Anaweza kucheza timu yenye malengo ya kushinda ligi ya ndani. Kimataifa hawezi kushindana na kasi ya akina Kampamba na Makusu.

Ova.
 
Huo sio uwekezaji sasa, hivyo ni vitu vinavyotokana faida za uwekezaji,

Ukisema utumie yote kufanya hivyo vitu hata haiwezi kutosha hata uwanja wa watu elfu 30 tu hupati
We ndo wasema..Ila inatosha kama lutakuwa na mipango mathubuti...na kuepukana na wachumia tumbo..
 
Mkuu watapinga tu lakin hoja zako zimesimama sana ,na nimegundua wewe ni mshabiki maumivu haswa yaani mpira unakukata maini!
Big up ngoja na mm nifanye mchalato wa kadi nailipia 10yrs
Pamoja sana mwana...SIMBA SC forever
 
WANOONDOKA NI..JUUKO NA GYAN WANOENDA YANGA.KWASI,WAWA,DIDA,MBONDE.SALAMBA ANAENDA MKOPO...WAFANYE WAFANYAVYO KAHEZA ARUDI WING YA KUSHOTO BADO RASHID JUMA HANA MAAMUZI KABISA YA MWISHO ZAIDI YA KUKIMBIA
vipi maendeleo ya kaheza huko leopard?
 
Hapa rwanda kuna vijana watatu hatayi sana
Ulimwengu jules na michael sarpong wanachezea Rayon sport hatari sana hawa vijana
Pia kuna Hakizimana muhadjri wa Apr nae si wa kawaida
Uongozi ujaribu kutupia macho huku
 
Hebu tuwe wakweli uwanja wa watu elfu 30 ni kiasi gani mkuu
Unataka kutuaminisha uwanja was chamazi ule unagharimu bilioni 10 kuujenga?? TP Mazbe uwanja wao umeuona??ule unataka kusema unagharama ya bilioni 50??

No anaweza kujenga uwanja mdogo wa kawaida tu kama.chamazi wenye thamani ya bilioni 2 hadi 8 na bado ukawa mzuri...

Okey..tuseme haiwezekani..lakini pia anaweza kutumia wabia alionao kayika biashara kulifanya hili kwa malipo ya muda mrefu na yenye faida ya riba..
 
Pamoja na Mo kusema tutafanya usajili hatari bado yaonyesha hatuna timu nzuri ya usajili naona jamaa zetu wameingia sokoni kwa kasi sana
Hii habari ya mchezaji wa zanzibar kumtumia ticket hapo zanzibar mtu serius si anaenda mara moja tu mwaka jana tulimkosa feisal hivi hivi kizembe zembe
 
Back
Top Bottom