Wana Simba SC wenzangu acheni Kununua Magazeti ya Mwanaspoti, Tanzania Daima na Nipashe kwani yana Upendeleo kwa Yanga SC

Wana Simba SC wenzangu acheni Kununua Magazeti ya Mwanaspoti, Tanzania Daima na Nipashe kwani yana Upendeleo kwa Yanga SC

Huwa unaangalia kipindi cha Kurasa za mwisho cha Azam tv siku za Jumamosi ambapo huwaalika wahariri mbalimbali wa mgazeti ya michezo kufanya uchambuzi?

Hao wahariri ndiyo wanaosema ya kwamba mashabiki wanaonunua magazeti kwa wingi ni wale wa Yanga! huku wenzangu wa Simba wakiishia tu kusoma vichwa vya habari. Nimeona nikujibu kwa niaba ya huyo mdau uliyemtolea mapovu.
Hii ipo hata kwenye Mabaa na sehemu nyingine za starehe,siku Yanga ikishinda vinywaji vitanyweka vingi na ofa zitatolewa za kufa mtu lakini Simba ikishinda hawanunui kitu ni maneno matupu tuu na stori
 
Hii ipo hata kwenye Mabaa na sehemu nyingine za starehe,siku Yanga ikishinda vinywaji vitanyweka vingi na ofa zitatolewa za kufa mtu lakini Simba ikishinda hawanunui kitu ni maneno matupu tuu na stori

Wanapiga mkwara mbuzi na wakati wahariri wa magezeti karibia yote wamekiri udhaifu wa mashabiki wa Simba kununua magazeti, zaidi tu ya kupenda kusoma vichwa vya habari na kutembea!

Sasa wanawataka hao waandishi na wahariri wa hayo magazeti wakate mikono ambayo inawalisha? Hata ningekua mimi nisingefanya hivyo. Kama vipi wanunue gazeti lao la Simba tu na hayo mengine yatendelea tu kununuliwa hata kama watasusa.
 
Wenye magazeti siku zote wanajua, wanunuzi au wateja wao ni mashabiki wa Yanga. Ndugu zetu wa Simba labda itokee tu.
 
Hata hivyo Simbwa SC muko wachache sana, kwahyo hata msipo nunua yataisha tu. Hahahahaha........
 
Brother sisi simba sio watu wa magazeti hilo liko wazi kabisa.. yanga wananunua sana magazeti sanasana timu yao ikifanya vizuri..washabiki wa simba wengi akili zao ni advanced huwa wanasoma habari zaidi kupitia internet na sio magazetini na ndo maana tuna Simba app ambayo yanga hawana. ndala huwa wananunua sana gazeti simba ikifungwa au gongo wazi ikishinda lakini washabiki wa simba wengi wameidharau yanga na wala hawafuatilii habari zake kama yanga wanavyofuatilia za simba.. hata hivyo mikaratasi ya nini brother?? tembelea simba app upate habari motomoto
IQ ndogo..wazungu wananunua magazeti ..unaweza kushindana nao kwa technology...Rage apewe tuzo ya heshima kuwaita Mbumbumbu
 
Cleverbright, magazeti yapo kibiashara zaidi licha ya kuhabarisha,,hivyo ukiona habari za watani zetu zikiandikwa kwa mapambio zaidi maana yake mashabiki wao ndio wanunuzi zaidi kuliko sisi wanamsimbazi.

Hii pia nilishaisikia kwenye kipindi cha wahariri wa magazeti ya michezo kikirushwa na Azam Tv siku za weekend, wanasema Yanga akifungwa magazeti hayauzi lakini siku akishinda biashara huwa nono.
Habari ya Yanga kuwa bingwa tpl itauza zaidi magazetini kuliko ya Simba kuwa bingwa CAF-CL
Hili nalifahamu tangu mwaka 1991.
 
Ni sahihi ..ila timu yao ikiwa vizuri hujitokeza kwa wingi kuliko Simba...
Sasa kama hadi iwe vizuri ndio waingie uwanjani, basi kumbe mwaka au msimu huu wote wa ligi wataingia wachache sana
 
Sasa kama hadi iwe vizuri ndio waingie uwanjani, basi kumbe mwaka au msimu huu wote wa ligi wataingia wachache sana

Hayo ni mawazo yako...msimu ndiyo kwanza umeanza tusubiri tuone...
 
Tatizo huwa unaendaga nunua gazeti ukiskia yanga kafungwa ndo maana unakutana na balaa ila simba akifungwa hununui by the way acha kampeni ya kuchafua kazi za watu wewe kama ni agent wa magazeti like msimbazi, champion and so on tafuta style nyingine ya kutangaza biashara yako na si kuharibu kazi za watu mother........ fu.........!
 
Back
Top Bottom