Hee, mbona matusi tena. Au kwa kuwa Jf tunaingia kwa ID fake, waweza kuta ni ndugu yako. Mimi nilithani umeanzisha huu uzi kwa nia njema kuwakutanisha ndugu zako ili siku nyingine mfikie kuonana uso kwa uso. Nami kwa kuwa nimeona baadhi ya vijiji umekosea majina, nikaona nikushauri uombe ushauri zaidi kuhusu majina ya vijiji na maeneo husika. Kwa mfano hakuna kijiji kinaitwa Nyamongo bali hilo ni eneo lenye vijiji vya Murwambe, Kewanja, Nyangoto, Matongo, Kemambo na Kerende. Umetaja Bwirege lakini bado ukataja Nyamwaga ilihali Bwirege ni mkusanyiko wa vijiji vya Nyamwagaa, Keisangora, Komerama, Kimusi, Muriba, Nyantira, Nyansicha, Kumwika, Itiryo, Genkuru n.k yaani hata 50 vinafika. Ulichoita Mgoto sio bali Magoto. Sasa kuwa kuwa nimeona upungufu katika ujumbe wako, nikaona tuuweke sawa ili uwapate watu husika. ..............kumbuka nimeandika hivi:.......Mkuu, hakuna vijiji vyenye hayo majina, kama ulihitaji watu kutoka vijiji husika. Hii inaonyesha wewe sio mzaliwa wa eneo hilo bali ulikaa kwa muda au unalisikia tu. Omba ushauri zaidi. .......kulikuwa na sababu gani ya kumwaga mitusi kiasi hicho.