Wana-uchumi: Dollar ndiyo inatumika katika manunuzi karibu Dunia nzima. Niaminishe USA ha-print pesa na kuzisambaza soko la dunia kupitia manunuzi!!!

Kwa hiyo suala ni trust?
Haiprint pesa zake ili kulinda trust kama nimekupata vizuri?
 
Point uliyoieleza ni kuwa

Marekani ha-print pesa zake maana akifanya hivyo zitarudi marekani . Itasababisha kuwa na mfumuko wa bei.

Sio pesa zote zinarudi marekani.... mataifa kariba yote yanafanya biashara kutumia dollar. Sisi tukitaka kununua kitu South Africa tunawapa Dollar.

South africa akitaka kununua kitu Japan anatumia Dollar. Utagundua hizi pesa nyingi hazimrudii mmarekani zinabaki kwenye soko la dunia.
 
Suala lingine.....
Marekani akiprint pesa...pesa yake ikawa nyingi duniani kiuchumi thamani inashuka. Right!

Hii binafsi kwa common sense itaapply kwa vinchi kama Zimbabwe ambavyo vipesa vyao vinatumika ndani ya mipka ya nchi. Nchi nyingi zinazalisha watu hawalali huko Asia bidhaa zinazalishwa nyiingi saana ....Marekani akiweza kubalance uhitaji wa Dollar na uzalishaji wa Dunia ataendelea kujipigia.

Maoni binafsi.
 
Kwa hiyo suala ni trust?
Haiprint pesa zake ili kulinda trust kama nimekupata vizuri?

Upo sawa,Trust na Confidence ndio kitu kikubwa na muhimu sana. Lakini pia kulinda uchumi wa USA ,ajira, biashara, bei kupanda hovyo kwa assets kama za nyumba, huduma kama za afya, elimu, stock markets, assets bubles. Kiufupi ni suala linaloathiri kila sekta ya uchumi.

Msingi wake mkuu ni trust and confidence katika uchumi wa USA, unajionyesha kupitia currency na uchumi ambao upo stable. Hauyumbiyumbi kama Banana Republic. Hivyo kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
 
Sawa sawa.

Uaminifu wa pesa unaletwa na nini ...hadi wawekezaji na watumiaji wa pesa waiamini pesa ?
 
Unipata vizuri kabisa. Kama kuna uhitaji mkubwa duniani wa dollar USA anaweza kuprint money na bado uchumi wake ukabaki imara. Hiyo inamaanisha uchumi wa Dunia umeongezeka kwa hiyo dollar inahitajika ili biashara zifanyike.

Lakini bado itaonyesha kwenye bei za vitu zitapanda kama gold, stock markets, interest rates, gharama za uzalishaji, usafiri, chakula, imports nk.
 
Sasa swali langu nani anafaidika hapa?

Si nchi maskini zinamfanyia kazi USA?

Wewe mwenyewe unajua uchumi wa vinchi maskini kama Tanzania uchumi ukikua kidogo waliowengi wanakimbilia liabilities....hivyo kwa hii formula tutaendelea kubakia maskini hadi tunazikwa.
 
Sawa sawa.

Uaminifu wa pesa unaletwa na nini ...hadi wawekezaji na watumiaji wa pesa waiamini pesa ?
Uaminifu wa pesa unaletwa na kama uaminifu mwingine wowote kwenye kitu chochote.

Kutekeleza makubaliano, vitu ulivyoahidi siku zote bilaa chenga, kutoa taarifa ya mipango yako mapema, kuwa muwazi, mkweli, serious kutobadilisha mawazo ghafla na kutoshtukiza watu.

Nchi zinakopa ili kufanya maendeleo, kuna nchi kadhaa ambazo ukiwakopa una uhakika utalipwa kwa wakati bila zengwe lolote. Kuna nchi hazijawahi ku- default, kushindwa kulipa mikopo yao. USA mmoja wao.

Mfano ukiwekeza bilioni moja US dollar wanasema watakulipa faida milioni 50 kila mwaka kwa miaka 30 watafanya hivyo bila kukosa kwa sababu yoyote ile na baada ya miaka 30 unapata mtaji wako.

Kama inflation itakuwa kubwa sana bilioni moja yako itakuwa na thamani ndogo sana baada ya miaka 30. Kwahiyo ili ku-maintain value ya dollar inabidi kuthibiti inflation, kiwango cha kushuka thamani kwa pesa ili wawekezaji waendelee kuwa na imani na uchumi wako na pesa yako. Pia itabidi uwalipe interest kubwa, ili kuwavutia na kuwafanya wasikimbie nchi na kuwekeza nchi nyingine au assets class zingine.
 
Kwa nchi kama za kwetu inabidi kuwa na umoja wetu. Kama USA tuwe na United States of Afrika. Hapo inabidi kufanya biashara pamoja na kuwa na our own currency, inayoweza kuwa back up may be by gold, something tangible therefore inakuwa vigumu kuyumbishwa.

Kingine ni kuongeza value added exports badala ya kuuza malighafi.

Ukiangalia mfumo wa sasa pesa nyingi inapelekwa USA, China, Japan, Uarabuni na Ulaya. Chache sana inatumika Afrika na kubaki Afrika kufanya shughuli za maendeleo. Nyingi inarudishwa Ulaya, China, USA, uarabuni kupitia njia nyingi, kununua mafuta, gasi uarabuni, magari Japan, kukopa Mabenki ya USA, kuweka pesa zetu kwa mabenki ya huko ili iwe salama, kufanya shopping, utalii, pamoja na kupata huduma za elimu, afya kununua vitu, finished products kutoka China.

Mfumo wetu wa sisi kuuza vitu malighafi kwa bei ndogo na kununua vitu finished products kwa bei kubwa unatufanya tuendelee kubaki maskini.

Hatuna monopoly or competitive advantages kwenye sekta yoyote. Hatuzitambui competitive advantages zetu. Mfano DRC, Tanzania, Botswana. South Afrika na zingine zinaweza kuaanzisha organisation kama OPEC ambayo kazi yake ni kulinda bei ya mafuta ila ya kwetu ikawa kulinda bei za madini na maslahi ya nchi wazalishaji.
 
Nipo hapa kupata madini muhimu ambayo hatupati vyuoni kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…