Tuanzie hapa wadau wengi wanahitaji dollar ili kununua USA assets, kama Bonds, Tresuary bills, stocks eg Tesla, Google, Apple, Amazon stocks, propeties na vitu vingine USA. Wengi wanawekeza USA ili kupata kipato cha uhakika cha mara kwa mara.
Uki-print money ukatumia kwenye nchi nyingine kwa mfano ambazo ziko hizo base inamaanisha unaongeza imports, dollar money supply kwenye hiyo nchi na nyingi zitarudi USA kununua vitu.
Mfano USA aka-print dollars atumie UAE. Atatumia vipi? Labda kununua silaha, huduma kwa wanajeshi wake kama chakula, afya, mafunzo, makazi nk.
Huduma kadhaa zinaweza kuwa zinatolewa na local people zingine na kampuni za USA mfano ununuzi wa silaha, mafunzo huduma za afya. Kwahiyo hilo pesa itarudi USA kupitia hapo.
Pia central bank za UAE zinaweza kuamua kutumia excess dollars kununua assets USA kama bond, stocks ili ku-maintain local price and currency stability, pesa yao mfano Dinar isipande thamani sana na kuifanya bidhaa zao zisiwe competitive. Pia hizo central bank zinaweza kuzirudisha USA kuwekeza kupata regular, predictable income.
Kumbuka kwenye vikao vya FED, ni lazima watoe taarifa juu ya inflation target yao, interest rate, money supply, hizo taarifa zitakupa mwanga FED ina- print money kiasi gani.