Kiukweli hawa kina hersi na bumbuli wanatuona sisi mashabiki vitoga, sijapenda.
Kama mnavyojua mimi ni yanga lia lia (haters watabisha) naona kabisa kuna point ya kuzingatia kutoka kwa mleta mada ambaye naye kimsingi ni yanga (haters watabisha tena)
Namimi nimeona niweke mawili matatu
Baada ya kuona makolo wamepoteza mechi wakaona sasa huo ndio muda sahihi kutema shombo zao, niliupenda ule ukimya uliojitokeza baada ya kutolewa na azam kule zenji
Walijua kwamba kile kipindi hakikuwa sahihi kwa wao kuongelea habari hizi za 29,000 wakasubiri gubu ituishe wajianze upya.
Yanga yetu hii haikuwahi kuwa na mfumo huu wa kutoa kauli zisizo na staha kwa mashabiki, lakini tumeanza kushuhudia haya baada ya kukaribisha kirusi kutoka kwa wahasimu wetu
Sasa nasema hii timu ni ya wananchi, GSM kuwekeza vibukubuku alivyovipata kwenye vigodoro vyake isiwe sababu ya kutuona sisi ni mazuzu, au kwakua tunaongoza ligi basi ndo watufanye mandondocha kwamba wanatupelekesha watakavyo, nasema hiyo haiwezekani tutazua utata zaidi ya vagi la machinga kuchomewa soko lao