Wana Yanga SC wenzangu Kura zetu zote tumpe Profesa Mshindo Msolla na Tajiri Eliud Mvela Siku ya Uchaguzi Mkuu Jumapili Kesho Kutwa

Wana Yanga SC wenzangu Kura zetu zote tumpe Profesa Mshindo Msolla na Tajiri Eliud Mvela Siku ya Uchaguzi Mkuu Jumapili Kesho Kutwa

Genta muhuni sana,karusha furushi LA nyuki gheto LA Yanga halafu kakimbia anasikilizia tu Yanga wanavyopiga mayowe
 
Wanayanga tusiyumbishwe tufanye maamuzi sahihi ambayo yataitoa timu hapa ilipo!! Hata Mzee Akilimali nae alituambia tumchague Igangula na akatuambia ndio atatutoa tulipo mwisho wa siku Igangula kakimbia aibu!
 
Nikiwa kama Mwana Yanga SC naomba tumchague Profesa Mshindo Msolla kama Mwenyekiti wa Timu yetu na Eliud Mvela kama Makamu wa Mwenyekirti. Siku ya Jumapili nami GENTAMYCINE nitakuwepo pale Police Officers Mess katika Kupiga Kura yangu hivyo kama Wewe ni Mwana Yanga SC mwenzangu usiniangushe tafadhali na kwa pamoja au umoja wetu tuwachague hawa Watu niliowataja hapa.

Ukiona Kitu chochote GENTAMYCINE anakipenda basi jua ' Kimebarikiwa ' hadi na Mwenyezi Mungu na Malaika wake akina Jibrili na Mikaela hivyo Siku ya Jumapili nitawadharau mno Wana Yanga SC wenzangu kama hatutowachagua akina Mshindo Msolla na Eliud Mvela Kutuongoza.

Nina uhakika kama wana Yanga SC wenzangu wote tutawapa hawa dhamana Kuu juu ya Klabu yetu basi Kombe hili la Ligi Kuu tunabeba, lile la ASFC tunabeba, Kombe la Kagame tunabeba, Kombe la Mapinduzi tunabeba na Kombe la Klabu Afrika tunabeba pia kwani Simba SC wamebahatisha tu na wala hawatuwezi ng'o.

Na mkiwachagua hawa Mshindo Msolla na Eliud Mvela wana Yanga SC wenzangu Simba SC tena hii mbovu mbovu kabisa haitotufunga tena ila mkiwachagua tu Wagombea wengine mtakuja Kujuta na Kunikumbuka Mimi mwana Yanga SC mwenzenu GENTAMYCINE.

Na kuhusu Ubingwa wa Ligi ( TPL ) wala wana Yanga SC wenzangu msiogope au kuwa na Hofu yoyote ile kwani Simba SC hawatutishi kabisa kwani Mechi zao Kumi ( 10 ) zilizobaki kuanzia hii ya leo wanaenda Kufungwa zote. Ila yote haya yatatokea kama tu mkiwachagua akina Mshindo Msolla na Eliud Mvela hiyo Siku ya Jumapili.

Naomba kila mwana Yanga SC hapa Mtandaoni JamiiForums ' aifowadi ' hii ' thread ' yangu kwa wana Yanga SC wote na isambae upesi na hakikisheni mnawaambia kuwa mwana Yanga SC mwenzao Mimi GENTAMYCINE nimesema wasiniangushe hiyo Jumapili tafadhali.

Naipenda mno na sana Klabu yangu ya Yanga SC na hata wana JamiiForums wote hapa wanalijua hili.

Nawasilisha.


Ndugu yangu title ya Msolla mgombea wa Yanga ni 'Doctor' na siyo 'Professa'...ila ni kweli kaka yake ni Professa na ambaye aliwahi kuwa Waziri...ila huyu mgombea wa Yanga ni Dr. Msolla na nadhani 'udaktari' wake ameupata baada ya kusomea na kufanya utafiti wa kitu kinachohusiana na 'soil science' kama sijakosea...
 
Back
Top Bottom