Wana-Yanga tusikubali matumizi mabaya ya fedha ya klabu. Kama Ally Kamwe yupo, Mzee Manara anarudi kufanya nini? Mbona Simba Ahmed Ally anatosha?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Naona kazi ya usemaji babu yetu Mzee Manara na yeye kaiingilia, yaani kazi iliyofanywa kwa ufanisi na weledi mkubwa, leo anaongezwa mtu mwingine.

Leo katika mkutano na wanahabari, yaani ikawa mvurugano tu, hamna consistency. Vitu vichache wamejaa wasemaji wawili. Vionjo vya Ali Kamwe vina miksa ya utaalamu wa ndani kabisa, lakini vionjo vya Manara ni vya wale wanaouza bidhaa kwa minada ya benki au wale wauza mitumba wa mitaani wenye vispika.

Kamwe aliuondoa usemaji kutoka hali ya zamani ya usema hovyo, kuwa package kamili ambayo ina proffessionalism.

Mbona Ahmed Ally ni jeshi tosha kabisa kwa upande wa Simba? Huyo Manara wa nini?

Mimi nimemuangalia leo, sura ina makunyanzi, ishara tosha kabisa kwamba huyu ni mzee wa miaka kama 55, anakaribia kustaafu, watu wengi wa Tanzania ni vijana, unawaletea lizee kama hilo badala ya kijana mwenzao?

Manara alikuwa anaenda kucheza muziki enzi za Moro Jazz, Cuban Marimba, na Marijani Rajabu, ndio ataelewama na hawa vijana?

#bwawaLimeingiaRuba
 
Mkuu angalia utamchongea Ally Kamwe apigwe miba na huyo mjinga ni mshirikina hatari sana.
 
Wanasimba mmeshaanza kuweweseka tarehe nane nahisi hamtatokea uwanjani kabisa. Na kama mnajua hamtatokea andaeni hela za faini na adhabu kwa TFF ili msifungiwe
 
Naona kazi ya usemaji babu yetu Mzee Manara na yeye kaiingilia, yaani kazi iliyofanywa kwa ufanisi na weledi mkubwa, leo anaongezwa mtu mwingine.
1. Msemaji wa Club
2. Mhanasishaji wa Club

Wamegawana hapo kule Ahmed Ally ana mwenzie Ila yule mwenzie sio Domotenga hajui kubwabwaja akiongea ni Maneno mawili matatu siku ya uzinduzi wa Jezi alikuepo kuhamasisha pale Makumbusho kabla hawajaelekea Mikumi

Ally Kamwe alikua anapiga 2 in 1 msemaji pia mhanasishaji, umeelewa Bwana we (in Mzee Magoma's Voice)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…