Wana Yanga wenzangu kinachoenda kufanyika Sudan na Al Hilal siyo mpira ni vita!

Sasa kwa Yanga hii ya akina Morrison, ndiyo ya kufanyiwa vurugu kweli! Waoneshe huo mchezo, wasioneshe! Bado kwa upande wao hautakuwa mchezo mwepesi hata kidogo.

Lolote linaweza kutokea kwa Yanga ya msimu huu.
Hawa waarabu siyo kama ni wagumu kiviile, ndiyo maana wanaanza mikwala mapema,ila mlikosea sana kuwaacha salama hapa, mngewapiga kama migoli mitatu bila wangelegea hata hizo amsha amsha zao zisingekuwa na nguvu. Hawa wanajua wakiwadindia mkatoka sare tasa tu wamepita.
 
Kaz ya Caf ni.kuhakikisha mbungi inapigwa uwanjani na si kuoneshwa kwenye Kideo..
Hivi mfano kwa wenzetu ulaya Man city wanaweza kuzuia mechi yake na Dortmund Tv zisionyeshe kweli?
 
Mmechelewa kutambua kwamba mpira wa afrika ni vita. Chakufanya mtumeni injinia akatafute mlango wa uani wa nyie kuingilia uwanjani😂😂😂 mkipita lango kuu mtakua mmekiuka masharti ya mganga wenu
 
Reactions: BRN
Ukipita huko utakutana na comment mbalimbali ila wewe umechagua hii kwakua inakufariji, hiyo comment moja sio mtazamo wa mashabiki wote wa Al Hilal.
 
Wewe kweli ni Achimwene[emoji23]
 
Hii CAF nayo ni ya hovyo kabisa. Kwanini isisimamie suala la matangazo au kulazimisha timu/nchi kuonyesha jamii ili dunia nzima ione haki inavyotendeka? sasa wanaziachia clab zijiamulie kuna siku wachezaji watauawa uwanjani na hakuna ushahidi
Caf hizi match hawana mpango nazo wao huanza kuzisimamia haki ya matangazo ya televisheni kuanzia makundi. Ndo maana kuna hela nyingi uuko
 
Unapotaka kumuua kunguni zima taa
 
Unahamisha magoli siyo! Wewe sema tu hao waarabu wenu koko wameingiwa na mchecheto.

Na kwa bahati nzuri wanatambua fika Yanga imesheheni wachezaji wenye uzoefu na mashindano ya kimataifa. Hivyo hawawezi kutoka kirahisi tu mchezoni kupitia hizo mind game zao.
 
Ni kawaida ukitaka kumshinda adui yako lazima umpe vitisho ili kumdhoofisha na kumuua kisaikolojia

Rejea mabondia na wapigana mieleka utajua

Suluhisho ni Yanga kujiamini na kupambana kufa na kupona
 
Hawa jamaa wanaihofia Yanga kiasi hiki? Mimi nilidhani ni makolo peke yao kumbe hata Hilal wanahofu ya kukutana na suprise ya ajabu wasije aibika pia ni kwa ajili ya wao kufanya upuuzi wao kwa kigezo cha mpira wa Africa.

Nonsense Hilal huu upuuzi ushapitwa na wakati weka gozi uwanjani waache wasio uwanjani nao wa enjoy football.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh wangeacha tuu tuone wanavyofumuliwa magoli mengi. Any way wameshapata kisingizio tayari cha kusema kuwa wameonewa n.k
😁😁😁 Kuwa serious aisee! Hii Yanga ya sasa ni ya kufumuliwa magoli mengi kweli!! Yaani kama ile simba ya khamsa khamsa!!

Kwa taarifa yako, Yanga ya msimu huu ni tamu zaidi ikicheza viwanja vya ugenini, kuliko hata pale kwa Mkapa.
 
Sio kwamba wanawahofia la

Hapo ni kama wanazoofisha na kuwaua psychologically usishangae wakaongeza vitisho zaidi ili wachezaji kuwatia wasi wasi
 
Sasa hapo vita ikowapi..unajua vita wewe..nenda Ukraine huko..
 

Mnajipa presha bure, Nabi ameshaifundisha hiyo timu, anaijua vizuri.
Nabi alipokua Merrekh alikuwa ni kibonde wa Hilala mpaka pale alipokuja kufurushwa baada ya kupoteza draw na Simba Sc huko Sudan kwenye CAFCL.
 
Imagine mchezaji kama Bernard Morrison, eti unamtishia nyau! Aisee anakumaliza. Yaani hao Wasudan waombee Nabi aanzishe tu kikosi dhaifu!

Ila akipanga kikosi chake kwa usahihi, kiukweli uwezekano wa kufuzu ni mkubwa sana.
 
Sasa wale mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wanasema Al Hilal ameridhika na matokeo ya kwa Mkapa na kuwa kule kwao wata defense ili wapate sare ya 0-0 wao wavuke naona wameanza kugundua hawakuwa sahihi

Mimi naamini hii mechi itaoneshwa live, kinachofanywa saizi hapa ni figisu za kuwatoa mchezoni ili focus yao katika kipindi hiki ipotee kwenye kuhangaikia kwenye maswala ya broadcasting

Na sio hivyo tu, wataweza kutengeneza propaganda nyingine ambazo zitaingia kwenye rotation katikati ya hili sakata ambalo wana dili nalo saizi.

Hayo yote yatafanyika wakati Yanga bado yupo hapa hapa Tanzania, unaweza ku imagine watakutana na figisu za kiasi gani wakifika huko.

Yanga na mashabiki wake wanapaswa waelewe kuwa timu pinzani haiwezi ikafanya hayo yote kwa lengo la kutafuta sare tena ikiwa nyumbani.
 
Umeliweka vizuri hili kabisa..wasome hapa
 
Nabi alipokua Merrekh alikuwa ni kibonde wa Hilala mpaka pale alipokuja kufurushwa baada ya kupoteza draw na Simba Sc huko Sudan kwenye CAFCL.
Ila baada ya kuja kwa wananchi, akaanza sasa kuwaangushia vipigo mfululizo! Mkijitutumua, basi ni sare!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…