Wanaanga walioko ISS washindwa kurudi ardhini. Mlango wa Boeing hautaki kufunguka

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Wanaanga wawili wa kimarekani kutokea shirika la anga la NASA wameshindwa kurudi nyumbani kwa wakati kutokana na chombo walichotumia kufika huko cha Starliner kilichotengenezwa na kampuni ya boeing kuwa na hitilafu kadhaa.

Hitilifu kubwa zaidi ni mlango wa kutokea na kuingilia kugoma kufunguka.Tatizo hilo limepelekea safari hiyo ya kurudi kuongezewa muda zaidi huku muda wa chombo hicho kubaki angani wa siku 45 tu ukizidi kupungua.
Mmoja ya wanaanga hao ni dada mmoja mzoefu wa safari hizo aliyewahi kuwavutia sana wafuatiliaji kutoka duniani alipokuwa akifanya maonesho ya televisheni moja kwa moja kutoka chombo hicho.Huyo ni Suni Williams.

Mpaka kufikia kufanikiwa kwa safari hiyo ya starliner iliwahi kuakhirishwa mara nyingi kutokana na hitilifu zilizokuwa zikijitokeza dakika za mwisho kabla ya safari kuanza.

Katika moja ya majaribio yaliyofanyika miaka ya nyumba ya chombo hicho kiliwahi kushindwa kuingia kwenye oribit iliyokusudiwa na kikaa kwenye eneo hilo mpaka pale kilipofanikiwa kurudishwa ardhini salama.

Astronauts stranded in space due to multiple issues with Boeing's Starliner — and the window for a return flight is closing

 
Boeing isingekua kampuni ya kimarekani sasa ingekua imefilisika kabisa,vyombo vyake mpk sasa vimeua watu wengi mno plus kinachowalinda ni kua ni wamarekani ingepigwa kila aina ya vikwazo na isingeuza chochote US and EU,na bado itawapoteza wengi tu wanadami
 
Kwa sayansi ya dunia najua wakishindwa warusi watachukua nafasi ya kuwarejesha duniani lakini pia hiyo kandarasi wangewapa bibi zangu wa Simiyu mbona chapu tu hakuna helcopter zinatembea kama zile
 
Mwana naona umetu bebabeba kama viroba
 
Chombo cha Starliner kilichoundwa na kampuni ya Boieng hatimae kimeweza kuaondoka kutoka kituo cha anga cha ISS lakini bila kuwabeba abiria wake wawili kutokana na hofu za kiusalama baada ya chombo hicho kupata hitilafu tangu kiwasili huko.

Wanaanga wawili wa kimarekani mmoja mwanamume aitwaye Butch na mwengine mwanamke aitwaye Sunni Williams wataendelea kubaki kwenye kituo hicho mpaka mwezi Februari mwakani ambapo chombo kingine cha Space X kinatarajiwa kupelekwa kuwarudisha nyumbani. Wanaanga hao tayari wameshakaa muda mrefu huko kinyume na muda waliopangiwa kukaa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…