SoC02 Wanaangamia kwa kukosa maarifa

SoC02 Wanaangamia kwa kukosa maarifa

Stories of Change - 2022 Competition

1998Calvo

New Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
4
Reaction score
5
Wanaangamia kwa kukosa maarifa

WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA​

Ni miaka sitini imepita tangu uhuru upatikane. Watanzania wanaendelea kuishi kwa kuambiwa na kutenda kwa kuongozwa. Ni wachache wanaoamini “Elimu ni ufunguo wa maisha.” Theluthi ya wanaojiita wasakatonge, wanawakejeli na kuwabeza walio na vyeti kabatini. Wengi wao wanasema kuwa elimu ya sasa haimsaidii mtu kama hana wa kumshika mkono. Nafasi za kazi zilizopo serikalini na katika jamii zimekuwa zikijazwa na ndugu wa wafanyakazi pasipo kuangalia nani anaweza nini na anashindwa nini.

Jamii imekosa maarifa. Wananchi wamashindwa kujikwamua kimaisha kwa kutumia elimu na ujuzi walio nao. Wamekuwa wakilalamika na hasa kuisema serikali yao. Wanatamani chama tawala kitoke madarakani wakiwa na imani na utawala mpya wa wapinzani. Wamesahau kuwa wapinzani pia ni watu na wanatamaa ya madaraka kama mimi na wewe.

Ni kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa. Viongozi wa serikalini, dini na wananchi kwa ujumla, wanaangamia na kuiangamiza jamii kwa kukosa maarifa. Kwa namna moja au nyingine kila kundi limekuwa likilipoteza kundi lingine.
1663073956357.png

Wanaangamia kwa kukosa maarifa

VIONGOZI WA SERIKALINI​

Viongozi wa serikalini wamekuwa mstari wa mbele kuiangamiza jamii. Imani yao juu ya wanachokijadili na wanachokipitisha bungeni imekuwa gumzo kwa wananchi.

Kwanza kabisa, wanaamini wananchi hawawezi pasipo wao. Hii ni imani kubwa sana wanayoishikilia. Ni kweli jamii haiwezi pasipo wao ila si wanavyofikiria. Jamii imewachagua ili waweze kuwawakilisha bungeni juu ya matatizo yao ila si kujibeza na kutunisha vifua. Viongozi wa serikalini wanachagua nini cha kufanya na kwa muda gani wafanye kazi. Hata jamii ilalamike vipi wamekuwa wakionekana siku za kampeni na sikukuu muhimu za serikalini. Wanasahau kuwa pasipo jamii hakuna kiongozi. Kwa namna hii wamepoteza muelekeo, kwani hawajui nini wazungumze, nini watetee, na nini kinahitaji kurekebishwa.Kimsingi, hawajui maana kubwa ya uwepo wa jamii.

Viongozi wa serikali wamekuwa mstari wa mbele kuahidi wasichoweza kutimiza. Viongozi wamekosa maarifa kwani hawana mbinu za kuishawishi jamii. Wengi wanaahidi maisha mazuri, maisha ya siagi na asali. Kipindi kizima cha kampeni wanaonekana wakitoa misaada, na kulazimika kushika jembe na vifaa vingine vya kazi kuzibua vyoo na mitaro, ilhali wakiibuka washindi wanapotea pasipojulikana. Huu ni ukosefu wa maarifa. Kwa nini jamii idanganywe ili mradi lengo ni kujenga maendeleo ya nchi? Kwa nini kuidanganya nafsi yako wakati wajua wananchi wanaitaji maisha mazuri? Viongozi wanahitaji kubadili mtazamo wao.

Vile vile, viongozi wanaamini maendeleo hayawezi kupatikana bila wananchi kulipa tozo. Sina maana kuwa jamii haihitaji kulipa tozo. Ni imani yangu kuwa nchi hii imeongozwa tangu tupate uhuru bila kodi ya kichwa. Maendeleo yalikuwepo na bado yanaonekana. Maisha yalikuwa mazuri na hakuna ambaye hakufurahia pasipo wachache ambao walilalamika kuonewa na mabavu. Kodi zinafaa kulipwa bila shuruti na sheria kali ifatwe kwa yeyote asiyelipa. Swali ni “Je, kila huduma itolewayo lazima ilipiwe kodi?” Serikali haitakiwi kupitisha kitu kwa sauti za ndio nyingi. Kodi zilipwe kwa huduma maalumu kwa kujali hali halisi ya maisha. Zaidi, kama lengo ni kuijenga nchi, bado najiuliza, “Ni lini viongozi wataanza kulipa kodi?” Serikali inatakiwa itambue kuwa kadri nchi inavyoendelea maisha ya wananchi yanatakiwa yaimarike. Zaidi, serikali inatakiwa itambue kuwa maendeleo ni mipango baina ya serikali na jamii nzima.

VIONGOZI WA DINI​

Viongozi wa dini wanachangia kuiangamiza jamii kwa namna mbalimbali ambazo wanadai si kwa kupenda kwao.

Wamekuwa wakichochea ghasia kwa kuitaka jamii iamini kuwa dini zao ni nzuri kuliko za wengine. Viongozi hawa wameupotosha umma kwa kulinganisha dini moja na dini nyingine. Hii imepelekea jamii kukosoana na kulumbana wakizitetea dini zao. Jamii imekosa mwelekeo kwani hawajui ni imani ipi ni sahihi ingawa Mungu ni yule yule mmoja. Viongozi wamejikita kufundisha ubora wa dini pasipo kuangalia matabaka yanayotengenezwa. Hawafikirii chuki inayotengenezwa ndani ya roho ya mtu kuhusu dini nyingine.

Pia, viongozi wa dini wamejikita katika maneno na si matendo. Viongozi wa dini wanazungumza yaliyomo katika vitabu vitakatifu ilhali matendo yao ni kinyume na wanachozungumza. Wanadiriki kusema kuwa usifate nachofanya bali tenda Mungu anavyotaka. Wanasahau kuwa matendo yana nguvu kubwa katika kuyajenga na kuyaaribu maisha ya mwanadamu. Kila mmoja anatakiwa ajitahidi kuyaishi maisha yaliyojaa matendo mema. Hasa viongozi wawe mstari wa mbele kutenda kwa mifano kama mitume walivyotenda. Maendeleo ya jamii kwa ujumla yanategemea matendo mema katika kila siku ya Mungu. Kwa kufanya hivi, jamii itakuwa katika misingi mizuri ya kuyaishi maisha ya viongozi wao.

WANANCHI​

Wananchi ni kundi kubwa linaloangamia katika nchi. Wamekuwa katika sehemu ngumu ya kimaisha kuamua nini kizuri na kipi kibaya kutokana na uongozi.

Ni ukweli kuwa wananchi wameshindwa kutambua mazuri na mabaya. Wameshindwa kuutumia uhuru wao wa kusema, kukemea mabaya na kusifia mazuri. Jamii nzima imenyamazishwa na sheria kali za viongozi. Wananchi wanaogopa kuadhibiwa na serikali. Ni rahisi kwa kiongozi kuwasema wenzake ila si kwa raia wa kawaida. Ukiongea ni kosa kubwa la jinai. Usipokuwa makini unapotezwa pasipojulikana na kama ukirudi basi una jambo la kusimulia umma. Hii imewafanya wananchi wengi kuogopa.Wananchi wengi wamejikita kufatilia mambo ya kijamii hasa wanamziki.

Wengine wamejikita kufatilia mapenzi yasiyowajenga wakidai bora maisha yaende. Hivi sasa kauli mbiu ni ,” Bongo si hami.” Hii ni kutokana na mambo wanayoyafanya wasanii. Wengine wanadai kuwa ukifa bongo na “stress” umejitakia.

Vile vile, wananchi wanaamini amani imetawala nchini. Ni ukweli mtupu kusema ivo. Hii ni kutokana na kuamini tunachoambiwa. Ukweli ni kwamba tunajitetea tuna amani kwa kuifananisha nchi yetu na mataifa mengine. Kamwe amani haiwezi kuwepo kama bado tunazungumza lugha tofauti, tunapangiwa nini cha kufanya, tunanyanyaswa na mabavu kwa kutaka madini tunayozalisha sisi wenyewe. Ni lini tutajipangia bei zetu wenyewe? Ni lini tutasimamia rasilimali zetu wenyewe?

Ni lini tutaacha kuonewa na kubambikizwa makosa ambayo si yetu? Tunapaswa kujiuliza ni lini. Taifa halina amani hata kidogo. Kila kukicha afadhali ya jana.

MWISHO​

Kiujumla, Viongozi wa serikalini, dini na wananchi hawana budi kuangalia mienendo yao. Kila kundi linahitaji kujirekebisha kwa njia ya kipekee. Kwa kutambua wajibu wa kila kundi tunaweza kuijenga nchi moja yenye amani, furaha , uhuru wa kukemea mabaya, kusifia mazuri na kutenda yaliyomema. Tusiogope kusema bali tuwe na nia na njia ya kusema. Tusemapo, tutambue tunaongea na nani na tutambue wajibu wetu ni nini na baada ya hapo tunataka nini. Imani yangu ni kuwa tukishirikiana tutaijenga nchi moja iliyo na misingi mizuri ya imani, uongozi bora na wananchi wenye furaha.
 
Upvote 2
Jamani kwakweli yakifuatwa haya niliyoyasoma hapa da! Tutakuwa wa kuigwa na mataifa meng kama sio yote kakaake congratulation👏👏👏👏👏👏
 
Wanaangamia kwa kukosa maarifa

WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA​

Ni miaka sitini imepita tangu uhuru upatikane. Watanzania wanaendelea kuishi kwa kuambiwa na kutenda kwa kuongozwa. Ni wachache wanaoamini “Elimu ni ufunguo wa maisha.” Theluthi ya wanaojiita wasakatonge, wanawakejeli na kuwabeza walio na vyeti kabatini. Wengi wao wanasema kuwa elimu ya sasa haimsaidii mtu kama hana wa kumshika mkono. Nafasi za kazi zilizopo serikalini na katika jamii zimekuwa zikijazwa na ndugu wa wafanyakazi pasipo kuangalia nani anaweza nini na anashindwa nini.

Jamii imekosa maarifa. Wananchi wamashindwa kujikwamua kimaisha kwa kutumia elimu na ujuzi walio nao. Wamekuwa wakilalamika na hasa kuisema serikali yao. Wanatamani chama tawala kitoke madarakani wakiwa na imani na utawala mpya wa wapinzani. Wamesahau kuwa wapinzani pia ni watu na wanatamaa ya madaraka kama mimi na wewe.

Ni kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa. Viongozi wa serikalini, dini na wananchi kwa ujumla, wanaangamia na kuiangamiza jamii kwa kukosa maarifa. Kwa namna moja au nyingine kila kundi limekuwa likilipoteza kundi lingine.
View attachment 2355600

Uzi wa Maana Sana
 
Huu Uzi inabidi uwekwe kwenye vitabu vya dini, na kwenye somo la civics.

Back
Top Bottom