PostGE2025 WanaCCM wengi tumefurahishwa na haya maandamano

PostGE2025 WanaCCM wengi tumefurahishwa na haya maandamano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Baba Kabunyee

Member
Joined
Jul 30, 2024
Posts
11
Reaction score
14
Tanzania mpya imezaliwa tarehe 29/10/2025. Kila mpenda haki amefurahi bila kujali yupo chama gani. Kwa CCM tumefurahi zaidi ila wengi hawataweza kuweka furaha zao wazi kwa sababu mbalimbali ikiwemo unafiki. Mungu awabariki wote waliofanikisha maandamano. Ninawaombea kwa Mungu wote waliopoteza maisha kwenye maandamano pamoja na wale waliopoteza mali zao. Hizo ndo gharama za mabadiliko.

Ninaamini reforms hazitaishia nje ya CCM tu hata ndani ya CCM kutakuwa na mabadiliko. Watu uoga hawana tena. CCM ya chini ya mama ilishaharibika mno. Machawa na watoto wa viongozi walikuwa wakikinajisi chama jinsi watakavyo. Kuna mwanaCCM gani anafurahishwa na jinsi viongozi wa CCM wanavyopambana kurithisha watoto wao uongozi hata kama hawana sifa? Imagine lile toto bonge la Mwigulu lilikuwa mgeni rasmi kwenye tukio fulani huko Singida...!!! Inakera kichizi. Huko Arusha baba ni meya mtoto ni mwenyekiti UVCCM.. Upuuzi mtupu.

Steve Nyerere na machawa wengine wana nguvu kuliko viongozi wengi wa CCM. Inashangaza kuona chawa Steve huwa anakuwa kama mmoja wa maofisa wa ikulu wakati mwingine. Machawa walikuwa wanaziba nafasi za wanachama waliokulia chamani na wenye mapenzi na chama huku wakiwa na sifa zingine za muhimu kama elimu. WanaCCM wengi wamekuwa wakiugulia ndani kwa ndani. Sitarajii kuona mwenyekiti akiendelea kuwakumbatia hawa chawa.

Baada ya raia kuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu ushenzi wa Mafwele na genge lake la wasiojulikana natarajia mwenyekiti na amiri jeshi kumtenga na ikibidi kumchukulia hatua. Huyu Mafwele anatajwa kuumiza kila mtu bila kujali chama. CCM kuendelea kuwa karibu na hawa wauaji haitasaidia kufika 2030 salama.
 
Tunashukuru Mungu nchi imepata Rais, na maandamano yameisha. Sasa ni Rais kuapishwa, kuunda serikali na itakayowatumikia watu wote kwa bidii...
 
Tunashukuru Mungu nchi imepata Rais, na maandamano yameisha. Sasa ni Rais kuapishwa, kuunda serikali na itakayowatumikia watu wote kwa bidii...
Mwambie tunampenda tumempigia kura za kutosha wapinzani wake wako jela basi awashe Internet tunataka kuandamana kwa ajili ya kumpongeza
 
1000187918.jpg
 
kutoka chama cha kisera mpaka kuwa chinja chinja, kuteka na kuua wakosoaji wake, CCM iko shimoni sasa,

Mwenyekiti anaonekana yeye ndiyo mwenye uchu wa madaraka, yupo tayari kumwaga damu ili atawale,

Tumepata Idd Amini mpya Nduli ndani ya Tanganyika.

Bahati mbaya hata wenye hekima nao wapo kimya kukemea haya yanayoendelea.
 
Kwa nini bado uko CCM?
 
Back
Top Bottom