MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Siku 7 zilizopita kuna thread ililetwa hapa ikitoa taarifa kuwa wanaCCM wote wa tawi la Kiterere kata ya Bumera katika jimbo la Tarime wamejiunga CHADEMA baada ya aliyekuwa kiongozi wa kijiji kwa tiketi ya CCM kukatwa jina lake katika kura za maoni ya kuchagua wagombea kwa tiketi ya CCM.
Thread hii hapa;
GONGALINK>>>Heche aendelea kuibomoa CCM huko Tarime
WanaCCM hao wamedai walipatwa na hasira na kufanya maamuzi yasiyo na busara, baada ya hasira zao kushuka wamegundua walichofanya hakifai na wameamua kurudi tena CCM kwa sababu CCM ina uwanja mpana wa mawazo na kutatua migogoro.
Kuna baadhi ya watu na hata wanaJamiiforums walimuonya Heche kuhusu uamuzi wa kuwapokea wanaCCM bila hata ya kufanya uchunguzi kama ilivyotokea kwenye kipindi cha ‘’Mafuriko ya Lowassa’’ lakini hakusikia.
Hii tabia ya viongozi wa vyama vya upinzani ya kusubiri wanaCCM wakatwe kwenye kura za maoni halafu wawapokee itaendelea kuwatafuna mpaka pale watakapojua msingi wa tatizo.

VIDEO YA WALIORUDI CCM WAKISHANGILIA NA KUTOA SABABU ZA WAO KURUDI CCM