GE2025 Wanachama na Viongozi wa CHADEMA wafanya maombi Mahakamani kabla ya Kesi ya Tundu Lissu

GE2025 Wanachama na Viongozi wa CHADEMA wafanya maombi Mahakamani kabla ya Kesi ya Tundu Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wanachama wa CHADEMA pamoja na Viongozi mbalimbali wakifanya maombi ndani ya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kabla ya kuanza kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.


Wafuasi wa Chama cha CHADEMA wamefanya maombi ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.

Maombi hayo maalum ya kumuhusu Lissu yamefanyika hii leo ikiwa kesi hiyo ya uhaini ikitarajiwa kuendelea kwa Upande wa Jamhuri kujibu hoja za Mshtakiwa huyo ambaye ameomba afutiwe kesi kutokana na dosari katika hati ya mashtaka.

Jamhuri itawasilisha majibu hayo mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akisaidiana na Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
 
Mungu wetu ni Mungu wa haki, ni Mungu wa upendo: naye hachelewi wala hawahi bila huyajibu maombi ya mwanadamu amtegemeaye kwa wakati ulio sahihi, na kwa namna iliyo sahihi. Mungu, tunaomba uyasikie maombi ya watu wako wanaodhulumiwa na watawala dhulumati.
 
Back
Top Bottom