Pre GE2025 Wanachama, Viongozi CHADEMA wagawanyika kambi tofauti, hofu ya mpasuko yaongezeka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
wakitaka chadema kife basi lisu apewe uenyekiti hii ni kwa sababu.
1.Lisu hana utulivu
2.Lisu ni mropokaji.
3.Lisu hana uvunilivu
4.Lisu hana uungwana
5.Lisu pumzi imekata kutokana na majeraha.
Kumbe chadema haijafa, nyie misukule ya Samia na magufuli si mliokuwa mnafarijiana kuwa chadema imekufa Leo mnasema wakitaka chadema ife, mizoga bhana.
 
Mbowe ni pandikizi limeshibishwa Rushwa.
 
Ccm bila mambo na polis kwishaaa
 
Mkuu sijakuelewa, kwamba Lissu akigombea uenyekiti ni mpango wa CCM kuisambaratisha Chadema?
 
CCM ni dhaifu sana. Na wao wanajua.

Kama CCM ingekuwa imara, na ingekuwa na uhakika wa ushindi, ingekubali uwepo wa tume huru ya uchaguzi ili ipate sifa hata kwa walimwengu kuwa ni chama kinachosimamia misingi ya demokrasia. Lakini kwa sababu wanajua udhaifu wao, wanaona kuwa namna yoyote ya kuruhusu uchaguzi uwe wa haki, ni kukubali wao kuondolewa kwenye madaraka.

CCM haina chembe ya uimara, siku itakapokuwa na uimara, mara moja itakubali Tume huru ya uchaguzi na uwepo wa katiba mpya. Kwa sasa wanajua kuwa wananchi hawapo upande wao, hivyo wameamua kuwatawala wananchi kwa nguvu, ndiyo maana wamekuwa wakoloni katili kuliko hata walivyokuwa wakoloni wageni.

Kwa sasa hakuna adui mbaya kwa maendeleo na ustawi wa demokradia na haki nchini, kuizidi CCM.
 
Wanaojadili ndio wamepasuka.
Hilo andiko wapinzani wa Chadema ndio wametoa fedha na maelekezo ya kuliandika.
Sasa CHADEMA wao ndio wachague kucheza mziki wautakao ama mziki wachaguliwao na CCM.
 

Mnajifariji baada ya kukataliwa na wananchi na bado hao wagombea wenu kila uchaguz mtawatangaza kwenye defender kila siku wapumbavu nyi

CCM DAIMA
 
Kwa siasa za Sasa LISSU is far better than Mbowe

Lisu anaaminika na Makundi mengi na anaogopwa na CCM pamoja na Dola , ila Mbowe ni mwana kwao

Lisu akiwa Mwenykiti CCM watabadilika sana na nchi itapiga hatua sababu ziko closed (siwezi kuzitaja) kwenye korido za CCM na Dola , threat ni LISU
 
..Ccm wana allergy na tume huru ya uchaguzi, na katiba bora mpya.
Mkuu hawa CCM ndio wanaochomeka hii hoja kuwa kuna mnyukano Chadema kuhusu uchaguzi wa ndani ili kututoa kwenye reli ya Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
HATUTOKI HUKO, ndio maana Mbowe na Lissu hawajatoka hadharani kubishania suala hilo maana ccm wanataka kutupangia mpaka wagombea wetu uchaguzi wa ndani.
Mbona sisi hatuwaingilii mambo ya form moja ya mgombea Urais? Kwani lini Samia aliwahi kuuza sera zake kwa wana CCM kuhusu akiwa Rais atafanya nini?
Kwani kufiwa na mtangulizi ni moja ya CV za kupewa nafasi kupeperusha bendera ya chama?
Womanizer yao kwanza, sisi wetu tutampata tuu kwa demokrasia yetu ya wakati wote!
 
Kama ni kweli,basi Chadema ni maarufu sana kiasi cha kuvutia mijadala mingi hivyo.
 
Mtu asiye na chama huwa haandiki hivi.
 
Mimi sidhani kama Lisu na Mbowe wanaweza wakawa na msuguano wakugombea madaraka labda kuwe na kitu kingine ndani yake. pamoja nakuwa wote wananguvu kwabwa ndani ya chama na nje ya chama lakini hawa watu wanaheshimiana sana na hasa Lisu anamuheshimu sana Mbowe. Chama kikubwa kama hiki safu za uongozi huwa zinapangwa mapema uchaguzi kwa asilimia kubwa huwa ni kiini macho tu. Kwa vyovyote Lisu na mbowe hawawezi kuwekwa pamoja kwenye kinyang'anyiro ya cheo kimoja. Kwanza huo utakuwa uharibifu wa lasilimali watu. Kuhusu Mbowe kuendea au kutoendelea kuwa mwenyekiti ni muhimu aje na hoja nzito kwa sasa, kulalama tu kila siku kuwa tunashindwa kwakuwa CCM wanatumia dola kubaki madarakani hiyo siyo issue tena kwasababu ilo tatizo limeonekana kuwa sugu na siku kwa siku linazidi kuwa baya zaidi na Mbowe na viongozi wake wameshindwa kulipatia ufumbuzi. Kitu kimoja kinacho mfanya Mbowe azidi kuabudiwa CDM ni swala la uwezo wa kupata fedha za kuendeshea chama kwa hiyo kiongozi mwingine yoyote Ambaye atataka kuwania uwenyekiti lazima aweke wazi mikakati yake ya kupata fedha kukiendesha Chama,, Kitu kinachomuogopesha Mbowe kuuwachia uwenyekiti nadhani ni pamoja na madeni na mahesabu mengi ya kubumba ambayo yanaikabili chama, Anataka apate mrithi ambaye ataendelea kulinda maslai yake zaidi kuliko ya Chama ambapo katika hilo Lisu hawezi kukubali. Kwa misingi hiyo, mtafaruku utaanza Pale Mbowe atakapo taka kuanza kuingilia michakato ya Chaguzi hizi za kitaifa. Sina maana Mbowe hafai kuongoza CDM kwa sasa la Hasha, Ila je ananguvu na ushawishi wa kutosha ndani ya Chama kama Mwanzo au lengo lake ni ukubwa na kupata heshima sehemu mbali mbali kwa Cheo chake? Kiongozi mzuri ni yule anayeshawishiwa na wenzake agombee wadhifa fulani siyo yule anayetumia njia za kuwashawishi watu wampe madaraka. Najua hili la vuguvugu la uchaguzi wa ngazi za juu kabisa CDM litapita ila litamipita kwa maumivu makubwa Sana, Watu kama Chacha Wangwe, Zito ni watu walio leta mtikisiko mkubwa kwenye kuwania vyeo hivyo na mmoja hayupo duniani ila mwingine aliaanzisha Chama chake.
Itoshe kusema kuwa kwa sasa kuwania uwenyekiti CDM ni kaa la Moto halishikiki kwa mkono mpaka upate Jaro.
Ila mimi niwaombee CDM kila la kheri ktk michakato yote yakupanga safu kamili ya juu ya CDM, Mimi naamini awe kiongozi mzuri au Mbaya wote wanawekwa na Mungu kwsa Sababu maalum.
 
Kwa kiasi fulani naona pia kama inakuzwa though, maana Mbowe akibaki dikteta, kukiwa na uchaguzi wenye ushindani wanasema mpasuko, yaani chochote wanachofanya ni nongwa
Uzuri wake Chadema yenyewe iko kimyaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…