Pre GE2025 Wanachama, Viongozi CHADEMA wagawanyika kambi tofauti, hofu ya mpasuko yaongezeka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe anapaswa astaafu kwa hiari vinginevyo ataabika, wananchama tumemchoka, tunataka fikra na mtazamo mpya.
 
lisu akipewa ataendelea kubwata kama mwendawazimu na kutukana hovyo.
hana simile yule mdomo mchafu sana
 
Mbowe bado yupo sana umwenyekiti Chadema kwa miaka mitano ijayo. Wenye uchu wa kuivuruga watasubiri sana maana haitakuwa chini ya wanaharakati wanaoweza kuhatarisha maisha yake kwa mihemko itakayompa Msajili wa vyama vya siasa nafasi ya kuichukulia hatua inapokiuka taratibu na miongozo ya vyama vya siasa.
 
Tanzania hakuna mpinzani imara, mwenye weledi, mtulivu, mwenye busara na msimamo kama mbowe.
lisu debe tu
 
Mpe Lissu maua yake. Huyu ndiye mtu anayefaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
 
Ndiyo! Hii ndiyo demokrasia makini inayotakiwa ndani ya CDM ili kiweze kujitofautisha na uchaguzi wa M/Kiti Taifa wa Chama Cha Mahayawani (CCM). Hakuna suala la mila, desturi wala utamaduni wa kumpisha mtu fulani.

Kila mwanachama mwenye sifa ana fursa sawa ya kushindanishwa na watia nia wengine, ili kumpata kiongozi kupitia katiba ya chama. Wasiwasi kuhusu yote yanayo ongelewa kwa sasa ni 'just fear of unkowns" na wala haviwezi kuathiri demokrasia iliyopo ndani ya CDM. Ni lazima mafahali mawili yapambane ili mmoja wao apate kumiliki boma.

Wote wawili natambua wanaijua thamani na gharama ya matokeo ya chaguzi za kidemokrasia. Sidhani kama yatatokea ya Kidume Sugu na yule mdangaji wa Iringa ambaye kwa aibu ya kushindwa akaamua kuingia mitini!
 
CDM wakiacha kufanya mikutano ya hadhara wanaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe ndani na kwenye magroup ya WhatsApp.

Kijiji kikikosa wazee kinakuwa Cha hovyo sana.
 
wakitaka chadema kife basi lisu apewe uenyekiti hii ni kwa sababu.
1.Lisu hana utulivu
2.Lisu ni mropokaji.
3.Lisu hana uvunilivu
4.Lisu hana uungwana
5.Lisu pumzi imekata kutokana na majeraha.
Huyu lazima atakuwa ni msukule wa mzee Mbowe ,tena atakuwa mchagga,
 
CDM wakiacha kufanya mikutano ya hadhara wanaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe ndani na kwenye magroup ya WhatsApp.

Kijiji kikikosa wazee kinakuwa Cha hovyo sana.
Saaa chama kizima kinaongozwa na vilaza kuliko wasomi wenye weledi ambao chadema ni wachache mnoo
 
CCM wanamuogopa Lissu kwasababu ya misimamo yao.
Chama hakigawanyiki na Hii ndio demokrasia yenyewe.
 
Saaa chama kizima kinaongozwa na vilaza kuliko wasomi wenye weledi ambao chadema ni wachache mnoo
Na CCM inayoongozwa na secretary wa form four je?

Mama yenu huyo alifeli form four.
 
Wanagawanyika ama wanagawanywa? Rekebisha kauli yako bwana maana Sisi sote twajua yaliyo nyuma ya hayo yote.

Kama wapinzani hawagawanywi unategemea ushungi anapataje Kula Pepo Tena?
 
Ndiyo! Hii ndiyo demokrasia makini inayotakiwa ndani ya CDM ili kiweze kujitofautisha na uchaguzi wa M/Kiti Taifa wa Chama Cha Mahayawani (CCM). Hakuna suala la mila, desturi wala utamaduni wa kumpisha mtu fulani.
Hadi chawa wakanyagane kiasi ninachoshuhudia humu, Chadema kwa hakika wanatisha...

Eti mgombea wa Uwenyekiti asiwe na mpinzani...hapana, Chadema waliuvuka ushenzi huo kitambo sana.

CCM wamezoea vya kunyonga, vya kuchinja katu hawaviwezi.
 
Kwa hali ya nchi ilipofikia, inahitaji wanaharakati wenye misimamo mikali ili kuwavusha wananchi.

Mwanaharakati halisi ni yule anakosa furaha kwa haki kusinginwa na haoni maana ya maisha katika hali hiyo!!

From above statement, l see investor(Mbowe) and activist (typical politician)(Lissu)
 
Tanzania hakuna mpinzani imara, mwenye weledi, mtulivu, mwenye busara na msimamo kama mbowe.
lisu debe tu
Mbowe yuko makini kama si umakini wa Mbowe JPM angeifuta Chadema kwa kumtumia Msajili wa vyama vya siasa.
 
"Kuna maisha baada ya uchaguzi. Usiseme jambo ambalo litakufanya uwe mtumwa baada ya uchaguzi. ⁠Atakayekubali kushindwa ndiye mshindi.
Nilikuwa sijasoma makala hii ndefu nilipo bandika maoni yangu huko juu. Kumbe ni makala ya gazeti la Mwananchi? Mwandishi wa makala hii bado anao mwendo mrefu wa uandishi wa habari unao someka na kueleweka vizuri.

Lakini, bado sijasoma makala yote. Nimefikia kwenye hayo maneno niliyo nyanyua hapo juu, ambayo yameni shangaza.
Haya maneno kayasema huyo Askofu Bagonza?
Yana maana gani maneno kama hayo? Huku siyo kujionyesha ujinga wa ajabu na kujivunjia heshima mbele za hao unao waelekezea maneno ya namna hiyo?
 
Ni hitimisho zuri la makala ambayo kwenye baadhi ya maeneo ni kama ilikuwa inamwaga sumu ndani ya chama.

Matumaini yangu ni kwamba, wote, Mbowe pamoja na Lissu; lakini hasa hasa Mbowe wataelewa vyema kilicho bebwa kwenye maneno hayo ndani ya hitimisho la makala.

Kuwa kiongozi wa chama kwa muda mrefu kusimfanye Mbowe aonekane kuwa na haki zaidi ya kuwa kiongozi wa chama hicho kuliko wengine ndani ya chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…