Pre GE2025 Wanachama wa CHADEMA Katavi wachapana makonde, Mbowe ashutumiwa kugawa pesa kwa wajumbe

Pre GE2025 Wanachama wa CHADEMA Katavi wachapana makonde, Mbowe ashutumiwa kugawa pesa kwa wajumbe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona hatujaona makonde hapo

Ova
Umeona wanakunywa bia na kukumbatiana sio?
Hiki Chama kinajaribu kuleta migogoro ya kidini nchini. Kulikuwa na sababu gani kumtuma yule Mzee wenu wa BAZECHA Kuongea yale Maneno?
 
Andiko lako linanukia harufu ya "uchama kwanza"! 😅

Unajifanya mwanasayansi wa asili lakini ukweli ni kwamba wewe ni mjumbe wa Kamati ya Ushindi wa Chadema, unayejificha nyuma ya "fake ID" ili uendelee kulinda na kutetea chama chako kwa nguvu zote!

Unadai huna chama, lakini unasemaje unazunguka kukusanya "qualitative data" kupitia mazungumzo ya JF, mitandao ya kijamii, na polisi? Hizi ni mbinu za kisiasa za hali ya juu, ndugu!🥴

Ni wazi kabisa unatumia falsafa za maji na lugha ya hila kusifu Chadema, ili tu kusambaza agenda yako. Yani "ukitaka kunywa maji ni Chadema, kuoga ni Chadema, kufulia ni Chadema, hata tongotongo ni Chadema!" 😂

Lakini usijali, tumekugundua sasa. Hatutashangaa ukija na "theory" nyingine ya upepo wa baharini kusaidia mikutano ya Chadema kufanikiwa!

Tunakusalimu, mjumbe wa Chadema uliyejificha kwenye "natural sciences" ukifanya kazi ya "defense unit" kwa jina la utafiti wa kibunif
u! 😂😂😂

Mawazo yako yanaheshimiwa kama wengine waliohusika kwnye study hii usijali, unarudi kwenye attitude, perceptions, emotions, thoughts etc, hizo zako pia ni qualitative data mjumbe so unaniongezea tu data bwana juma! Kiufupi nawe umeingia kuyaoga, kuyanywa, kufulia etc.
 
WE UNAAMBIWA NI MBOWE UNASEMA CCM YAANI AKILI YAKO UNAONYESHA WAZI HAIFANYI KAZI
Usi-panic, jifunze siasa za hii nchi na ujue jinsi wanasiasa wanavyocheza na akili za wananchi kwa kutumia pesa za wananchi kwa maslahi yao(bila kujali chama).

Bado ninailaumu ccm kwa vile ni chamadola kinachotumia pesa kupitia viongozi kanjanja wa vyama pinzani kuua demokrasia ya kweli hapa nchini.
 
Ndio maana wenye akili Timamu na wanaojitambua wanaondoka CHADEMA na kuhamia CCM chama kilichobeba matumaini ya mamilioni ya watanzania
Naona unachekelea.naomba nikwambie katika ujenzi wa nchii na maendeleo mwanachama mmoja wa upinzani ana thamani sawa na wanaccm 5,000.wewe na wenzako ni adui wa 4 kati ya maadui 3 aliowaacha mwalimu Nyerere.
 
Hii habari ikipelekwa JamiiCheck itaonekana ni uongo na uzushi. Juzi na jana habari za Lucas Mwashambwa na chiembe zimeonekana ni za uzushi. Hata hii nayo ni uzushi tu. Kuelekea uchaguzi mkuu tutaona na kusikia propaganda nyingi sana. Ni jukumu la JamiiForums na JamiiCheck kuzimulika na kuzifuatlia hizi habari zinazoandikwa na hawa wanaojinasibu ni Wanachama wa CCM. Maana wamekuwa wakitumia muda wao na akili zao vibaya kuleta habari za Uzushi na Uongo humu ndani.
JamiiForums hii habari ina walakini na dosari nyingi sana namna ilivyowasilishwa, lindeni hadhi na heshima ya huu mtandao.
Ikagueni hii habari na muithibitishe
Mimi mwana chadema, ila umelia sana katika post yako
 
Lakini hicho Chama si ni cha Mbowe, aliachiwa na Baba Mkwe? Hivyo ana haki ya kuwaweka viongozi anaowataka. Nyinyi ambao hamna hati miliki, mna haki ya kuondoka pia. Kila mtu abaki kwenye haki yake.
 
Mawazo yako yanaheshimiwa kama wengine waliohusika kwnye study hii usijali, unarudi kwenye attitude, perceptions, emotions, thoughts etc, hizo zako pia ni qualitative data mjumbe so unaniongezea tu data bwana juma! Kiufupi nawe umeingia kuyaoga, kuyanywa, kufulia etc.
Nashukuru kwa heshima yako, lakini sidhani kama unajua unachokisema! 😄
Unaigiza kukubali mawazo ya wengine, lakini ukweli ni kwamba unalinda maslahi ya chama chako kwa nguvu zote.

Kama unadhani kuwa mawazo yangu ni "data," basi ni dhahiri kuwa hujui maana halisi ya utafiti.

Unapozungumzia "attitude, perceptions, emotions, thoughts," inadhihirisha tu kuwa umekosa uelewa wa dhati wa sayansi.

Utafiti wa kweli unahitaji ukweli, si "kuoga, kunywa, na kufulia."Hayo ni mambo ya kisiasa ambayo unajaribu kuyatumia kubeba ajenda yako.

Na kuhusu kusema "Chadema ipo kila mahali," ni dhihirisho la kutokuweza kuzungumzia masuala muhimu!

Inaonekana unataka kila kitu kiwe Chadema. Lakini hebu tuzungumzie ukweli wa mambo kwa kuzingatia kuwa kila mtu ana haki ya kufikiri tofauti!

Tafadhali acha kujificha nyuma ya lugha nzuri na falsafa za maji. 😆😆

Ni wazi, wewe ni mjumbe wa Chadema na unataka tu kuficha ukweli ili kutimiza majukumu yako ya propaganda mitandaoni na jioni upokee 10000 yako kutoka kwa "Bon yai" ukapate kiburudisho🤚
 
Mimi sio mwanasiasa wala mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, na wala sio social scientist bali nipo kwenye natural sciences. Kwa mujibu wa research nazofanya mojawapo ni qualitative ambayo haihitaji empirical data, tunapata conclusions kwa human perceptions, feelings, thoughts, says, mitazamo, mazungumzo, reactions, nk nk.

Kwa ujumla utafiti wangu usio rasmi qualitatively, naona Chadema ni lidude moja kubwa mno na linalotisha sana kwa kutazama namna reactions, na qualitative data zilizopo humu JF, radioni, social media zingine, TV, blogs, Polisi, jeshini, mitaani, magengeni, chats, groups za chawas etc. hamna siku chadema haijatajwa mara 10 hadi 20! Kuanzia mama yao/yetu akilala, akiamka, akiongea, akiwaza, chadema inazunguka kichwani kwake, makondeko kule kwa landrover kila akiamka, makalai kwenye mizunguko yake ya perdiem, joni nchambi, tulizo kule dom, mcheza kiduku wa daslam, hapi, mkumbwa, cc yote ya ccm, machawa wazoefu na wapya kote mitandaoni, mwashamba, talalalah, choicevariable, yohana mbatizaji, na wengine lukuki. Polisi ndio wakisikia kuanzia kaka yao mkubwa anayevaa official dress na buti hata kwenye sherehe ikulu kama yupo vitani ndio wanapagawa kabisa na kuitana nchi nzima, na kuwasha mazimamoto yao ya kipigaji. Hili dude linawatisha sana kisaikolijia.

My conclusion kwa haya naona chadema sasa niifananishe na maji kwa kweli, yani ni lazima uyatumie tu ili uishi, kuna watu kwa kuitajataja tu wamepata uwaziri, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa, ubunge, uchawa rasmi, ukatibu-kata na uenezi wa ccm, wengine wakapigwa na pesa, wengine ubalozi, wengine ucovid-19 sasa hii si sawa na maji tu wandugu??

Yani utake usitake utayanywa, usipoyanywa utayaoga, usipoyaoga utafulia, usipoyafulia utapikia, usipopikia utaoshea hata tongotongo. Ili tumbo lako lisitirike kwa sasa we andika, taja, waza, ongea kuhusu chadema, ukiongelea mwengine unafutika tu kama upepo. Relavance yako itakuja kwa kusema chademaaaaa, chademaaaa hata kama huna logic km mwashamba.

Yani kuna watu wasipotaja chadema wanapotea so ili wawe relevant lazima kila siku waje na uzi kuhusu chadema tu, gosh!! Wengine hata spelling hawajui lkn chadema ipo midomoni mwao kutwa kucha.

No offence hii ni perception ya jamii ya watanzania kuanzia mama yetu shuka chini hadi kwa machawa wa level za chini kbs kama hapa nilipo cholesamvula.
Maelezo meeeengi lakini Sijaona ulipozungumzia huo mada husika; yaani huo ugomvi hapo wa Hela.
 
Vurugu kubwa zilizotokea Katavi katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Chadema, zimeonesha wazi jinsi migawanyiko inavyoathiri demokrasia ndani ya chama.

Wanachama walichapana makonde na kuchaniana sare walizovaa, hali iliyopelekea kutoana damu na polisi kuingilia kati ili kutuliza machafuko.

Uongozi wa kitaifa, chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu, umeonekana kushindwa kuzuia migongano ya makundi inayozidi kuota mizizi, hali ambayo imepelekea rushwa kuwa silaha inayotumiwa na viongozi hao kuimarisha ushawishi wao kwa wanachama.

Mbowe, licha ya kutoa rushwa, anashutumiwa kutumia kiti chake cha Mwenyekiti wa Chadema kuwashinikiza wajumbe wachague viongozi anaowataka kwa maslahi binafsi.

Katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob alishinda kwa asilimia 77, jambo linalodaiwa kufanyika kwa maelekezo ya Mbowe, hali inayothibitisha ukandamizaji wa demokrasia ndani ya chama.

Hali hii imemchukiza Tundu Lissu, ambaye ameanza kuwachochea wanachama wanaomuunga mkono kuharibu chaguzi za ndani ya chama kwa kuanzisha fujo.

Mbowe na kundi lake wanatuhumiwa kuwapendelea wagombea kwa kutoa hongo ili kuhakikisha wanapata nafasi za juu katika chama, wakati kundi linaloongozwa na Tundu Lissu linatumia mbinu hizohizo za kutoa hongo kwa wajumbe ili kuwaweka madarakani wagombea wenye maslahi kwao.

Hii imeleta mgawanyiko mkubwa ndani ya Chadema, huku rushwa ikionekana kama kipimo cha kufanikisha uchaguzi badala ya sifa na uwezo, na kutishia hadhi ya chama kama chombo cha demokrasia, kwani vitendo vya kuhonga wajumbe vinapingana na misingi ya uwazi na haki.

CCM tukae chonjo kwani Chadema kinazidi kuongeza mvuto.
Kama kuna hekaheka kiasi hicho kwenye chaguzi kama inavyotokeaga kwenye chaguzi za ndani ya CCM,ujue Chama hicho kimeshakuwa na mvuto mkubwa.
 
Vurugu kubwa zilizotokea Katavi katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Chadema, zimeonesha wazi jinsi migawanyiko inavyoathiri demokrasia ndani ya chama.

Wanachama walichapana makonde na kuchaniana sare walizovaa, hali iliyopelekea kutoana damu na polisi kuingilia kati ili kutuliza machafuko.

Uongozi wa kitaifa, chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu, umeonekana kushindwa kuzuia migongano ya makundi inayozidi kuota mizizi, hali ambayo imepelekea rushwa kuwa silaha inayotumiwa na viongozi hao kuimarisha ushawishi wao kwa wanachama.

Mbowe, licha ya kutoa rushwa, anashutumiwa kutumia kiti chake cha Mwenyekiti wa Chadema kuwashinikiza wajumbe wachague viongozi anaowataka kwa maslahi binafsi.

Katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob alishinda kwa asilimia 77, jambo linalodaiwa kufanyika kwa maelekezo ya Mbowe, hali inayothibitisha ukandamizaji wa demokrasia ndani ya chama.

Hali hii imemchukiza Tundu Lissu, ambaye ameanza kuwachochea wanachama wanaomuunga mkono kuharibu chaguzi za ndani ya chama kwa kuanzisha fujo.

Mbowe na kundi lake wanatuhumiwa kuwapendelea wagombea kwa kutoa hongo ili kuhakikisha wanapata nafasi za juu katika chama, wakati kundi linaloongozwa na Tundu Lissu linatumia mbinu hizohizo za kutoa hongo kwa wajumbe ili kuwaweka madarakani wagombea wenye maslahi kwao.

Hii imeleta mgawanyiko mkubwa ndani ya Chadema, huku rushwa ikionekana kama kipimo cha kufanikisha uchaguzi badala ya sifa na uwezo, na kutishia hadhi ya chama kama chombo cha demokrasia, kwani vitendo vya kuhonga wajumbe vinapingana na misingi ya uwazi na haki.

Video na headline vitu viwili tofauti

Anyway, tumekuelewa
 
Nashukuru kwa heshima yako, lakini sidhani kama unajua unachokisema! 😄
Unaigiza kukubali mawazo ya wengine, lakini ukweli ni kwamba unalinda maslahi ya chama chako kwa nguvu zote.

Kama unadhani kuwa mawazo yangu ni "data," basi ni dhahiri kuwa hujui maana halisi ya utafiti.

Unapozungumzia "attitude, perceptions, emotions, thoughts," inadhihirisha tu kuwa umekosa uelewa wa dhati wa sayansi.

Utafiti wa kweli unahitaji ukweli, si "kuoga, kunywa, na kufulia."Hayo ni mambo ya kisiasa ambayo unajaribu kuyatumia kubeba ajenda yako.

Na kuhusu kusema "Chadema ipo kila mahali," ni dhihirisho la kutokuweza kuzungumzia masuala muhimu!

Inaonekana unataka kila kitu kiwe Chadema. Lakini hebu tuzungumzie ukweli wa mambo kwa kuzingatia kuwa kila mtu ana haki ya kufikiri tofauti!

Tafadhali acha kujificha nyuma ya lugha nzuri na falsafa za maji. 😆😆

Ni wazi, wewe ni mjumbe wa Chadema na unataka tu kuficha ukweli ili kutimiza majukumu yako ya propaganda mitandaoni na jioni upokee 10000 yako kutoka kwa "Bon yai" ukapate kiburudisho🤚

Nakubaliana kutofautiana nawe na hiyo si big deal. "Kama unadhani kuwa mawazo yangu ni "data," basi ni dhahiri kuwa hujui maana halisi ya utafiti". Kama ndio uelewa wako upo hivi nafikiri naongea na mtu anayekariri anyway naheshimu mawazo yako ila unapaswa kujielemisha kidogo usitie aibu ndogondogo hizi. Anyway sipo kwenye siasa na mtazamo wangu haupo kwa maslahi ya mwanasiasa wala chama chochote. Chadema haiwezi kunilipa mie na wala sitegemei lolote toka huko. Level unayoitaja nilitoka miaka zaidi ya 30 iliyopita na nina mawazo huru 100% unaweza kuchukua au acha.

Ninajua watu wamepata uwaziri, ukatibukata, ubunge etc kwa kutaja chadema tu na wewe upo mkondo uleule probably (no judging) hii ni fact, nyuzi za chadema deile ni fact, mama yetu kuteseka na chadema ni fact, mapolisi kuteseka na chadema ni fact, mwashambwa na machawa wengine kusafiria chadema ni fact, chukua au kataa is up to you, uzuri ukweli haupigwi nyundo unajidhihirisha muda wote. Ukikataa hizi ntakuona una tatizo naomba nisifike huko.

Kwamba napigia chadema debe huu ni upuuzi tu wa kuondoka kwenye mada, najua kabisa pamoja na kugopwa sana kisaikolojia na ccm na watawala bado chadema haina uwezo wa kuchukua nchi na siogopi kusema hivyo. Wanaogopa jina lakini kimsingi chadema haina strategy yoyote ya kuisha watawala, labda (assuming though) wawe wanatumia kupigia pesa (sishangai kwa ccm) kujenga unessary fear ili watengeneze mradi wao.

I am independent bro hahaha na 10,000 kunipa labda mie iwe in $$$ sio madafu. Yani JF nipo kurefresh na kutoa mawazo yangu baaasi!
 
Maelezo meeeengi lakini Sijaona ulipozungumzia huo mada husika; yaani huo ugomvi hapo wa Hela.

Utakuwa unaishi kwa kukariri basi sio lazima kila kitu uelewe hata darasani kuna wa mwisho na kuna anayemaliza hata kusoma hajui! Inakubalika tu, ni normal distribution
 
Back
Top Bottom