Pre GE2025 Wanachama wa CHADEMA Katavi wachapana makonde, Mbowe ashutumiwa kugawa pesa kwa wajumbe

Pre GE2025 Wanachama wa CHADEMA Katavi wachapana makonde, Mbowe ashutumiwa kugawa pesa kwa wajumbe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watu kama hawa ukiwapa ridhaa ya kukuongoza, ujue wazi kuwa mpaka wajaze matumbo yao na yafamilia zao ndipo wawaze kuwawazia nyie mliowapa ridhaa ya kutumikia.

..waheshimuni walioko Chadema sasa hivi.

..hao ndio wenye dhamira ya kweli ya mabadiliko.

..hawajajiunga Chadema kujaza matumbo kwasababu chama hicho hakina uwezo huo.
 
Haswa..! Wanahusika kwa kiwango kikubwa. Pesa zinazogombewa/zinazotolewa kama rushwa ni 'fupa' walilorushiwa na ccm.

..Ccm akimhonga Chadema ujue na yeye amehongwa mahali fulani.

..Na kwasababu wameshika dola basi huenda wamehongwa kuhujumu rasilimali za nchi.
 
Vurugu kubwa zilizotokea Katavi katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Chadema, zimeonesha wazi jinsi migawanyiko inavyoathiri demokrasia ndani ya chama.

Wanachama walichapana makonde na kuchaniana sare walizovaa, hali iliyopelekea kutoana damu na polisi kuingilia kati ili kutuliza machafuko.

Uongozi wa kitaifa, chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu, umeonekana kushindwa kuzuia migongano ya makundi inayozidi kuota mizizi, hali ambayo imepelekea rushwa kuwa silaha inayotumiwa na viongozi hao kuimarisha ushawishi wao kwa wanachama.

Mbowe, licha ya kutoa rushwa, anashutumiwa kutumia kiti chake cha Mwenyekiti wa Chadema kuwashinikiza wajumbe wachague viongozi anaowataka kwa maslahi binafsi.

Katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob alishinda kwa asilimia 77, jambo linalodaiwa kufanyika kwa maelekezo ya Mbowe, hali inayothibitisha ukandamizaji wa demokrasia ndani ya chama.

Hali hii imemchukiza Tundu Lissu, ambaye ameanza kuwachochea wanachama wanaomuunga mkono kuharibu chaguzi za ndani ya chama kwa kuanzisha fujo.

Mbowe na kundi lake wanatuhumiwa kuwapendelea wagombea kwa kutoa hongo ili kuhakikisha wanapata nafasi za juu katika chama, wakati kundi linaloongozwa na Tundu Lissu linatumia mbinu hizohizo za kutoa hongo kwa wajumbe ili kuwaweka madarakani wagombea wenye maslahi kwao.

Hii imeleta mgawanyiko mkubwa ndani ya Chadema, huku rushwa ikionekana kama kipimo cha kufanikisha uchaguzi badala ya sifa na uwezo, na kutishia hadhi ya chama kama chombo cha demokrasia, kwani vitendo vya kuhonga wajumbe vinapingana na misingi ya uwazi na haki.

Hizo hapo unazoleta ni porojo na propaganda unazoleta ili kuwachonganisha wanachama wa Chadema, hakuna rushwa yoyote kwenye uchaguzi huo , Lissu yuko Ulaya. Chadema ni watu wanaojielewa hizo mbinu unazoleta sasa hivi ni za kizamani sana.
 
Back
Top Bottom