Pre GE2025 Wanachama wa CHADEMA Katavi wachapana makonde, Mbowe ashutumiwa kugawa pesa kwa wajumbe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona hatujaona makonde hapo

Ova
Umeona wanakunywa bia na kukumbatiana sio?
Hiki Chama kinajaribu kuleta migogoro ya kidini nchini. Kulikuwa na sababu gani kumtuma yule Mzee wenu wa BAZECHA Kuongea yale Maneno?
 

Mawazo yako yanaheshimiwa kama wengine waliohusika kwnye study hii usijali, unarudi kwenye attitude, perceptions, emotions, thoughts etc, hizo zako pia ni qualitative data mjumbe so unaniongezea tu data bwana juma! Kiufupi nawe umeingia kuyaoga, kuyanywa, kufulia etc.
 
WE UNAAMBIWA NI MBOWE UNASEMA CCM YAANI AKILI YAKO UNAONYESHA WAZI HAIFANYI KAZI
Usi-panic, jifunze siasa za hii nchi na ujue jinsi wanasiasa wanavyocheza na akili za wananchi kwa kutumia pesa za wananchi kwa maslahi yao(bila kujali chama).

Bado ninailaumu ccm kwa vile ni chamadola kinachotumia pesa kupitia viongozi kanjanja wa vyama pinzani kuua demokrasia ya kweli hapa nchini.
 
Ndio maana wenye akili Timamu na wanaojitambua wanaondoka CHADEMA na kuhamia CCM chama kilichobeba matumaini ya mamilioni ya watanzania
Naona unachekelea.naomba nikwambie katika ujenzi wa nchii na maendeleo mwanachama mmoja wa upinzani ana thamani sawa na wanaccm 5,000.wewe na wenzako ni adui wa 4 kati ya maadui 3 aliowaacha mwalimu Nyerere.
 
Mimi mwana chadema, ila umelia sana katika post yako
 
Lakini hicho Chama si ni cha Mbowe, aliachiwa na Baba Mkwe? Hivyo ana haki ya kuwaweka viongozi anaowataka. Nyinyi ambao hamna hati miliki, mna haki ya kuondoka pia. Kila mtu abaki kwenye haki yake.
 
Nashukuru kwa heshima yako, lakini sidhani kama unajua unachokisema! πŸ˜„
Unaigiza kukubali mawazo ya wengine, lakini ukweli ni kwamba unalinda maslahi ya chama chako kwa nguvu zote.

Kama unadhani kuwa mawazo yangu ni "data," basi ni dhahiri kuwa hujui maana halisi ya utafiti.

Unapozungumzia "attitude, perceptions, emotions, thoughts," inadhihirisha tu kuwa umekosa uelewa wa dhati wa sayansi.

Utafiti wa kweli unahitaji ukweli, si "kuoga, kunywa, na kufulia."Hayo ni mambo ya kisiasa ambayo unajaribu kuyatumia kubeba ajenda yako.

Na kuhusu kusema "Chadema ipo kila mahali," ni dhihirisho la kutokuweza kuzungumzia masuala muhimu!

Inaonekana unataka kila kitu kiwe Chadema. Lakini hebu tuzungumzie ukweli wa mambo kwa kuzingatia kuwa kila mtu ana haki ya kufikiri tofauti!

Tafadhali acha kujificha nyuma ya lugha nzuri na falsafa za maji. πŸ˜†πŸ˜†

Ni wazi, wewe ni mjumbe wa Chadema na unataka tu kuficha ukweli ili kutimiza majukumu yako ya propaganda mitandaoni na jioni upokee 10000 yako kutoka kwa "Bon yai" ukapate kiburudisho🀚
 
Maelezo meeeengi lakini Sijaona ulipozungumzia huo mada husika; yaani huo ugomvi hapo wa Hela.
 
CCM tukae chonjo kwani Chadema kinazidi kuongeza mvuto.
Kama kuna hekaheka kiasi hicho kwenye chaguzi kama inavyotokeaga kwenye chaguzi za ndani ya CCM,ujue Chama hicho kimeshakuwa na mvuto mkubwa.
 
Video na headline vitu viwili tofauti

Anyway, tumekuelewa
 

Nakubaliana kutofautiana nawe na hiyo si big deal. "Kama unadhani kuwa mawazo yangu ni "data," basi ni dhahiri kuwa hujui maana halisi ya utafiti". Kama ndio uelewa wako upo hivi nafikiri naongea na mtu anayekariri anyway naheshimu mawazo yako ila unapaswa kujielemisha kidogo usitie aibu ndogondogo hizi. Anyway sipo kwenye siasa na mtazamo wangu haupo kwa maslahi ya mwanasiasa wala chama chochote. Chadema haiwezi kunilipa mie na wala sitegemei lolote toka huko. Level unayoitaja nilitoka miaka zaidi ya 30 iliyopita na nina mawazo huru 100% unaweza kuchukua au acha.

Ninajua watu wamepata uwaziri, ukatibukata, ubunge etc kwa kutaja chadema tu na wewe upo mkondo uleule probably (no judging) hii ni fact, nyuzi za chadema deile ni fact, mama yetu kuteseka na chadema ni fact, mapolisi kuteseka na chadema ni fact, mwashambwa na machawa wengine kusafiria chadema ni fact, chukua au kataa is up to you, uzuri ukweli haupigwi nyundo unajidhihirisha muda wote. Ukikataa hizi ntakuona una tatizo naomba nisifike huko.

Kwamba napigia chadema debe huu ni upuuzi tu wa kuondoka kwenye mada, najua kabisa pamoja na kugopwa sana kisaikolojia na ccm na watawala bado chadema haina uwezo wa kuchukua nchi na siogopi kusema hivyo. Wanaogopa jina lakini kimsingi chadema haina strategy yoyote ya kuisha watawala, labda (assuming though) wawe wanatumia kupigia pesa (sishangai kwa ccm) kujenga unessary fear ili watengeneze mradi wao.

I am independent bro hahaha na 10,000 kunipa labda mie iwe in $$$ sio madafu. Yani JF nipo kurefresh na kutoa mawazo yangu baaasi!
 
Maelezo meeeengi lakini Sijaona ulipozungumzia huo mada husika; yaani huo ugomvi hapo wa Hela.

Utakuwa unaishi kwa kukariri basi sio lazima kila kitu uelewe hata darasani kuna wa mwisho na kuna anayemaliza hata kusoma hajui! Inakubalika tu, ni normal distribution
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…