Wanachama wa JamiiForums waliotambuliwa kwa kuwa na michango chanya Jukwaani kwa mwaka 2024

Wanachama wa JamiiForums waliotambuliwa kwa kuwa na michango chanya Jukwaani kwa mwaka 2024

umenifurahisha umenikumbusha mwaka Jana kuna jama kaja pm kachat weekend gaflaa br naweza tukameet wapi tushare ideas

Nkazima simu
Nkatoa betri kwa mda
πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Hongereni wote pamoja na Madmax mzee wa magari ya umeme na yale mengine ya kwenye movie.
 
michakato mbali mbali katika kuthamini jitihada za kila mmoja ndani ya jamiiforums. jambo jema saana
 
Shida mnataja real names..!! Ingependeza hata huko tuzoni mtaje fake names According to his/her USERNAME ID..
Dunia ya Leo fake name ni illusion! Maana hautumii gadget fake kuingia mtandaoni.
===
Hongera sana wote kwa kutambuliwa mchango wenu hapa Jukwaani. Ushauri, muendelee kuliheshimisha jukwaa hili pendwa kwa kuendelea kutuletea kazi nzuri. Mtabarikiwa.
 
Ha
Katika kuendeleza dhamira yake ya kuthamini na kuhimiza uzalishaji wa maudhui yenye ubora na tija mtandaoni, JamiiForums usiku wa leo, wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Shindano la Stories of Change 2024, inawatambua Wanachama wake watano waliotoa michango chanya mwaka huu 2024 ndani ya Majukwaa yake.

Wanachama hao watapokea zawadi maalum kama sehemu ya shukrani kwa juhudi zao za kudumu na mchango wao wa kipekee katika kuzalisha maudhui yenye maana kwenye jukwaa.

Hafla mbashara ya utoaji tuzo kwa washindi wa Stories Of Change 2024, soma Yanayojiri katika usiku wa kutoa tuzo kwa Washindi wa Shindano la Stories of Change 2024

Wanachama hao ni pamoja na:

Mwl.RCT
Mwl. RCT amefanikiwa kuibuka Mwanachama Bora kutokana na kushiriki kwa namna ya kipekee katika Shindano la Stories of Change mwaka huu wa 2024.

Mwanachama huyu amefanya jitihada kubwa kutengeneza maudhui yenye kuleta mabadiliko huku mwaka huu akitoa mapendekezo mbalimbali kuelekea Tanzania Tuitakayo.

Takwimu zinaoneshwa ndani ya shindano la mwaka huu Mwl.RCT amechapisha jumla ya makala jumla ya makala 42 na kumfanya awe mshiriki mwenye machapisho mengi zaidi kwenye shindano hili la SoC la mwaka huu.

Mbali na michango yake katika SoC, Mwl. RCT amekuwa mshiriki hai na mwenye heshima kwenye majukwaa mbalimbali, akijenga mijadala yenye tija kwa kutumia lugha ya kistaarabu. Uwezo wake wa kuhamasisha mijadala yenye maana umemfanya kuwa nguzo muhimu ya jamii ya JamiiForums.

Fungua Link kusom moja ya chapisho lake: SoC04 - From Savanna to Silicon: Tanzania's Unlikely Tech Hub Transformation

Robert Heriel Mtibeli
Robert anajulikana kwa kutengeneza na kuleta machapisho yake binafsi (Original Content) yaliyojaa hoja, fikra na maoni yenye msimamo thabiti. Amekuwa miongoni mwa sauti ya pekee kwenye jukwaa kwa kuzungumzia masuala nyeti kama udanganyifu wa kisiasa na kijamii, na umuhimu wa watu kuachana na hofu ya yasiyojulikana. Robert ni mfano bora wa mchangiaji anayesukuma mbele ajenda za majadiliano huru, akitekeleza dhamira ya JamiiForums ya kukuza fikra huru na za kina.

Fungua Link kusom moja ya chapisho lake: Watibeli tunalaani matukio ya utekaji na watekaji wenyewe

Mad Max
Mad Max amebainisha uwezo wake kwenye jukwaa la JF Garage kwa kuwa mmoja wa wachangiaji wenye maarifa ya kina kuhusu magari. Mara kwa mara amekuwa akitoa uzoefu wake katika sekta ya magari na michezo ya magari umewavutia Wanachama wengi wanaotembele Jukwaa la JF Garage. Ameonesha uelewa mkubwa kwenye teknolojia mpya kama magari ya umeme na kuchochea majadiliano muhimu kuhusu mustakabali wa usafiri nchini Tanzania. Amekuwa Active Member ambaye ametoa amechangia mijadala zaidi ya 500 kwa mwaka huu wa 2024.

Fungua Link kusoma moja ya chapisho lake: Content Creators mnaoanza (Episode I): Unatumia camera gani kutengeneza maudhui yako?

SteveMollel
SteveMollel ni mdau wa Filamu ambaye ameonesha utofauti kwa kutengeneza maudhui mbalimbali yanayohusu filamu na Wasanii ndani ya Jukwaa la Entertainment. Amekuwa na uwezo wa kuandaa maudhui yenye mpangilio mzuri na kutoa mapendekezo ya filamu kwa Wanachama wengine wa JamiiForums.

Fungua Link kusoma moja ya chapisho lake:Movies nne kali za kucheki wiki hii

Nifah
Nifah amekuwa Mwanachama muhimu na ameonyesha umahiri wake katika Jukwaa la Celebrities na Jukwaa la Entertainment kwa kuleta habari za ndani zinazohusu burudani na Wasanii na kulifanya Jukwaa letu kuwa la kwanza kupata taarifa hizo kabla ya wengine.

Kwa mfano, aliripoti kashfa inayohusisha msanii Harmonize kudaiwa na Benki ya CRB (Soma Hapa). Taarifa hiyo ilipata zaidi ya maoni 470 kabla ya kuenea kwenye vyombo vya habari vingine. Uwezo wa Nifah kutoa taarifa zenye mvuto na uchambuzi wa kina unamfanya kuwa mmoja wa wachangiaji muhimu wa jukwaa la burudani.

Fungua Link kusom moja ya chapisho lake:Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!
po kwenye celebrities mlinisahau?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Halafu nililetaga habari ya kweli ya mwenye mji wake kule kaskaz kurudi modes wakaifuta...Ile ilikuwa ya kwel na JF ndo ilikuwa iwe ya kwanza kubreak the newsπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom