Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Wakutana kutatua changamoto zinazokwamisha Biashara

Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Wakutana kutatua changamoto zinazokwamisha Biashara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-09-22 at 16.35.30w.jpeg
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinakutana jijini Dar es Salaam kujadili na kuweka mikakati ya kutatua changamoto na vikwazo vinavyokwamisha biashara ndani ya Jumuiya, hususan Vikwazo Visivyo vya Kikodi (Non-Tariff Barriers – NTBs).

Mkutano huo ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi za EAC, uliofanyika jijini Arusha Machi 7, 2026, ambao ulizitaka Nchi Wanachama kuchukua hatua za haraka za kuondoa vikwazo vyote vya biashara visivyo vya kodi vilivyoripotiwa ndani ya Jumuiya ifikapo Juni 30, 2026.
WhatsApp Image 2026-09-22 at 16.35.31.jpeg
WhatsApp Image 2026-09-22 at 16.35.31e.jpeg
Sanjari na hayo, mkutano huo utajadili hatua za utekelezaji wa maelekezo ya Mkutano Maalum wa Pili wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) uliofanyika Novemba 25, 2025, ambao ulielekeza nchi wanachama kuondoa ushuru, ada, tozo na kodi za ndani zinazobagua bidhaa za Nchi Wanachama kinyume na matakwa ya Ibara ya 10 na 15 ya Itifaki ya Umoja wa Forodha ya EAC, ifikapo Juni 30, 2026 na kufanya marekebisho ya tafsiri ya baadhi ya maneno katika sheria za ndani ili kuendana na makubaliano ya Jumuiya.

Miongoni mwa ajenda muhimu zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na; tathmini ya utendaji wa Vituo vya Pamoja vya Huduma Mpakani (One Stop Border Posts – OSBPs), Mpango Kazi wa Kutatua Masuala Yanayoathiri Biashara ndani ya Jumuiya, pamoja na Jedwali la Utekelezaji wa Mpango Kazi huo.

Mkutano huo pia utajadili na kupitia Orodha ya Vikwazo Visivyo vya Kodi (Non-Tariff Barriers Index) ya EAC, ambayo ni miongoni mwa nyenzo zinazotumika kufuatilia, kutambua na kupima hatua zinazochukuliwa na Nchi Wanachama katika kushughulikia vikwazo vinavyoathiri biashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
WhatsApp Image 2026-09-22 at 16.35.32.jpeg
Hatua hizo ni muhimu katika kuimarisha utekelezaji wa Soko la Pamoja la EAC, ambalo linalenga kurahisisha usafirishaji bidhaa, watu, huduma na mitaji na haki ya kuanzisha shughuli za biashara katika Nchi Wanachama. Kuondolewa kwa vikwazo visivyo vya kodi na kurahisishwa kwa taratibu za mipakani kunatarajiwa kupunguza gharama na muda wa kufanya biashara, kuongeza ushindani na kukuza biashara ya ndani ya Jumuiya.

Mkutano huo unatarajiwa kutoa mapendekezo na hatua mahususi za utekelezaji zitakazosaidia kuharakisha uondoaji wa vikwazo vya biashara, kuboresha ufanisi mipakani na kuimarisha biashara ya kikanda, ikiwa ni sehemu ya jitihada za EAC kujenga Jumuiya yenye ushindani, jumuishi na inayotoa fursa zaidi kwa wananchi wake.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ngazi ya Wataalamu unaongozwa na Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benjamini Mwesiga, akiongozana na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali.
 
Benki ya dunia na IMF mwaka 2019 viliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati baada ya maboresho makubwa ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na hayati Magufuli na Makamu wake Samia.

Serikali ya awamu ya tano ilifikia hayo mafanikio ya kuingiza nchi uchumi wa kati baada ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi, kujenga viwanda na kuhimiza wananchi kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.

Hali ilibadilika ghafla baada ya Rais Samia kuapishwa serikali yake ya awamu ya sita ikaacha kuhubiri viwanda wala wananchi wake kuchapa kazi na akatangaza sera mpya ya kula kulingana na urefu wa kamba yako! Matokeo yake ni kuuzwa kwa sekta muhimu za kuingizia nchi kipato kama bandari zote na makaa ya mawe.

Kutokana na kuzorota huku kwa usimamizi wa rasilimali za taifa Tanzania imeshushwa kutoka uchumi wa kati na sasa haieleweki iko uchumi gani! Hivyo Rais ajaye baada ya Samia atakuwa na kazi kubwa ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi serikali, kulinda rasilimali za taifa na kuirudisha nchi uchumi wa kati tena.

Kuna kila aina ya ushahidi kuwa Rais Samia amekata tamaa na haumizi kichwa tena kuhusiana na shida za watanzania ila inaonekana awamu yake hii ya pili alijipanga kula raha na kusafiri sana duniani ila mauwaji ya oktoba 29 yamempunguza speed baada ya kupigwa marufuku kusafiri ndani ya nchi za Ulaya.
 
Hakuna kitaasisi cha ovyo kama Bank ya dunia.
 
EAC Haina maamuzi kabisa. Summit ilishatoka directive Non Tarrif Barriers ziondelewe nchi zote ifikapo tarehe 30 June 2026 lakini mpaka Leo hakuna la maana lilifanyika. Ndio kwanza vinywaji vimezuiliwa.
 
Back
Top Bottom