KWELI Wanachama wa NSSF na PSSSF wanaweza kutumia Michango yao kama dhamana ya kuchukulia Mikopo Kujenga, Kuboresha au Kununua nyumba

KWELI Wanachama wa NSSF na PSSSF wanaweza kutumia Michango yao kama dhamana ya kuchukulia Mikopo Kujenga, Kuboresha au Kununua nyumba

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
National_Social_Security_Fund_Tanzania_NSSF.jpg


Nimeona taarifa mtandaoni ikisema watumishi wa Umma na Binafsi ambao wamechangia kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 katika NSSF au PSSSF sasa rukhsa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania.

Kanuni namba 141 za Mwaka 2024 zimeanza kazi tangu Machi 8, 2024.

JamiiCheck tusaidieni kujua ukweli wake.
 
Tunachokijua
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeanzishwa chini ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018 kwa lengo la kutoa huduma ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Mfuko huu huwa na Majukumu ya Kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na isiyo rasmi, Kukusanya michango, Kuwekeza na Kulipa mafao.

Aidha, Serikali kupitia Sheria namba 2 ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma mwaka 2018, ilifuta Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya LAPF, PSPF, GEPF, PPF na kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Hivyo kuanzia Agosti 1, 2018 waliokuwa wanachama wa Mifuko iliyounganishwa yaani LAPF, PSPF, GEPF na PPF walihamishiwa katika Mfuko wa PSSSF na wataendelea kuwa wanachama na kuchangia katika Mfuko (isipokuwa wanachama wote waliokuwa watumishi wa sekta binafsi kutoka Mifuko iliyounganishwa walihamishiwa NSSF, na watumishi wa Umma waliokuwa NSSF walihamishiwa PSSSF kuanzia Februari, 2019).

Kuibuka kwa Madai tajwa
Machi 14, 2024 kupitia Mtandao wa X, Taarifa za Watumishi wa Umma/binafsi ambao wamechangia Kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 NSSF/PSSSF kuruhusiwa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania zilianza kusambaa.

Madai haya yalichapishwa tena kwenye Mtandao huo huo Machi 15, 2024. Tazama hapa.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini mambo kadhaa kuhusu taarifa hii.

Mosi, ni taarifa ya kweli, ilitangazwa kupitia tangazo la Serikali Namba 141 toleo la Machi 8, 2024 ikiwa na Jina la 'Social Security (Use of Members Benefit Entitlements as Collateral for Home Mortgage) Regulations, 2024.'

screenshot-2024-03-18-105435-png.2938081

Picha ya kipengele kinachoonesha jinsi Mafao yanavyoweza kutumika kama Dhamana
Pili, tofauti na inavyodaiwa kuwa mtu anayepaswa kuomba ni yule aliyechangia kwa miezi 108 (Miaka 9), JamiiCheck imebaini ni Miaka 15 (Miezi 180). Mtanzania aliyetimiza kigezo hiki anaweza kuchukua mkopo kwa kutumia dhamana ya mafao yake ili ajenge nyumba, kununua nyumba au kufanya ukarabati wa nyumba.

Aidha, Mwanachama hatopaswa kuomba mkopo unaozidi 50% ya Mafao yake wakati wa kuomba mkopo na marejesho ya mkopo huo hayatakwenda zaidi ya muda wa kawaida wa kustaafu kazi kwa lazima.

Kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha kanuni hizo, mifuko haitatoa dhamana zaidi ya moja kwa wakati mmoja na kifungu cha 3(3) kinasema dhamana hiyo itatolewa baada ya mwanachama mwenyewe kuomba kwenye mfuko.

Kifungu cha 4(1) (b) kimeweka sharti kuwa bei ya kununulia nyumba haitapaswa kuzidi thamani ya soko la nyumba inayohusika kwa wakati husika.

Aidha, kifungu cha 7 (1) kinataka taasisi ya fedha inayotaka kutoa mkopo hiyo, iwasilishe ombi hilo kwa maandishi na ndani ya siku 30, mfuko utatoa idhinisho la maandishi na endapo utakataa utatoa sababu kwa maandishi.

Hivyo, JamiiCheck imejiridisha kuwa taarifa hii kama ilivyochapishwa na Sildenafil Citrate ni ya kweli, isipokuwa muda wa uchangiaji wa Mwanachama aliyekidhi vigezo vya kuomba dhamana ya mkopo huo ni Miaka 15 (miezi 180) na siyo miezi 108 (Miaka 9) kama alivyobainisha.
Mimi hela zangu nimpe NSSF, NSSF anaenda kufungua fixed account benki ya biashara. Kisha mimi tena naenda huko CRDB kukopa nusu ya pesa zangu mwenyewe zilizowekwa kwao na NSSF kwa riba kubwa na dhamana ya pesa hizo hizo zilizo mara mbili yake. Na kwakuwa ni mkopo wa makazi utakuwa wa muda mrefu.

Biashara kichaa hii, kwanini NSSF wasinikopeshe wenyewe kwa kuchangia gharama kiduchu za uendeshaji wa huu mchakato.
 
Hakuna mateso makali anavyo pitia mtumishi kama kuishi kwa nusu na robo ya mshahala...Kisha huo mshahala ukatwe bima, payee, NSSF na Chama Cha wizala Yako. Utabakiwa na nusu ya mshahala 😭😭😭 harafu huo mradi ukwame

Hiyo nusu sasa igawe ada, chakula, nauli ya kazini, Tanesco, bili ya maji, vocha n.k...!

Ukitaka kujikwamua mfanyakazi ni Bora ukajijengea nidhamu ya matumizi kile kiasi ambacho benki ingekukata kwa kuongeza na riba juu. Ukawa unajiwekea mwenyewe...!

Mathalani benki ukiwakopa watakuwa wanakukata pengine 90k kwa mwezi. Wewe Jenga mazoea ya kuiweka hiyo pesa benki kwa miaka sawa na Ile unge katwa kama unge kopa.

90,000*12*5=5,400,000

Lakini hilo ni gumu sana kwakweli 😭😭😭​
Makato yakizidi si unaiba iba umalize Mwezi.. kama wao wanakuibia kwa riba why you usiibe.. malipo hapa hapa duniani ule msemo nimeukumbuka.
 
Msiifurahie hio mikopo...akuna mkopo wenye manufaa...lengo la mikopo kwa nchi yetu hii ni kukudidimiza uzidi kuwa masikini...

Mkopo ni utumwa ndugu zangu​
Labda ni utumwa kwako, dunia hii inaendeshwa kwa mikopo, iwe ughaibuni au popote pale. Tatizo litakuja iwapo mkopo hautoutumia vyema.
 
Wakikujibu naomba uniambie. Kama wanakata hukohuko nina hela nyingi nikazipunguze nijenge lodge ndogo.
Unakopeshwa kulingana na salary slip Yako inavyo soma...ila wenyewe wanakopeshana mamilioni...pesa zetu🙈🙈🙈​
 
Unakopeshwa kulingana na salary slip Yako inavyo soma...ila wenyewe wanakopeshana mamilioni...pesa zetu🙈🙈🙈​
Sasa kama ni mambo yaleyale ya kuangalia 1/3 ibaki kwenye salary slip yako, kuna haja gani ya kutuambia hao PSSSF na NSSF wanafadhili watumishi au wanachama wao kukopa ili wajenge au kukarabati nyumba?.
Kama ni hivyo, siendi kukopa.
 
Msiifurahie hio mikopo...akuna mkopo wenye manufaa...lengo la mikopo kwa nchi yetu hii ni kukudidimiza uzidi kuwa masikini...

Mkopo ni utumwa ndugu zangu​
Duniani kote mikopo ndiyo inayoleta maendeleo. Miradi na uwekezaji wote mkubwa asilimia kubwa hufadhiliwa na mikopo. Umuhimu ni kukopa kwa malengo siyo kama Tanzania inavyokopa halafu inaenda kutumia kufanya sherehe za Uhuru. Huo unakuwa upumbavu
 
Ni jambo zuri iwapo itabainika kuwa kweli.

Kwa kuwa umesema ni taarifa inayofanyiwa kazi nadhani tutapata taarifa kamili soon

Ila nina wasiwasi kwamba iwapo jambo hilo likafanyika, basi mifuko mingi itakuwa kwenye Ukata.

Kama mnakumbuka, Serikali imekuwa ilikopa fedha nyingi kwenye hii mifuko, hivyo Sina uhakika kama baada ya kukopa iliweza Kurejesha.

Kuna wakati niliwahi kwenda ofisini kwao, kuomba huu Mkopo lakini sikufanikiwa. Kipindi hicho ndiyo kulikuwa na vuguvugu la Serikali kutaka kuunganisha mifuko hii.
 
Kwamba kila mfuko iwe umechangia miaka 9 ama kwa pamoja baina ya hiyo mifuko iwe imetimia miaka 9?
 
Nimeona taarifa mtandaoni ikisema watumishi wa Umma na Binafsi ambao wamechangia kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 katika NSSF au PSSSF sasa rukhsa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania.

Kanuni namba 141 za Mwaka 2024 zimeanza kazi tangu Machi 8, 2024.

JamiiCheck tusaidieni kujua ukweli wake.
Lucas mwashamba yupo?
Analizungumziajee hili
 
Hivi nini kazi / maana ya Pension ?

Wakikopa wakashindwa kulipa inakuwaje Pension yao Inakufa ?, Na wakizeeka wanakuwa mzigo wa nani ?

Hivyo nauliza tena.... Nini maana / kazi ya Pension ?
 
Wakikujibu naomba uniambie. Kama wanakata hukohuko nina hela nyingi nikazipunguze nijenge lodge ndogo.
Mie nilishazilambaga huwa siwaachii hawa jamaa, Kila contract na mafao yake yaani nikiutumikia mkataba Kwa kampuni A Kwa miaka 4 nikimaliza nalamba changu labda itokee nimeunganisha kazi kampuni B lakini kama nita-delay Kwa miezi kadhaa uraiani kijiwe changu huwa ni NSSF na bahasha yangu kufuatilia mafao

Hii nzuri Kwa watu wa sekta binafsi maana unakuta unaingiza Kwa mwezi ela nzuri kiasi ila ukienda bank hukopesheki simply because taasisi binafsi huwa zinatoa mkataba wa mwaka mmoja mmoja hata kama utadumu nao miaka kadhaa na bank wanataka umri wa mkopo uendane na umri wa mkataba yaani kama umeomba loan miaka 2 basi uwe na contract ya miaka 2 and above, vinginevyo mwajiri akuwekee kifua na wengi miyeyusho wanajua wakikudhamini wanahofu ukifanya chini ya kiwango watapata kazi ya kuku-retain mpaka mkopo wako uishe
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom