KWELI Wanachama wa NSSF na PSSSF wanaweza kutumia Michango yao kama dhamana ya kuchukulia Mikopo Kujenga, Kuboresha au Kununua nyumba

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Makato yanakuwa na riba? Kiasi gani? Riba itamnufaisha nani?
Niliulizia tu nikajibiwa na mtu Kwa mdomo nae hayupo aware kivile ila habari hii imetoka wiki hii ngoja tutafute document tuangalie kilichomo
 
Waweke mfumo wa electronic kuwawezesha kukopa, mambo ya kwenda kuwapigia magoti warasimu maofisini yamepitwa na wakati
 
Hapa watumishi wengi watajua/wanajua wanachukua pesa walizo wekeza kwenye mfuko ( michango yao ya kwenye mfuko ) kitu ambacho sio sahihi.

Mifuko ilicho kifanya (Sheria mpya inavyo sema) michango yako iliyopo NSSF/PSSSF inatumika/itatumika kama dhamana ya mkopo, yani ukishindwa kulipa uo mkopo unao chukua bank mafao yako (michango yako) ndio itakuwa dhamana ya kulipa hilo deni (Mkopo). Na sio mfuko kutoa Mikopo kwa wanachama wake.

Kwa maana hiyo rejesho la lile deni (mkopo) ambao mtumishi ameuchukua bank, ambao dhamana yake ni michango yake iliyo kuwepo NSSF/PSSSF, haita katwa kwenye michango yake ambayo ipo kwenye mfuko NSSF/PSSSF bali itakatwa kwenye mshaara wake. Michango yake ipo kama dhamana tu, hii ni sawa kuwekea nyumba, gari au kiwanja dhamana ambapo ukishindwa kulipa deni dhamana yako ndio itachukuliwa.

Watumishi wakumbuke, Kazi ya mifuko ya hifadhi ya jamii sio kutoa mikopo. Lengo mama la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kutuoa mafao. Mikopo ni kazi ya Financial institutions kama Mabank etc.

Naomba kuwasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…