KWELI Wanachama wa NSSF na PSSSF wanaweza kutumia Michango yao kama dhamana ya kuchukulia Mikopo Kujenga, Kuboresha au Kununua nyumba

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Hapa watumishi wengi watajua/wanajua wanachukua pesa walizo wekeza kwenye mfuko ( michango yao ya kwenye mfuko ) kitu ambacho sio sahihi.
Nahisi umenyooka vizuri mkuu,alafu,riba inakuaje? Pia,kama mtumishi ni mfanyabiadhara,anaweza kutumia mfuko kama dhamana kwenye biashara zake?
 
Huu mpango sio mbaya. Tatizo urasimu wa kitanzania. Na kama ni kupitia kwenye ma benki shida nyingine itakuwa moja ya tatu ya baki ya mshahara kwa wanachama wengi
 
Hivi kama mtu kabakiza miaka 5, 4, 3, 2 au 1 kuelekea kustaafu, kwa nini asikopeshwe sehemu ya mafao yake? Hili ndilo nililolitegemea. Lakini kama ni mikopo kama ya kibenki, na ukizingatia watumishi wengi wamekwisha kopa kwenye mabenki, hapo utakata nini kwenye mishahara?
 
Sasa Kuna haja Gani kwenda kukopa kama wanakata kwenye mshahara kila mwezi? Alafu,Jana nimeenda kwenye mabenki tofauti kuulizia,wanasema hawajui kitu kama hicho,nikaenda PSSSF,wakasema pia hawajui Hilo swala.
 
Ni jambo jema sana kwa kuimkwamua
Mfanyakazi mwenye kipato kidogo kwamaana wapo wengi mbaka wanastaafu hawana nyumba na wanaishi nyumba za kupanga
Itasaidia kwa kua kodi ya pango italipa riba ya mkopo
((ILA RIBA ISIWE KUBWA))
 
Je mikopo wanatoa kwenye mabenki au Nssf wenyewe
 
Mbona mama anakopa si tungeweka ela
Kwa miaka 50 ndio tuanze hii miradi mikubwa
 
Hakuna namna sasa
Si kweli usijidanganye
Hivi kwa mwenye kipato cha chini
Awekeze ela kwa miaka 10 huku akiwa anakaa nyumba ya kupanga nakodi analipa
Na kukaa kwenyenyumba yake kwa miaka 10 akiwa anayejenga deni taratibu BORA NN
 
Nzuri hiyooo
 
Sasa Kuna haja Gani kwenda kukopa kama wanakata kwenye mshahara kila mwezi? Alafu,Jana nimeenda kwenye mabenki tofauti kuulizia,wanasema hawajui kitu kama hicho,nikaenda PSSSF,wakasema pia hawajui Hilo swala.
Kwa jinsi walivyoiweka hii huduma ili ikunufanishe inabidi uwe umefanya analysis ya kutosha tena sana, maana hela zako wanazo wao ambazo wameziwekeza kwenye mabenk hayo hayo then we unaenda kopa hukohuko kwa riba ya 16 na zaidi kwa mwaka na tena wamelimit mikopo kwenye Kujenga, Kuboresha au Kununua nyumba, hapo ujiandae kukutana na mlolongo wa viambatisho wanavyohitaji. Yaana hapa nadhani wao wametengeneza utatu mchafu yaani mfuko wa pensheni+nhc+benki=nyumba hapo wote wanampiga mande mtumishi nyuma mbele ndani nje wananyonya michango ya mtumishi.

Ndo maana hawatotaka upate hela cash maana wana ajenda yao na ctually pia huenda ukidefolt mkopo mafao yako ni last option but first option ni hiyo nyumba kuuzwa tena ili bank wapate chao. Sasa nenda kacheki hizo nyumba za nhc aisee kwa mtu mwenye mahesabu makali hawezi nunua zile nyumba labda kama anapata pia pesa za wizi na ubadhirifu kwa mwajiri wake. Kwakifupi hapa watapata wateja wasio na taarifa za kutosha but wenye uelewa mpana hawatowapata
 
Ntashindwaje kulipa kama wanakata kutoka kwenye mshahara directly mkuu?
 
Kuna tofauti gani na Ile ya Mikopo ya nyumba kutumia mshahara? Ambayo ulikuwa unawekeza kiasi Fulani Halafu unaanza kukatwa kwenye mshahara!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…