Wanachama wa vyama vya siasa na wadau wa siasa kwa ujumla acheni mihemko, mizaha na matusi kwenye mijadala yenye maslahi muhimu kwa taifa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kuweni wastahimilivu na wenye subra ikiwa hoja, mitazamo, maoni na fikra tunduizi za wadau kwenye masuala mbalimbali ni nzito, za maana na muhimu zaidi ya mawazo, maoni au mitazamo yenu ambayo labda ni dhaifu na yasiyo na mashiko kwa wakati huo.

Ikiwa umefikia ukomo wako wa mwisho wa mawazo mapya na fikra mbadala, huna sababu hata moja kulazimisha hoja au kuhitimisha maoni yako dhidi ya mjadala mahususi jukwaani kwa kuporomosha dhihaka, kejeli na pengine matusi ya nguoni kwa mtoa hoja au wadau na wachangiaji wengine.

Tumia haki na uhuru wako wa kujieleza kwa staha na kuchochea uhai na afya ya mijadala ya kistaarabu ili hatimae kwa pamoja tujenge Taifa au jamii iliyostaarabika na yenye kuheshimiana.

Hekima ikuelekeze kukaa kimya, ama kuperuzi mada nyingine kwenye majukwaa mengine kujiliwza kidogo au kuchukua nafasi ya kupumzika kidogo ikiwa utakua umejiskia kuchoka kulingana na uwajibikaji wa majukumu mbalimbali ya kila siku.

Kua mstaarabu mwenye weledi na bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda.

Aidha nawatakia wadau wote wa JF utulivu na maandalizi mema katika mapumziko ya sherehe za Christmass na mwaka mpya 2025.πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania
 
Naunga mkono hoja,kuliko kutukana au kuharibu mada,kukaa kimya pia ni busara。

Kwenye bandiko langu hili Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
niliendesha somo la kujifunza kunyamaza
P
 


Je machawa kama ninyi ni wanachama au! πŸ€• maana ni kama mnajisema wenyewe mnaongeaga hapa bila hoja na kuongelea tetesi kila siku. Hii nchi wakati wa hekima umeshapita watu wanatekwa na kuuliwa, wahombea wanaenguliwa , majengo yanaanhuka ovyo oyo, rushwa ndiyo utamaduni wa serikali, upendeleaji na ubaguzi waziwazi hasa balozini, mikataba ya sirisiri mpaka bandari, airports. Usarabu utatoka wapi wakati sheria hazifuatwi. Yaani serikali yenyewe haifuati katiba wala sheria

Juzi watu walikuwa wanafurahia wabunge kupata ajali, mtu wa TRA ameuliwa na wananchi mnafikiri hawa ni wanachama au ni watu waliochoka?. Serikali hii imeoza na kila siku hapa mtaona busara na upendo baina ya watanzania utaendelea kushuka sana. Mama wa sasa na yule wa 2021 hata mimi niko upande wa kumchukia wakati nilikuwa namuunga mkono
 
Shida kubwa iliyopo ni hii hapa; huna mamlaka ya kuwapangia watu kuwa na mtazamo kama wa kwako.

Halafu wakati mwingine ujiulize ni kwa nini watu wanaamua kuwakejeli na kuwafanyia dhihaka? NI kwa sababu ya matendo yenu maovu dhidi yao.
 
Wewe ndio uache mihemko na matusi. Maana wewe ndio chawa usiyejali maslahi ya Taifa zaidi unajali maslahi ya CCM .
Gentleman kua mkweli basi hata kidogo tu,
sijisufii ila angalau nina siha njema na bongo kali,

siwezi na sintaweza kua na mihemko wala kuthubutu kumporomoshea mwananchi yeyote matusi katika jukwaani hili lililosheheni wadau wabobevu na wa heshima sana kwangu,

ila nikiri tu kwamba,
nina udhaifu na mapungufu katika kujizuia na kukudhibiti katika kusema ukweli bila woga wala kificho.
Hata hivyo, siwezi kamwe kujifunza uongo na upotoshaji.
niwie radhi kwa hilo gentleman,

Hata hivyo,
tunapoelekea kuhitimisha mwaka huu 2024, nichukue fursa hii kukuomba msamaha wewe binafsi econonist na wadau wengine ambao kwa namna moja ama nyingine huenda kupitia hoja, makala, maelezo au ufafanuzi wangu uliwakwaza.


ni matumaini yangu,
tunapoelekea mwaka mpya 2025, ambao pia ni mwaka wa uchaguzi, tutakua na mijadala muhimu ya kistaarabu zaidi kwa maslahi mapana ya ustawi wa demokrasia ya Taifa letu.

nakutakia maandalizi mema ya Christmass na heri ya mwaka mpya 2025 in advance.πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania
 
gentleman,
hoja yangu mahususi inasisitiza mno habari ya kujizuia na mihemko na kuupa kipaumbele utulivu na ustaarabu kujieleza, ambao kwakweli ni jambo muhimu na la maana sana katika kuwasilisha maoni na mtazamo wako juu ya mambo kadha wa kadha yanayotokea katika taifa letu.

Mihemko na ghadhab zinakufanya ukose utaratibu mzuri wa kujieleza na matokeo yake kuwapa kazi kubwa sana wadau kukuelewa. Lakini pia kwa kiasi unawakosesha fursa ya kujifunza kwenye maelezo yako yaliojaa ghadhab kuna jambo muhimu la kuongeza Ufahamu na uelewa wa wadau.

Tunapoelekea kuhitimisha mwaka huu 2024, ni muhimu kujipanga2025, kwa kuepuka mawenge katika kureply na kukomenti mambo mahususi kwa kuchanganya hisia ambazo ni artificial dhidi ya uhalisia na ukweli wa mambo.

Nakutakia maandalizi mema ya Christmass na happy new year 2025 in advance πŸ’
 
Kwenye kutoa pongezi tutoe pongezi, tatizo linakuja kwenye kumsifia mtu kwa kupitiliza nadhani hukela watu wengi, (over selling), tukumbuke tunajenga nyumba moja, Vile vile tunajenga jamii ambayo ina uelewa tofauti, (different level of understanding)

Angalizo viongizi wa kitaifa wajitahidi kutunza kauli zao, (public figures have to keep their words), kaulizao huwa beba na kuwabomoa

Mimi binafsi napenda mijadala ya kuelimisha tutabishana kwa hoja siyo mpenzi wa kuanzisha uzi, (thread)
 
Shida kubwa iliyopo ni hii hapa; huna mamlaka ya kuwapangia watu kuwa na mtazamo kama wa kwako.

Halafu wakati mwingine ujiulize ni kwa nini watu wanaamua kuwakejeli na kuwafanyia dhihaka? NI kwa sababu ya matendo yenu maovu dhidi yao.
Gentleman,
sijatumia mamlaka yoyote kutoa hoja hii mahususi humu jukwaani.Hata hivyo sina mamlaka ya kufanya hivyo kabisa, licha ya kwamba pia haiwezekani.

Hayo ni mawaidha yangu kwa wadau muhimu sana wa jukwaa hili. Ni hiyari ya kila mdau kuyaunga mkono ama kutoyazingatia au vinginevyo.

Uhuru na haki ya kutoa maoni kwa kila mwanainchi linabalika kua ni suala la kikatiba na hakuna ubishi kwenye hilo.

Rai yangu,
ni ustaarabu, kustahimiliana na kua na subra tunapojadiliana masuala mbalimbali kama wanachama wa vyama vya siasa, wabobevu na wadau katika siasa, ili hatimae tuwe na Taifa la watu ambao wanaweza kutofautiana kwa hoja na wasiporomosheane matusi wala kupigana lakini wakabaki wamoja, kama ndugu na familia ya Taifa moja la Amani.

Gentleman,
nakutakia Neema na Baraka za Mungu katika kujiandaa na sherehe za Christmass na mwaka 2025.
Mungu akubariki sana πŸ’
 
Unamaanisha wale walompiga kipigo cha mbwa koko Mzee Sinde WARIOBA akiwa kwenye mjadala muhimu wa katiba mpya mbele ya Waandishi wa habari na muda huohuo haohao waliompiga ndio wakamuamlia?
 
🀣Gentleman, wewe ndio uache mizaha kwani wewe hujui huyu mama hapaswi kuendelea? Atupishe. We hujui? Au unafanyia kejeli?
Gentleman,

give me and JF stakaholders a break tafadhali dah 🀣

ati unasema nini?🀣

kua mstaarabu bas.
mwaka ujao, jitahidi kua na mbadala wa maoni, mtazamo na mapendekezo yako.

Mathalani ikiwa unaona Tlaatlaah hastahili kua Waziri kwenye serikali ijayo, make sure unapendekeza anaestahili nafasi bila kuogopa wala kuona haya au aibu. vivyo hivyo kwa diwani, mbunge na Rais,


vinginevyo,
nakutakia maandalizi mema sana ya likizo za Christmass na mwaka 2025πŸ’
 
Mimi siyo mwanachama wa chama chochote lkn hii movie ya KIFO NI KIFO TU a.k.a DRAMA DRAMA ninaifuatilia kwa karibu sana hasa baada ya kuonekana hadharani kwa baadhi ya wahusika ambapo mmoja ana status ya Dereva officer wa tra student imenivutia saaaana.

Ukiongeza lile bus pale palipo na nyama nyiiingi za kuchoma sijui huwa ni za wanyama gani lkn hili la bus nalo kidooogo linipe tabasamu sema malengo ya kuwaunganisha abiria waliokuwemo na yule wa tra hayakutimia hivyo tabasamu langu halikufika kileleni.
 
Tatizo siyo hoja. Tatizo ni pale hoja ya kijinga inapotolewa na mjinga. Wewe ni mjinga kweli kweli na ni hasara kwa nchi hii nzuri
 
pamoja sana gentleman πŸ’ͺπŸ‘Š πŸ™

Nakutakia maandalizi mema ya Christmass na mwaka mpya 2025 πŸ’
 
Changamoto isipo tatuliwa kwa wakati huleta kizungumkuti, unapo unda tume nyuma ya mikamera majibu ya tume nyuma ya pazia,
cha ajabu matukio ambayo yanafanana na ulilo undia tume yanapo tengeneza muendelezo husababisha mishangao na mabalaa endelevu
 
Unamaanisha wale walompiga kipigo cha mbwa koko Mzee Sinde WARIOBA akiwa kwenye mjadala muhimu wa katiba mpya mbele ya Waandishi wa habari na muda huohuo haohao waliompiga ndio wakamuamlia?
gentleman,
mawaidha yangu kwa wadau ni katika kujijengea uwezo wa kustahimiliana na kuvumiliana miongoni mwetu humu jukwaani kabla hatujakutana field. Vinginevyo, pasipokua na ustaarabu na subra kwenye mijadala humu ndani matokeo yake itakua ngumu kuvumiliana tukiwa field, maana mafarakano na malumbano ya hoja yasio na ustaarabu, matokeo yake ni matukano na pengine mapigano kule field.

Tujifunze kua na subra,
kujadiliana kwa hoja, lakini pia kukubaliana kutokukubaliana kwa hekima, salama na amani.

my friend,
marry Christmas and happy new year2025 in advance
 
gentleman,
nadhani una hoja mahususi unajaribu kuijenga na kutaka kuitoa, lakini nadhani ingefaa zaidi ingejitegemea.
hata hivyo haidhuru,

ikiwa hoja na maelezo yako yakawekwa kwenye mpangilio na mtiririko rasmi, wadau wasiofahamu chochote kuhusu hilo wangepata kujua, kuelewa na kuongeza ufahamu na uelewa wao juu ya jambo lenyewe,
na ndiyo maana nasisitiza ustaarabu katika kuwasilisha mijadala lakini piakujadiliana mambo mbalimbali ili hatimae tuwe na uelekeo na hitimisho la amani hata kama hatujakubaliana mawazo, maoni na mtazamo.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Tatizo siyo hoja. Tatizo ni pale hoja ya kijinga inapotolewa na mjinga. Wewe ni mjinga kweli kweli na ni hasara kwa nchi hii nzuri
gentleman,
jambo la maana zaidi, ingekua sasa muerevu kama wewe unakuja na mawazo mapya na fikra mbadala na bora zaidi ya hoja mahususi mezani,

kuexpose level ya IQ yako kwa ghadhabu na mihemko ya kiwango cha juu namna hiyo, ni kudhihirishia wadau wa Jf jinsi ulivyokata tamaa, huenda kwasababu ya kulemewa na madeni ya kausha damu, huku chrismass na mwaka mpya ndiyo hizo zinabisha hodi.

mbaya zaidi katika mwaka huu unaoisha hujatimiza hata lengo moja katika malengo yako uliojiwekea kwa mbwembwe nyingi sana mwanzoni mwa mwaka2024

Mary Christmas and happy new year in advance gentleman..
 
Ukileta za kuleta .....nina kupa vivyohivyo. Paaap. Mumo humo

haswa waleeee

Wengine humu wakishashindwa hoja, wanarudi na vi ID vya wanazotumia kule kwenye kula matunda kwa masihara na kuanza kurusha manina manyoko.

Nawajueni

Wakome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…