Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kuweni wastahimilivu na wenye subra ikiwa hoja, mitazamo, maoni na fikra tunduizi za wadau kwenye masuala mbalimbali ni nzito, za maana na muhimu zaidi ya mawazo, maoni au mitazamo yenu ambayo labda ni dhaifu na yasiyo na mashiko kwa wakati huo.
Ikiwa umefikia ukomo wako wa mwisho wa mawazo mapya na fikra mbadala, huna sababu hata moja kulazimisha hoja au kuhitimisha maoni yako dhidi ya mjadala mahususi jukwaani kwa kuporomosha dhihaka, kejeli na pengine matusi ya nguoni kwa mtoa hoja au wadau na wachangiaji wengine.
Tumia haki na uhuru wako wa kujieleza kwa staha na kuchochea uhai na afya ya mijadala ya kistaarabu ili hatimae kwa pamoja tujenge Taifa au jamii iliyostaarabika na yenye kuheshimiana.
Hekima ikuelekeze kukaa kimya, ama kuperuzi mada nyingine kwenye majukwaa mengine kujiliwza kidogo au kuchukua nafasi ya kupumzika kidogo ikiwa utakua umejiskia kuchoka kulingana na uwajibikaji wa majukumu mbalimbali ya kila siku.
Kua mstaarabu mwenye weledi na bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda.
Aidha nawatakia wadau wote wa JF utulivu na maandalizi mema katika mapumziko ya sherehe za Christmass na mwaka mpya 2025.🐒
Mungu Ibariki Tanzania