Wanachama wa vyama vya siasa na wadau wa siasa kwa ujumla acheni mihemko, mizaha na matusi kwenye mijadala yenye maslahi muhimu kwa taifa

Kuweni wastahimilivu na wenye subra ikiwa hoja, mitazamo, maoni na fikra tunduizi za wadau kwenye masuala mbalimbali ni nzito, za maana na muhimu zaidi ya mawazo, maoni au mitazamo yenu ambayo labda ni dhaifu na yasiyo na mashiko kwa wakati huo.

Ikiwa umefikia ukomo wako wa mwisho wa mawazo mapya na fikra mbadala, huna sababu hata moja kulazimisha hoja au kuhitimisha maoni yako dhidi ya mjadala mahususi jukwaani kwa kuporomosha dhihaka, kejeli na pengine matusi ya nguoni kwa mtoa hoja au wadau na wachangiaji wengine.

Tumia haki na uhuru wako wa kujieleza kwa staha na kuchochea uhai na afya ya mijadala ya kistaarabu ili hatimae kwa pamoja tujenge Taifa au jamii iliyostaarabika na yenye kuheshimiana.

Hekima ikuelekeze kukaa kimya, ama kuperuzi mada nyingine kwenye majukwaa mengine kujiliwza kidogo au kuchukua nafasi ya kupumzika kidogo ikiwa utakua umejiskia kuchoka kulingana na uwajibikaji wa majukumu mbalimbali ya kila siku.

Kua mstaarabu mwenye weledi na bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda.

Aidha nawatakia wadau wote wa JF utulivu na maandalizi mema katika mapumziko ya sherehe za Christmass na mwaka mpya 2025.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Bado mtu nzima upo CCM?!
 
Changuzi mnazikuza tu hata huu uchafu uliopita unaitwa uchaguzi. Mimi naongelea hali halisi za watu na mambo tunayo yaona ground. Hizi chaguzi ni ratiba tu. Tanzania tuna dharaulika kuliko 2021 na 2022
Nadhani wewe mwenyewe ni shuhuda. Mitaani mijini na vijijini kumetapakaa frem za maduka, masoko minada na magulio, hiyo ni ishara uchumi wa nchi na maisha ya waTanzania ni bora na mazuri zaidi kiuchumi...

Nenda kwenye stand ya sgr, stand ya mabasi ya Magufulu na hata huko mikoani, nenda airport au bandarini, watu wanasafiri na kusafirisha biashara na bidhaa mbalimbali kuelekea maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, hii ikiashiria uchumi wa waTanzania ni Imara mno.

Huenda unajidharau mwenyewe gentleman. Tanzania inaaminika, inakubalika na inaheshimika mno Africa na duniani kote na ndiyo maanatunaweza hata kuongoza mataasisi makubwa ya ulimwengu.

kwa kuhitimisha,
uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025 utakua ni wa kihistoria, kwa Tanzania kuchagua rais mwanamke kwa kishindo kikuu 🐒
 
Bado mtu nzima upo CCM?!
Gentleman,
huna haja ya kubabaika kwenye hilo,
ni uhuru na haki ya kikatiba kwa kila mTanzania kuamua kwa hiyari yake mwenyewe, tena bila aibu kua mwana chama wa CHAUMA , UDP, CCK, n.k

akiamua kua mercenaries miongoni mwa vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi nayo pia anaweza kufanya hivyo 🐒
 
Huwa nafikiri mtu akiwa CCM ni kwa sababu za maslahi binafsi au ni mtu asiyenazo vizuri.
 
Kuweni wastahimilivu na wenye subra ikiwa hoja, mitazamo, maoni na fikra tunduizi za wadau kwenye masuala mbalimbali ni nzito, za maana na muhimu zaidi ya mawazo, maoni au mitazamo yenu ambayo labda ni dhaifu na yasiyo na mashiko kwa wakati huo.

Ikiwa umefikia ukomo wako wa mwisho wa mawazo mapya na fikra mbadala, huna sababu hata moja kulazimisha hoja au kuhitimisha maoni yako dhidi ya mjadala mahususi jukwaani kwa kuporomosha dhihaka, kejeli na pengine matusi ya nguoni kwa mtoa hoja au wadau na wachangiaji wengine.

Tumia haki na uhuru wako wa kujieleza kwa staha na kuchochea uhai na afya ya mijadala ya kistaarabu ili hatimae kwa pamoja tujenge Taifa au jamii iliyostaarabika na yenye kuheshimiana.

Hekima ikuelekeze kukaa kimya, ama kuperuzi mada nyingine kwenye majukwaa mengine kujiliwza kidogo au kuchukua nafasi ya kupumzika kidogo ikiwa utakua umejiskia kuchoka kulingana na uwajibikaji wa majukumu mbalimbali ya kila siku.

Kua mstaarabu mwenye weledi na bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda.

Aidha nawatakia wadau wote wa JF utulivu na maandalizi mema katika mapumziko ya sherehe za Christmass na mwaka mpya 2025.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Acha uchawa na upumbavu wakati waTanzania walio wengi wanaishi kwa taharuki! Keki ya Taifa ikimegwa na wachache!! Ficha aibu zako!
 
mihemko sio deal na sio ustarabu mzuri hata wa kufikia malengo binafsi tu gentleman, sembuse malengo ya jumla?

nadhani alie too late inaweza kua ni wew binafsi pekee. kwamba mwaka unaishi, hujatimiza lengo hata moja,eti sasa hivi ndio unachanganya miguu 🤣

that is too late,
relax na ujipange kwajili ya mwaka ujao gentleman.

kama taifa, kistaarabu kabisa tunajipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, baada ya kumaliza kwa mafanikio makubwa sana uchaguzi muhimu wa kihistoria wa serikali za mitaa.

ustarabu umefanya uchaguzi huo muhimu kua wa amani na Utulivu sana 🐒
Ustaarabu ungekuwepo mngeheshimu sanduku la kura
 
Huwa nafikiri mtu akiwa CCM ni kwa sababu za maslahi binafsi au ni mtu asiyenazo vizuri.
Of course yes,
inaweza kua ni kweli,
Kwasasababu ni muhimu sana kila mwananchi mTanzania kua mwana chama wa CCM, kwa maslahi mapana ya umoja, amani na mshikamano wa Taifa letu.

Na kwakweli kua mwana CCM ni uzalendo wa kiwango cha juu sana.
Kua upinzani Tanzania, watu wengi wa ndani na nje ya nchi wanaona ni kama ushirikina au utumwa tu, kwasabb vyama vingi vya upinzani viko chini na vinafadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi 🐒
 
Gentleman,
Kama mdau muandamizi katika siasa za Tanzania, mwaka ujao wa fedha na uchaguzi mkuu, utakua ni mwanzo wa mageuzi na mabadiliko makubwa mno ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika Taifa letu.

Tanzania inakwenda kuweka historia katika bara la Africa kwa kufanya uchaguzi mwingine ambao ni wa amani zaidi, pengine kuliko hata ule wa marekani katika ngazi za ubunge, udiwani na urasi.

Tujipange vizuri kama Taifa ndrugu zango 🐒
Wadanganye watoto
 
Ustaarabu ungekuwepo mngeheshimu sanduku la kura
kwasasababu ya ustarabu na kuaminika kwa CCM,
waTanzania kwa mamilioni yao waliojitokeza kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na wakaipigia kura nyingi sana na za kishindo CCM.

Waliopuuza kujiandikisha kwasabb zao binafsi, leo hii ndio hao wanung'unikaji wakubwa kana kwamba kuna kitu kitabadilika

Ni muhimu kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao 2025 bila kujibakiza 🐒
 
Of course yes,
inaweza kua ni kweli,
Kwasasababu ni muhimu sana kila mwananchi mTanzania kua mwana chama wa CCM, kwa maslahi mapana ya umoja, amani na mshikamano wa Taifa letu.

Na kwakweli kua mwana CCM ni uzalendo wa kiwango cha juu sana.
Kua upinzani Tanzania, watu wengi wa ndani na nje ya nchi wanaona ni kama ushirikina au utumwa tu, kwasabb vyama vingi vya upinzani viko chini na vinafadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi 🐒
Ukiangalia wapenzi wengi wa CCM ni watu wajinga jinga au wenye tamaa za kupata vitu kwa mteremko bila kufuata haki.
 
Gentleman kua mkweli basi hata kidogo tu,
sijisufii ila angalau nina siha njema na bongo kali,

siwezi na sintaweza kua na mihemko wala kuthubutu kumporomoshea mwananchi yeyote matusi katika jukwaani hili lililosheheni wadau wabobevu na wa heshima sana kwangu,

ila nikiri tu kwamba,
nina udhaifu na mapungufu katika kujizuia na kukudhibiti katika kusema ukweli bila woga wala kificho.
Hata hivyo, siwezi kamwe kujifunza uongo na upotoshaji.
niwie radhi kwa hilo gentleman,

Hata hivyo,
tunapoelekea kuhitimisha mwaka huu 2024, nichukue fursa hii kukuomba msamaha wewe binafsi econonist na wadau wengine ambao kwa namna moja ama nyingine huenda kupitia hoja, makala, maelezo au ufafanuzi wangu uliwakwaza.

ni matumaini yangu,
tunapoelekea mwaka mpya 2025, ambao pia ni mwaka wa uchaguzi, tutakua na mijadala muhimu ya kistaarabu zaidi kwa maslahi mapana ya ustawi wa demokrasia ya Taifa letu.

nakutakia maandalizi mema ya Christmass na heri ya mwaka mpya 2025 in advance.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Gentleman una akili sana , sema kuna wakati unajizima data
 
Gentleman una akili sana , sema kuna wakati unajizima data
Gentleman,
I can confirm to you without fear of contradictions kwamba , wadau na members na viongozi wote JF ni ndugu, marafiki, jamaa, walimu na wanafunzi wangu katika mambo mengi sana kijamii, kisiasa, kiuchumi, kitaifa na kimataifa..

Nitawaheshimu na kuwapenda upeo, maana uelewa na ufahamu wangu wa leo juu ya mambo mbalimbali ni tofauti mno na kabla sijajiunga JF, na huenda viongozi wengi wa kisiasa wanafanya kama wanavyofanya kwasasababu hawajapata fursa kwenye platform kama hii muhimu, ili walau kupata picha, maoni, hisia, mapendekezo, matamanio, mahitaji na matarajio ya wananchi kutoka kwao.

mimi ni mtu wa watu, kiongozi wa kisiasa wa kisasa, mwenye nia, dhamira dhabiti, lakini mwenye na maono ya mbali na bongo kali sana, kwa maslahi mapana ya jamii ninayoingoza lakini pia kwa taifa kwa ujula..

nachukia sana rushwa, majivuno, uvivu na utovu wa nidhamu 🐒
 
Ukiangalia wapenzi wengi wa CCM ni watu wajinga jinga au wenye tamaa za kupata vitu kwa mteremko bila kufuata haki.
hilo ni kosa kisiasa,

mwanasiasa mwerevu hawezi kamwe kumdhihaki mpiga kura asie unga mkono sera au chama chake, na wala hawezi kuthubutu kumbeza alie na mawazo tofauti dhidi ya anachoamini yeye.

bali atatumia mawazo mapya na fikra mbdala kumshawishi mpiga kura huyo ili hatimae amuunge mkono na awe upande wake.

Mwanasiasa asie na maono ya mbali na aliepoteza uelekeo na kukata tamaa. Kwanza hajui kua politics is about numbers. Kukuwaita wapiga kura wajinga ni kwamba, you are rejecting numbers in your side instead of adding them.

Zaidi sana,
mwanasiasa aliefilisika hoja, hajui kwamba politics has two constants i.e interests and betreyal. Ni lazima kuishi katika mazingira hayo kwa kuchunga sana interests za wanachama wako wote na maslahi ya taasisi yako kwa ujumla. Ukimesup kidogo tu utajikuta uko betreyed hata na wanachama wako na utabaki pekeyako na dhihaka zako, unless hizo dhihaka ziwe kipaumbele cha chama chako.

Jambo la mwisho,
ni kujitenga na majivuno, kujipa umuhimu au utakatifu wa kipekee kanakwamba wewe ni malaika mweupe kama pamba, huna tamaa, huna kosa na wala hata chooni huendi.

Na kwamba utakachosema wewe ndicho bora zaidi kuliko wengineo na ni wewe pekee tu ndiye mkamilifu licha ya kwamba maoni n mtazamo wako wa kuhisi ni useless na nonsense kabisaa 🐒
 
Gentleman,
I can confirm to you without fear of contradictions kwamba , wadau na members na viongozi wote JF ni ndugu, marafiki, jamaa, walimu na wanafunzi wangu katika mambo mengi sana kijamii, kisiasa, kiuchumi, kitaifa na kimataifa..

Nitawaheshimu na kuwapenda upeo, maana uelewa na ufahamu wangu wa leo juu ya mambo mbalimbali ni tofauti mno na kabla sijajiunga JF, na huenda viongozi wengi wa kisiasa wanafanya kama wanavyofanya kwasasababu hawajapata fursa kwenye platform kama hii muhimu, ili walau kupata picha, maoni, hisia, mapendekezo, matamanio, mahitaji na matarajio ya wananchi kutoka kwao.

mimi ni mtu wa watu, kiongozi wa kisiasa wa kisasa, mwenye nia, dhamira dhabiti, lakini mwenye na maono ya mbali na bongo kali sana, kwa maslahi mapana ya jamii ninayoingoza lakini pia kwa taifa kwa ujula..

nachukia sana rushwa, majivuno, uvivu na utovu wa nidhamu 🐒
Basi kama wewe ni kiongozi mwanasiasa wa kisasa usijifunze yale ya wanasiasa niwajuavyo wakwetu na mambo yao,ukifanikiwa hilo hata wadau humu wataacha kukupopo mawe.Nakatika mafunzo ya siasa uliyoyapata kutoka kwao yafanyie upya mapitio huru kwa ukisasa unaousema na ujitenge na maovu yao katika siasa a.k.a sii hasa.
 
Relax and thank you very much gentleman

I wish you mery Christmas and happy new year 2025🐒
 
Ila kwa maoni yako unaona upo ulazima wake?Kwa hali na mazingira ya sasa katika chaguzi zetu?
 
uchaguzi ni uchaguzi tu,
dosari na kasoro ndogo haziepukiki na kiwango cha ustahilivu na uelewa kwa wapiga kura ni tofauti sana dhidi ya dosari hizo.

Na kwasasababu uchaguzi huo ni wa kikatiba, ni Lazima ufanyike vinginevyo tutakua tumekiuka katiba.

Jambo la maana zaidi kwa wanasiasa na na wapiga kura ni kua serious katika kuhakikisha wanajiandikisha kupiga kura, wanakwenda kuhakiki majina yao kabla ya siku ya uchaguzi, ili kuondoa sintofahau na uzushi eti jina langu limeondolewa au halipo, kumbe umekutana na orodha ya majina 4000 ukajikuta umechoka hata kabla ya kuanza kutafuta jina lako.

kumbe ungehakiki jina lako mapema,
unataja tu uko namba ngapi kwenye orodha na unaelekezwa pa kupigia kura, within 3umemaliza unakwenda nyumbani kusubiri matokeo.

Nikuhakushie tu gentleman,
tunajifunza kutokana na makosa. Dosari na kasoro ndogo zilizojitokeza kwenye uchaguzi ulopita, haziwez kujirudia tena kwenye historia ya nchi yetu.

Tume huru makini sana ya uchaguzi ipo, mahakama huru zipo, vyombo vya ulinzi na usalama vipo, shirikisho la umoja wa vyama vya siasa nchini lipo, waangalizi wa uchaguzi kitaifa na kimataifa wapo.

Muhimu ni wanasiasa na wapiga kura kuhamasishana na kujizatiti kweli na kujitokeza kupiga kura kwa pamoja na kuamua mustakabali wa uongozi wa Taifa letu kwa amani na utulivu.

Binafsi naona inawezekana kabisa gentleman 🐒
 
Je na tuseme uchafuzi ni uchafuzi? Kwa namna hiyo na maelezo yako ukiingia kwenye siasa na ukapewa nafasi wewe ni janga zaidi ya wana sii hasa wakwetu leo hii,wanao sema uchaguzi/uchafuzi ulikuwa huru na wahaki ila zilikuwepo kasoro ndogo ndogo,badala ya kusema ukweli hapakuwa na uchaguzi ila uchafuzi na uhuni ulioratibiwa na waonao ni wamiliki wa taifa.
 
ukienda kwenye huku ukiwa na dhana potofu kama hiyo utaambulia hicho ndicho kilichokua kwenye mindset yako, kwasabb you will completely not be serious to the whole process..

ndiyo ile waswhahili walisema,awazalo mjinga ndilo litakalo mtokea.

If you think and trust in failure, you will fail taribly without contradictions 🐒

jifunze kuziendea changamoto kwa kwa utulivu wa fikra, hekima na busara ili hatimae uibuke na suluhusho muafaka la uhakika,

vinginevyo uta mbwelambwela mno bila muafaka bila suluhisho 🐒
 
Back
Top Bottom