Wanachama wa Yanga kutibiwa kwa bei ya punguzo kwenye Hospitali za Agakhan

Wanachama wa Yanga kutibiwa kwa bei ya punguzo kwenye Hospitali za Agakhan

Sawa, vizuri, ila isijekuwa ni yale mapunguzo ambayo hata chenji hurudishiwi maana hiyo sarafu hakuna.

Ugonjwa: Malaria.
Gharama za kawaida: Tsh 300,000
Gharama kwa mwanayanga: Tsh 299,960
 
Punguzo rahisi kabisa la matibabu ni kuwa mwanachama wa Bima ya Taifa (NHIF), na sio hizo porojo za kujiunga uanachama wa Yanga. Bila NHIF, punguzo la matibabu Agha Khan bado ni ghali kulinganisha na hospitali nyingi nchini kwa matibabu ya bila pungozo
 
Wanajua washabiki wa Yanga wana raha hawana maradhi kama pressure na visukari vinavyosababishwa na msongo wa mawazo ya kufungwa kama wale jirani zetu
 
Mkuu hayo ni masuala ya kimkataba hayatakiwi kwenda hewani kwa kila mtu. Ila Wahusika (Wachezaji, Wanachama na Mashabiki) watajulishwa vipengele vyote vya mkataba.
Kwa gharama za Aga Khan hata mngepata punguzo la 50% bado ni wachache mno wangemudu hizo gharama. Hiki ni kilemba cha ukoka tu lakini kwa vile watu wenyewe ni nyani wanachekelea tu,naona huruma mimi
FB_IMG_1700028629335.jpg
JamiiForums-1395422526.jpg
FB_IMG_1707213280656~3.jpg
 
Attachments

  • JamiiForums-1395422526.jpg
    JamiiForums-1395422526.jpg
    93.3 KB · Views: 3
Inayoongelewa hapo ni agakhan polyclinics sio ile makao makuu. Hata kwenye bima za afya nyingi hawakubali kutibiwa hapo ila wanakubali kutibiwa kwenye zile polyclinic zao.
 
Sasa hizo hospital zitafurika kina mzee mpili tu
 
Punguzo rahisi kabisa la matibabu ni kuwa mwanachama wa Bima ya Taifa (NHIF), na sio hizo porojo za kujiunga uanachama wa Yanga. Bila NHIF, punguzo la matibabu Agha Khan bado ni ghali kulinganisha na hospitali nyingi nchini kwa matibabu ya bila pungozo
Mnaoneea wivu hadi wagonjwa
 
Kwa namna hii Nchi ilivyo na Ujanja janja hawachelewi kutoa punguzo la elfu 7 ama elfu 5 Kwa Kila huduma

Wakati gharama za matibabu hapo Agha Khan ni shilingi 700,000 hadi milioni kadhaa kutegemeana na ugonjwa

Anyways, Kila la kheri Mtani 🤗
Yanga ina Wagonjwa Wengi unataka hospital ifilisike?
 
Back
Top Bottom