dong yi
JF-Expert Member
- Jan 31, 2016
- 5,906
- 8,243
hata upande wa klabu ni hivyo hivyo,.....Azam Media kuna shida kubwa ya viongozi wengi kukosa weledi na dira ya wapi wanataka taasisi hiyo kuelekea.
Na shida kubwa ni aina ya ajira zao kuwa za kijamaa na urafiki, na sio uzoefu na taaluma. Ndiyo maana haya yanatokea.
Viongozi wengi pale hawafukuziki hata wafanye makosa ya namna gani, kwa sababu labda wameletwa na Yusuf.
Niliwahi kuzungumza na Tido wakati akiwa pale, nikimuuliza kukosa kwao kukua, kwa maana ya kuongeza channels za michezo.
Alisema kuwa, amekosa timu sahihi ya kukuza taasisi, kwani wakati wote akitoa maelekezo/ mwongozo huwa kuna utekelezaji hafifu.
Fikiria, baada ya kustaafu Tido kwa sasa Kahemele ndiyo kiongozi Mkuu pale, ila yeye yuko kwenye nafasi hiyo kwa kuwa walikuwa naye kwenye timu ya Azam kabla kuanza TV.
Hadi sasa wana miaka kumi tangu walipoanza, ila bado wana channels saba au nane tu, nyingine zote siyo zao. Kuna shida pale.
Ova
jamaa hawapo serious