Wanachofanya AZAM TV kwenye mpira ni uhuni na utapeli, wadau amkeni

hata upande wa klabu ni hivyo hivyo,.....

jamaa hawapo serious
 
kuna zile azam one na two sielewagi ni moja au zina utofauti,maudhui yanajirudia ya one unayakuta two na two unayakuta one,kuna ile cinema zetu movie za ajabu ajabu tamthilia mbovu

sport hd hazieleweki zinaingiliana maudhui pia,azam nimeambulia channel ya kix tu naangalia zangu waki yuen biao na kina samu hongi enzi zao lakini ukijichanganya e movie,movie moja unaangalia masaa ma5 kuna matangazo ya waarabu muda wote[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na hakuna offer ya aina yoyote kama wenzao startimes, DStv,mzee bakhresa aache tamaa hela anazopata ni nyingi sana kupitia ving'amuzi vyake
 
Hivi kwanini TBC wasiwe na channel ya michezo tu, japo hata waoneshe ndondo cup, chandimu na umiseta?
Kuwategemea Azam pekee ndio tunaishia kupata tabu hizi.

Ngoja nimwambie Nape na Ayubu walichukue hili kama majaribio ya kuwa bora zaidi kurusha matangazo.

Hatuwezi kuwa na TBC chovu.
 
Wakuu Azam tv hivi karibuni imeanza uhuni ambao lazima ukemewe!

Azam walijinasibu kuonyesha ligi ya ufaransa (Ligue 1) ligi ya ujerumani (bundesliga) ligi kuu ya Tanzania (NBC) na hivi karibuni wakasema na Ligue ya waarabu kwa kina Ronaldo...
Nakuuliz hivi mwezi wa June fifa world cup je, zitaonyesha mpira ya world cup ipo kweny Azam tv?
 
Hivi kwanini TBC wasiwe na channel ya michezo tu, japo hata waoneshe ndondo cup, chandimu na umiseta?
Kuwategemea Azam pekee ndio tunaishia kupata tabu hizi.
TBC pale wamejaa wazee tupu mbaya zaidi wanawalisha ujinga na uzembe baadhi ya vijana wa hapo ndio mana TBC hakuna content inayofatiliwa.

atleast sasa hv wameshtukia fursa ya kuonyesha mechi za CAF na Fifa kitu ambacho walitakiwa kukifanya tangu kitambo.
 
Siku azam wakilogwa copyright ya kuonyesha NBC premiere L. Ikaingia dstv au kwingine kokote,basi hapo ndiyo nafunga nao mkataba rasmi kulipia kifurushi.
Unaweza kudhani hii itasaidia ila nakuambia ligi itaporomoka vibaya mno.

Kabla ya hii copyright ya Sasa ya Azam kuonyesha ligi, pia DStv walitaka kuonyesha ligi ila wao walitaka kuonyesha mechi za simba na Yanga tuu wakati Azam yeye anaonyesha mechi zote za ligi.
 
Hahahahah!!!!. ni movie za uturuki, ufilipino, documentary za mpira kila siku msuva, na dogo fulani hivi wa kike anachezea twiga stars. kuna baadhi ya channel kamera low quality utazani tupo miaka ya 1900's.
 
Ila tuache masihara Zanzibar ingekuwa inajitegemea kama nchi pengine ingekuwa mbali sana imagine kwa sh 12000 tu kwa mwezi naangalia ligi zote kubwa Ulaya mfano Leo Kuna FA cup final, DFB Pokal, Coupe de France, Caf champions ligi final, zote nimeziangalia kasoro huu utumbo wa NBC tu ndio huwezi kuona.
 
Hama nenda DSTV



KAZI ni kipimo cha UTU
 
Unawaza azam anaweza akawafurahisheni na kuwaridhisha wateja wake wote mamilioni nchini. Lazima mtakuwepo pimbi kama nyinyi msioona jema popote. Hamna shukrani kwa hata hicho anachofanya mtamsaidia nini kumboresha?
Mkuu ukimjibu mdau yeyote kwa kumwelewesha itapendeza sana mkuu wangu.
 
Kwenye EURO 2024 ni bora kutumia DSTV tu huko Azam level zao ni ligi za kwetu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…