Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Utandawazi kwa muda mrefu umekuwa dhidi ya maslahi ya Waislamu, kiasi kwamba kuna dhana iliyoenea mijini na mitaani na kwa wanachama wengi wa JF kwamba Uislamu ni shida duniani, na kwamba hii ni dini ya kuripua na kuua watu.
Ukweli wa matukio yanayoendelea sasa duniani na yale ya kihistoria ni kinyume kabisa na dhana hiyo, na inashangaza kwamba wanaoamini hivyo hawaoni haya kuleta madai hayo.
Kinachofanywa na Mayahudi kule Gaza na Palestina kwa takriban miaka miwili ni kitu kibaya sana kiubinadamu. Kwa bahati, safari hii ubaya huo umekuwa ukioneshwa mubashara kote duniani, japo haijasaidia sana kusitisha balaa hilo kwa Wapalestina.
Mbinu wanazotumia Mayahudi kwa Waislamu wa Palestina zinalingana sana na zile walizotumia Wakristo kwa taifa la Kiislamu la Bosnia katikati ya Ulaya. Wote wamekuwa wakiwaua Waislamu bila huruma na kubomoa majumba yao.
Kilichozidi kwa Mayahudi ni ukatili wa kuwanyima chakula, na wanapokuwa wamekuwa na njaa sana, wanawawekea chakula sehemu kama wanavyotegeshwa wanyama, na wanapofika wanawaua kwa risasi. Mpaka sasa, inakisiwa wameshawaua 65,000 na idadi kubwa kuwafanya wawe vilema wanaoishi kwenye mahema.
Ama kwa upande wa Bosnia, Wakristo waliua takriban watu laki tatu kwa kuvamia vijiji na miji yao na kuwamiminia risasi kila waliyempata bila kubagua umri wala jinsia. Baada ya hapo, walibomoa majumba yao na kuchoma moto misikiti.
Kinachofanana sana kwa mazingira kati ya wauwaji hawa ni kukaliwa kimya wanachokifanya na kuungwa mkono na mataifa makubwa.
Kilichotofauti ni kuwa Katibu Mkuu wa UN wakati wa mauaji ya Wakristo kwa Waislamu katika vita vya Bosnia alikuwa na sera za kuunga mkono Wakristo wenzake, wakati yule anayeshuhudia mauaji ya Wapalestina kutoka kwa Mayahudi, japo ni Mkristo, amepinga waziwazi unyama huo.
Kwengineko ambako Wakristo wamewaua mamilioni ya Waislamu bila sababu za maana ni Iraq, Afghanistan, na Libya, chini ya watawala wao wenye misimamo mikali ya Kikristo.