The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
1. Kabla ya mgomo Wafanyabiashara wamekaa vikao zaidi ya 10 na mamlaka ya mapato TRA ,hawakupata majibu.
2.kabla ya mgomo Wafanyabiashara wamekaa vikao na serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Ilala wakiomba Waziri wa fedha afike kuwa sikiliza lakini Waziri wa fedha hakuwahi kwenda.
3.Mkuu wa Wilaya ya Ilala amepambana sana kuhakikisha mgomo hautokei (Wafanyabiashara wanampongeza) Mkuu wa wilaya ya ilala akaomba Wafanyabiashara wasubiri mwezi mmoja ,ili awasiliane na Viongozi wake kwanza
Mwezi ukaisha Mkuu wa Wilaya akapuuzwa na viongozi wake wa Juu.
4. Mkuu wa Mkoa mara zote hizi hakuwahi kuonekana katika vikao chochote cha Wafanyabiashara, wala hakuwahi kusaidia kupeleka malalamiko ngazi za Juu.
Ameonekana Jana tu, ktk Vitisho.
5. Viongozi wa Wafanyabiashara wakaomba waende Dodoma kuonana na Waziri wa fedha ili madai yao yaingizwe katika Bajeti hii na sheria mpya ya fedha- Wakapuuzwa
6. Viongozi wa Wafanyabiashara kupitia kamati yao Maalumu iliyoundwa wakati Waziri Mkuu alipofika Kariakoo iliwajulisha wafanya biashaara wenzao kuwa hoja zao zote 27 zimetupiliwa mbali.
7. Katika hoja zao 27 za awali,Wafanyabiashara wanahoja za haraka 7 zikifanyiwa kazi watafungua Maduka yao wakati wanasubiri serikali wafanyie kazi hizo 20.
8. Hoja hizo ni
9. Leo saa 7: 00 mchana, Dodoma, Waziri wa fedha na Waziri wa viwanda na biashara wamekutana na viongozi wa wafanya biashara(Mrejesho utaletwa hapa hapa).
Msimamo wa wafanyabishara ni kwamba hawataki kusikia lolote kutoka kwa Mawaziri hao baada ya kuongopewa kwa muda mrefu
10. WANATAKA RAIS AENDE KARIAKOO au KAULI YA RAIS KUHUSU HOJA ZAO
Pia soma:
News Alert: - Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Soma:Chalamila awasili Kariakoo awaambia Wafanyabiashara “Fungueni maduka, Biashara sio Siasa”
Soma: Chalamila: Kama Serikali inatuma vikosi kupigana Congo, inashindwa kuja kupigana Kariakoo?
Soma: Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam umenikuna sana leo sakata la wafanyabiashara Kariakoo

- Kupunguza faini ya kuto toa risiti ambayo kwa sasa ni 15M
- Kuondoa service levy.
- Kamtakamata ya TRA mitaani
- Kunyan'ganywa kwa VAT baadhi ya wafanya biashara
- VAT kukusanywa bandarini,airport na ktk Mipaka
- Kuzuia wachina na Wageni ktk biashara ndogondogo Kariakoo
- VAT ianze Tsh millioni 500 hadi Tsh billioni 1 badala ya sasa ya Tsh million 200