Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Mkuu ni chaguo lao sababu anakuwa hana namna. Mzigo huu hapo, bei M230. Lipa upewe risiti ya M50 au usinunue.Ewaa....jamaa hawawezi kutoa risiti kwasababu wanaleta mzigo kupitia makambale na hawapewi documents. Lakini hio pia ni chaguo lao. Wapo wafanyabiashara wengi tu wanaleta mzigo wenyewe. Mfano mimi. Tra hata uwe compliant 100% lazima wakutafutie zengwe, ni wewe tu una deal nao vipi.
Binafsi naona ni rahisi sana kuikusanya VAT inapoanzia kisha ukaacha iflow automatic. Swali ni kuwa, kwanini inapoanzia inakuwa shida? Kwanini hawa wa kati ndo wabanwe sana? Mbona ni rahisi zaidi kubana viwandani na bandarini kila anayenunua anunue na risiti kuliko kuacha mzigo ufike huku katikati ndo uanze kubana risiti? Huko juu ukishanunua kwa risiti ukalipa VAT lazima utataka uikusanye kupunguza deni ulilolipa na kuikusanya ni kutoa risiti. Sasa kwanini inakuwa ngumu?