Wanachotamani na wanachoshikililia MATAGA ni Mbowe kuwapigia magoti jambo ambalo mpaka leo hawaamini kuwa halitokei kutoka kwa Mbowe

Hujui nature na history ya Mbowe - kaa chini kijana. Ndo nakwambia waambie na hao mnaofikiri Mbowe ni mwanasiasa msaka fursa - mmepotea.
Hitimiaho la hoja yangu hujalitafakari kwa ujumla wake. Nisome tena.
 
Kuna kitu wafuasi wa Mbowe wanaweza kukifanya kuishinikiza serikali kumuachia Mbowe?
Mtateska sana kwa kulezwa ukweli kuwa hii ni kesi ya mchongo kama huko ndio kushinikiza.
 
Tun
Tunalaumu Majaji na serikali lakini tunasahau kulaumu waleta Uchuro kule space na Mahakamani. Hakuna Jaji atakaye kubali kutoa uamuzi kwa kelele na shinikizo la mashabiki wanaojaribu kumuelekeza nini afanye. Mnamnyima nafasi hata ya kutumia busara ktk kutoa maamuzi.
 
Ataka asitake, huyo Jaji na walio nyuma yake lazima waelezwe ukweli.
 
Samia anahusika vipi hapo?
 
Mtateska sana kwa kulezwa ukweli kuwa hii ni kesi ya mchongo kama huko ndio kushinikiza.
Hoja yangu ni kwamba Mbowe alipaswa kuungwa mkono kwa vitendo na siyo maneno matupu.

Yaani yeye anateseka huko mahabusu halafu mamilioni ya watu (wafuasi wake) wanaishia kuandika maandishi ya kiujumla jumla tu.

Mahakamani hawaendi, maandamano hawafanyi, kuziba barabara hawazibi, Wala hawachomi moto matairi ya gari, n.k. Sasa mfumo ukiamua kumfunga Mbowe kutatokea shu yoyote ya kukitikisa serikali ya ccm?
 
Mimi naomba Mungu amtendee kama Mwendazake,
SSH hawajui CCM vyema akimfunga Mbowe tukapigwa ban na wazungu CCM wote watamkimbia aachane na siasa za kijinga hizi. Mbowe angetaka kuwa gaidi angefanya 2015 wakati wa Lowasa, anaona sifa kumtesa mwenzake ila ajue kabisa kuna kiama chake. Siasa za wenzetu Wakenya hazina ujinga huu japo kuna ubabe ila sio wa kutesana hivi. Ngoja tuache amfunge halafu tuone atapata nini. Urais wenyewe kaupata kwa bahati ya mtende ngoja agombee tena atajuta. Nimemchukia sana huyu bibi leo.
 
Makamanda wako mbele ya Muda. T-shirt hizo wamezipata lini??👏👏👏
 
Tuendelee kumwaombea. Hayati tulimsihi sana lakini hakuwahi kusikiliza.

Kilio cha wengi kinamfikia Mwenyezi Mungu.
 
Ushindi pekee kwao ni Mbowe kupiga goti, aombe msamaha! Otherwise, hata wamuue, Mbowe atakuwa amekufa kishujaa, demokrasia na upatikanaji wa katiba mpya nchini, vitakuwa na jina jipya! Mabadiliko ndani ya taifa hili yataitwa Mbowe!
 
Mbowe anatembea kwenye ukweli na haki kamwe hawezi kuvisaliti kwa mateso anayopitia. Tuendelee kumuunga mkono na kumuombea sana kwa Mwenyezi Mungu.
 
Aombe msamaha kwa kosa lipi?
 
Mbowe ndo mwamba wa siasa za Tanzania..watake wasitake atatoka na watacheza mziki wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…