Wanafunzi 330,000 Wa Shule za Sekondari & Msingi Wameacha Shule Mwaka 2022 Pekee. Kanda ya Ziwa Yatia Fora

Wanafunzi 330,000 Wa Shule za Sekondari & Msingi Wameacha Shule Mwaka 2022 Pekee. Kanda ya Ziwa Yatia Fora

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Aisee pamoja na Juhudi za Serikali kupanua Elimu ila school dropout inazidi kuongezeka

Wanafunzi takribani 330,000 ni wengi sana kuacha shule Kwa mwaka mmja tuu.

Hali ni mbaya zaidi Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kigoma.Kwa Hali hii Mbulula hawatakuja kuisha hapa Tanzania. Nini kifanyike iki kuokota kizazi Hiki?

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1703840973652955281?t=hzgeZVAkwv2l9gwYiVfcUg&s=19
20230919_211840.jpg
20230919_211832.jpg
 
Kwa mujibu wa TAMISEMI, Jumla ya Wanafunzi 329,918 wa Shule za Sekondari na Msingi waliacha Shule katika Mikoa 26 Nchini mwaka 2022 kutokana na sababu mbalimbali.

Sekondari walioacha Shule ni 136,313, Wavulana wakiwa ni wengi (69,847) na Wasichana 66,466. Shule za Msingi walikuwa 193,605 (112,366 Wavulana na Wasichana 81,239).

Aidha, katika kipindi cha mwaka 2017-2019 jumla ya Wanafunzi 308,611 wa Shule za Msingi waliacha Masomo ambapo Utoro, Mimba, Vifo na Nidhamu vilitajwa kuwa visababishi vikuu.
 
Mimba si cherikali iliruhusu...
Mjomba magu akaonekana si chochote kwa ule msimamo wake!
 
 
Ni hatari taifa kuwa na watu wengi wasio na elimu za kutosha. Serikali haina budi kubadili mfumo wa elimu kuendana na wakati. Hao walioacha wamekata tamaa ya kupata maisha mazuri ya kupata kazi za kuajiriwa. wanaona waliosoma hawana ajira wanasota mitaani hali zao ni mbaya. Serikali ijifunze kwa mataifa mengine wanafanyaje raia wao kuwa na elimu kubwa na hawajaajiriwa serikalini, wanaendesha maisha yao vizuri tu na si rahisi kuwageuza watumwa kwa wageni kiasi cha kuishia kufanya kazi za vibarua kwa makampuni ya kigeni. Elimu ni muhimu sana kwa raia
 
Back
Top Bottom