Wanafunzi Dar na Dharau kwa Wakubwa Wao

Wanafunzi Dar na Dharau kwa Wakubwa Wao

Ifike mahali hao wanaoitwa Wakubwa, wazee, wajawazito, walemavu na wamama wenye watoto wawe wanaangalia na gari za kupanda. Utakuta gari zipo foleni, inayopakia ishajaa inaanza kuondoka anakuja mjamzito au mzee anapanda anasimama halafu anaanza kutia huruma akiwa kasurubiwa. Ifikie mahali kama unajijua una watoto au mtoto na umekwenda mahali, jitahid urudi mapema kabla ya mida ya tabu za usafiri hapa mjini haujaanza.
 
Leo kwenye daladala kuna mama alimwambia mwanafunzi ampishe mzee akae. Yule mwanafunzi badala ya kujibu kistaarabu labda mama nimechoka au nnitalipa nauli ya mtu mzima ila alichokifanya ni kujibishana na yule mama. Akaanza kumwambia simpishi mtu angetaka angewahi. Mama kujibiwa vile akapata moto. Akamwambia nyie watoto wa siku hizi hamna adabu mzee kasimama wewe umekaa halafu unajibu vibaya. Mwanafunzi akamwambia mama "usitafutie kik kwangu kama una stress mshahara hujatoka achana na mimi." "Kwanza nakushangaa unavyoniambia nimpishe si ungempisha wewe". Mama akamwambia "we mtoto nina mtoto kama wewe nyumbani usinijibu vibaya". Mwanafunzi akamjibu "mama kama mtoto yuko kwako ungekua na mtoto kama mimi ungemleta kwenye garia saa hizi mbona hayupo kwanza achana na mimi na stress zako za kutolipwa mshahara".

Haki nilijisikia vibaya yule binti kumjibu vile mama wa watu. Sawa sio jambo zuri kumsimamisha mwanafunzi ili mtu mzima akae lakini yule binti ana mdomo mchafu sanaa. Kwa style hii hawa wanafunzi wa Dar wataendelea kufeli kwa sababu hawana adabu kwa mkubwa wala mdogo. Nimewazia walimu wake atakua anawajibu dharau kiasi gani wakiwa wanamgombeza.
[emoji23] ndio maana wanapata mimba
 
Leo kwenye daladala kuna mama alimwambia mwanafunzi ampishe mzee akae. Yule mwanafunzi badala ya kujibu kistaarabu labda mama nimechoka au nnitalipa nauli ya mtu mzima ila alichokifanya ni kujibishana na yule mama. Akaanza kumwambia simpishi mtu angetaka angewahi. Mama kujibiwa vile akapata moto. Akamwambia nyie watoto wa siku hizi hamna adabu mzee kasimama wewe umekaa halafu unajibu vibaya. Mwanafunzi akamwambia mama "usitafutie kik kwangu kama una stress mshahara hujatoka achana na mimi." "Kwanza nakushangaa unavyoniambia nimpishe si ungempisha wewe"

Mimi naona wote wana makosa. Huyo Mama alipaswa kukaa kimya Mwanafunzi ajiongeze mwenyewe kama ana adabu au ampishe yeye. Kuna vitu vingine ni vya kuacha tu, hivi kweli Wanafunzi wa Dar wanavyohangaika na usafiri mara Konda amsukume, wengine wakishaona wanafunzi hawasimami leo kapata siti unamwambia simama umpishe Mzee!! Kweli, na hapo ukute ni busy hours gari hazitembei.
 
Back
Top Bottom