Mwanafunzi pekee ndio mwenye maamuzi ya kusoma au kutosoma
Si kazi yake mwalimu kuamua Nani asome!
Hata Kama Mwanafunzi amepata F form two, ni haki yake kuamua asome chemistry au aache,
Hizo geography, Biology na maths wanafunzi wanapata F na wanaendelea kusoma
Unamwamuliaje Mwanafunzi, mustakabali wake?
Unaijua hatima ya maisha yake mbeleni?
Waalimu wajue kuwa shule sio zao, maabara sio zao, maburette, mahydrochloric sio zao, Ni za serikali kwa Kodi za wazazi wa hao anaowakataa,
Mtoto amepata C, D form two, anataka kuendelea kupambania kombe yeye anamzuia kwa mamlaka gani? Kwa muongozo gani?
Mwalimu Bora Ni yule anayemwezesha kilaza kuperform kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji
Mwalimu huyohuyo, ameshasahau alipata chemistry C form four, chemistry D form six, na alipata sup ya kozi ya chemistry kule DUCE
Hizo D, vijana wetu zinawasaidia kwenda kusomea ufugaji wa kuku na wakaanzisha ufugaji kujikimu na maisha
Waalimu wanajifanyaga ndio wafalme wa shule, ndio watunga sera za Elimu wakati wao ni watekelezaji wa sera tu
Watunga sera wametoa option kwa Mwanafunzi, na si kwa mwalimu,
Kazi ya mwalimu Ni kufundisha tu!
Waalimu hawapendi kufuata miongozo ktk uendeshaji wa shule, ndio maana serikali itasema wanafunzi warudi likizo, wao wanasema hapana wasirudi likizo
Serikali itasema bakora ni fimbo tatu, wao ni bakora za mvua tena za changizo waalimu wote staff