choza choza
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 2,081
- 3,831
Hivi wale wanaoingia form iii wana c moja ya kiswahili masomo mengine F nao wafukuzwe kwenye hayo masomo au!Nchi hii ina wazazi/walezi wapumbavu sana, mtu anashindwa kumpambania mtoto wake halafu ankuja kulialia mitandaoni kwa kubebesha watu lawama.
Hivi unadhani PHY/CHEM ni fuvu kila mmoja analo?.
Kusoma masomo hayo kunahitaji mtoto mwenye IQ kubwa ambaye yuko tayari kujibidisha.
Mimi sio mwalimu lakini nimebobea kiasi kwenye moja ya masomo ya sayansi, hivyo ninaelewa uzito wa hayo masomo kuanzia O-level hadi University.
Mwalimu hawezi kuwa na uchungu wa kuhangaika na mwanao uliyemtelekeza mithili ya kuku wa kienyeji, unaona shida kutoa elfu 5 mwanao asome tuition ili kumuongezea uelewa halafu unakuja kumlaumu tu mwalimu.
Umeona elimu ni gharama bakini na ujinga wenu, pia mchuma janga hula na wakwao
Wengine familia ziliuza vingi ili kututengenezea mazingira ya kumudu hayo masomo ila nyie mmekaza fuvu kutafuta lawama kwa serikali na waalimu kwenye vitu mnavyopaswa kuwajibika wenyewe moja kwa moja.
Cc DeepPond
Sera inasema mwanafunzi atachagua, wala haijasema awe amepata grade ipi
Kazi ya mwalimu ni kufundisha sio kuchagulia watoto kitu cha kusoma, hiyo ni kazi ya watu wengine
Huyo mtoto akipata F, cheti chenye F kitakua ni cha huyo mtoto sio mwalimu