SoC04 Wanafunzi kundi kubwa la kulisha taifa

SoC04 Wanafunzi kundi kubwa la kulisha taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

deovshayo

New Member
Joined
Jun 7, 2024
Posts
1
Reaction score
2
KUBADILISHA TANZANIA TUITAKAYO.

Tanzania nchi Yangu iliyobarikiwa kila njanja,
Tanzania iliyo na Neema ya uoto asili,
Nchi iliyo na Watu Wenye afya ,Iliyobarikiwa Viongozi walioleta Amani na Chakula kwa Wanachi wake.
Napenda Kuongea na Nyie kupitia Jamii Forum,
Huenda mawazo Yangu yakawa Chachu ya kubadilisha Nchi Yangu.
Mungu na ayabariki Mawazo Yetu,na Forum hii.

Taifa lolote,Familia yeyote ,Mtu yeyote akiwa na Chakula na Afya,huwa ni Chanzo cha Amani.
Hivyo yatupasa kuzalisha sana tuipate hii Amani.
Amani ya kiuchumi,
Amani ya akili zetu.
Amani ya kupata muda wa kufikiria na kugundua Tekinilojia mbalimbali.

Njia ambayo tunaweza kuitumia,njia ambayo nataka kuongea na Taifa langu ni pamoja na haya.

Taifa litumie Wanafunzi ,kundi hili kubwa sana katika uzalishaji.
Kundi hili kila mwaka huingia mtaani pia.
Hivo tutengeneze Jamii katika Vitendo zaidi.

Katika miaka ya kukaa shule,ile miaka 6.
Au shule ya upili ,sekondari ama Chuo.
Mwaka Mmoja uwe ni mwaka wa kuzalisha,
Na alama za mitihani zitoke hapa.
Mfano,Mwanafunzi anatengewa heka Moja za kulima mahindi,kiasi cha Mavuno yatakayo toka ndizo Alama zake za ufaulu.
Mfano gunia moja liwe na alama zake,

Kuna Maeneo makubwa sana Tanzania ambayo yapo wazi,
Serikali ikiamua kutoa maeneo haya Tutapata Chakula Cha kutosha.

Pili ,Kila baada ya miezi mwaka Mwanafunzi Apande angalau miti ya matunda Mitano,na ustawi wa alama za mitihani zitoke hapa,
Hakika baada ya miaka 25 tutakua na utoshelevu wa chakula cha kutosha na Afya Njema kwa Taifa hili.

Inawezekana kutengwa aina mbili ya kuleta mabadiliko haya kwa wanafunzi,
Aina ya kwanza ni wale watakaoleta uvumbuzi wa kurahisisha tekinolojia ya uzalishaji,
Hawa watengewe alama zao.

Na wale wa uzalishaji kabisa,
Lazima kuwe na motisha kubwa vijana waweze kuipenda,
Kuwatafutia soko la waliozalisha,
Serikali kuwawezesha na vifaa,mbolea na maghala ya kuhifadhi mazao yao.

Kuandaa wakufunzi watakaowezesha hili.
Wenye matokeo mazuri kupata ajira za haraka katika taasisi mbalimbali,
Hii ni kuwafanya wanafunzi kuwa na Ari kubwa zaidi katika uzalishaji.

Si wote watakaoweza kusimamia hili.
Ardhi hiyo itumike kwa mzunguko,
Kwa wale watakaofanikiwa zaidi wapewe muda zaidi wa kuendeleza,
Hata baada ya kuhitimu.
Na mashamba ambayo ambayo hayataendelezwa yanyanganywe.

Hii iwe ni lazima kwa kila shule ama Chuo,
Nahakika miaka kadhaa tutalisha mataifa ,
Uchumi wa Vijana utakua,
Utegemezi na malalamiko ya Ajira itakua Mwisho.

Shule ama Chuo kununua Chakula ndio itakua Mwisho,
Kila mwanafunzi atajilisha sasa na kulisha wazazi na Taifa hili zuri lililo barikiwa Rutuba na maeneo makubwa sana.

Tusiache upenyo wowote usiwe na uoto,
Maeneo haya makubwa yote yatawaliwe na mimea ya chakula.

Tukipata Wakufunzi wazuri,
WAtakaoleta Tija katika hili,
Taifa litakua na chakula cha kutosha.

Mwisho kabisa napenda kutoa ushauri tusisite kuvunja mifumo yetu mibaya ya Elimu,na kuongezea mifumo imara yenye kuleta Tija.

NI muda stahiki,kwa Taifa letu kuwa kitovu cha Kulisha mataifa mengine.
Asante.
Deo Jx.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom