KERO Wanafunzi MUHAS hatufundishwi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba waziri wa sayansi na elimu ya juu na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) mtusaidie tuweze kupata wahadhiri wa kutufundisha masomo ya tiba kwa njia ya vitendo ngazi ya shahada ya kwanza ( occupational therapy) katika chuo kikuu MUHAS.

Tangu chuo kifunguliwe hatujaanza kusoma masomo hayo , tunaambiwa walimu watakuja ila hatuwaoni wakati mwisho wa muhula unazidi kukaribia.

Kwakweli ada tumelipa ila hatupati haki ya kufundishwa kama inavyotakiwa kuwa.

Tunaomba kuwasilisha.
 
Madogo hebu tulieni, mtafundishwa tu...

Hiyo bachelor degree ni mpya kabisa kwa hapa Tanzania, na inatolewa na MUHAS tu..

Hivyo hata walimu wake inabidi waletwe kutoka nje ya nchi, ambayo ni gharama kubwa...

Hiyo kozi muwe na uhakika mtafundishwa kwa zimamoto sana, hilo mkae mkilijua. Ila mkimaliza mtakuwa na soko sana..

Cha kufanya kwa sasa, chukueni curriculum yenu kisha muanze kujisomea mdogo mdogo, hiyo ndiyo maana ya "Adult Learning"...
 
Nanukuu: "..................kupata wahadhiri wa kutufundisha masomo ya tiba kwa njia ya vitendo ngazi ya shahada ya kwanza ( occupational therapy) katika chuo kikuu MUHAS."
Ina mana Theoretical part Tiba ya magonjwa ya kiKazi mnafundishwa sio?
 
Mchakato wa kupata waatalamu wa kufundisha hayo masomo unaendelea mkuu.

Kumbuka hii ni kozi mpya nchini hivyo kuweni na subira na jiongezeni kutafuta maarifa mtandaoni naamini mtaala wenu mnaujua.

Kila la kheri wataalamu
 
Occupational Therapy inatolewa pia na KCMC muda mrefu kabla ya hao Muhas
 
Mchakato wa kupata waatalamu wa kufundisha hayo masomo unaendelea mkuu.

Kumbuka hii ni kozi mpya nchini hivyo kuweni na subira na jiongezeni kutafuta maarifa mtandaoni naamini mtaala wenu mnaujua.

Kila la kheri wataalamu
Kabisaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…