Wanafunzi na walimu ni kama maadui

Wanafunzi na walimu ni kama maadui

Mwanangu alirudi nyumbani siku moja huku akiongea kusema "Ile shule siitaki , usiponihamisha siendi tena"
Imagine mtoto wa darasa la kwanza Mwalimu anamwadhibu kwa kumpigisha ukutani...
Kama hautaki mtoto wako achapwe baki nae nyumbani.

Ungekua na busara ungefika shuleni kujua shida nini sio kutukana watu hapa.
 
Mwanangu alirudi nyumbani siku moja huku akiongea kusema "Ile shule siitaki , usiponihamisha siendi tena"
Imagine mtoto wa darasa la kwanza Mwalimu anamwadhibu kwa kumpigisha ukutani....
Kwa maelezo haya mfundishe mwanao wewe mwenyewe Kwa masomo ya darasa la Kwanza yatakushinda?

Wazazi wenye katoto kamoja mna nongwa Sana.
 
Mwanangu alirudi nyumbani siku moja huku akiongea kusema "Ile shule siitaki , usiponihamisha siendi tena"
Imagine mtoto wa darasa la kwanza Mwalimu anamwadhibu kwa kumpigisha ukutani...
Wazazi wanyakati hizi mmekuwa waovyo Sana, mnawadekeza hao wakina junior mwisho wasiku mnarudi humu kuomba ushauri kuwa watoto wamewashinda
 
Walimu chapeni mboko ila kwa kiasi mkijua na ninyi mna watoto nao wana walimu wao . mtoto bila viboko ni kazi sana kumuweka kwenye msingi mwema.
 
Poleni
Hivi Huwa mnaonaje ukikaa nyumbani mwezi na watoto wako wawili asubuhi had jioni hiv nyumbani izo vurumai zao imagine mtu anakaa nao 70 had 200 baadhi ya shule lazima Kuna mambo hayawez kua sawa kama unavotarajia
 
Kadri miaka inavyoenda tunazidi kuwa na wazazi wa hovyo sana! Kina baba juniors wanaoshikwa makalio na watoto wao, kisa wazungu hawachapi! Ipo siku atakutia kidole makalioni mbele ya watu ndio utajua kwa nini walimu huadhibu watoto Ili kuepusha tabia hasi
 
Hiyo chuki yako hadi kuandika uzi wenye maneno ya kudhalilisha waalimu imevuka mipaka. Kama kuna shida mahali malizana na mwalimu katika namna sahihi ila sio kuwaona kuwa ni mataahira.

Kusema kwamba wanafunzi wasichapwe viboko ni upumbavu tunaoweza kujutia baadae. Huko Marekani vijana ni kama wameshachanganyikiwa kwa tabia za hovyo hasa wale black. Sisi tuko sahihi kulinda maadili yetu. Ukikereka zaidi hamishia mtoto wako London.
Kweli kabisa huko Marekani si ndo watoto wanakwenda na bunduki kuuwa wenzao
 
Mwanangu alirudi nyumbani siku moja huku akiongea kusema "Ile shule siitaki , usiponihamisha siendi tena"
Imagine mtoto wa darasa la kwanza Mwalimu anamwadhibu kwa kumpigisha ukutani.

Hilo nikamtuma wife akaongee na mwalimu aliyefanya huo ujinga likaisha. That was January.

Maisha ya shule huyu mwanangu yanaendelea vizuri.

Majuzi kachapwa kwa kutokufanya zoezi na utoro huku mwanangu hana trend ya utoro. Ilikuwa mistake tu ya utoto aliandika zoezi karatasi ya nyuma badala ya mbele. Akiona uwazi kwenye daftari kwa nyuma huwa anatumia huo uwazi. Sasa mwalimu hakuona zoezi la jana na kuhesabu tu kuwa mtoto hajafanya kazi ya Jana.

Nimeongea na mwanangu kuwa asiandike nyuma sasa hata kama ameacha karatasi isiyo na maandishi.
Sasa hata ingekuwa ni kweli mtoto hajafika shule au alifika lakini hajaandika ni sahihi umchape?

Enzi hizi bado walimu wanaendelea kuchapa watoto?

Walimu mpaka kesho hawajui kuwa mabosi zao sio maafisa elimu, madiwani na ma DED bali wanafunzi.

Je, kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kumchapa boss wake?

Kama watoto ni wasumbufu hiyo haiwapi uhalali wa kuwachapa watoto ni aina ya maboss waliowachagua , wawahudumie vivyo hivyo.

Shule za serikali zinaongoza kwa kuzalisha watoto vilaza kwakuwa walimu hawajagundua kuwa wanafunzi ndio maboss wao.

Wanafunzi na walimu ni kama maadui.
Kwa primary kama umejaliwa kauwezo, mpeleke mtoto English Medium apate msingi wa kiingereza.
 
Mathematics O level nimefundishwa na Mzungu, ni mmarekani. Anasema kule darasa zima wanapata One na ikitokea mtoto ka loose basi ana two.

Adhabu ya viboko waliiondoa kwakuwa ni utumwa.

Je, kati ya nchi hii ya mafimbo na US ni nchi ipi ina wasomi bora?

Hizi shule za kata ambazo walimu wanashindana kupiga fimbo ukitazama matokeo ya form four ni uchafu mtupu
Tiba ya Wenzetu imeanzia Nyumbani.Hakuna kitu Wazungu wametupita kama kulea Familia,tuachane na Series au Movies hizo.

Ninayo mifano hai mikubwa.Na ndio maana wako hivyo.
Japo kuna familia ziko huko pia hazina tofauti na baadhi ya familia za huku baadhi.

Kulea watoto kunataka Adabu kubwa sana na utulivu wa hali ya juu kama Mzazi.
 
Kumbe ulipenda Masomo ya hela hela tu 😜

Binafsi nilipenda Sayansi na nilifanikiwa kusoma Sayansi(Engineering ) ambayo inasaidia kusolve matatizo ya Jamii hapa Bongo

Japo ningeendaga kusoma vyuo vya mbele huko huenda ningekuwa best Engineer kuliko ilivyo sasa🥲
Karibu Bongo,tuliotaka kuwa Marubani mambo yakagoma.

Sasa hivi tunaendesha ndege watu😃😃😃😃😃
 
Karibu Bongo,tuliotaka kuwa Marubani mambo yakagoma.

Sasa hivi tunaendesha ndege watu😃😃😃😃😃
Hii Nchi inaua ndoto za Vijana wengi tu

Watu walikuwa na ndoto ya kuwa Madaktari wanaishia kuwa waendesha Bodaboda 🙌
 
Sawa viboko ni Moja ya njia ya kumrekebisha mtoto, lakini walimu wa siku iz wanashindana kuchapa Yani awe kinara wa kutia bakora, na walio wengi wanasemaga kabisa Mimi sikupenda kuwa mwalimu imetokea Tu bahati mbaya. Sasa mwalimu huyu ataacha kukuchapa fimbo 10 za hasira na kukupigiza ukutani Kwa kosa na kuruka karatasi na kuandika kazi karatasi inayo fuata? UALIMU NI WITO.
 
Back
Top Bottom