The Best Of All Time
JF-Expert Member
- Aug 30, 2022
- 3,282
- 7,730
Wanafunzi wafanya maandamano ya kupinga Muungano wa Ulaya juu ya mzozo wa mafuta wa Uganda
Patience Atuhaire / BBCCopyright: Patience Atuhaire / BBC
Mamia ya wanafunzi wa Uganda wanaandamana dhidi ya bunge la Ulaya, baada ya kupinga mradi wa mafuta baina ya nchi hiyo nan chi Jirani ya Tanzania.
Wabunge wa EU mapema mwezi huu walipitisha azimio wakionya kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu na hatari za kijamii na mazingira zinazoweza kusababishwa na mradi huo.
Wanafunzi hao wanaandamana mjini Kampala kufikisha hoja yao kwa ubalozi wa EU.
Maandamano hayo yanaonekana kuidhinishwa na taifa na wanafunzi wanatembea huku wakisindikizwa na polisi.
Wakati ujenzi wa bomba hilo la mafuta lenye urefu wa km 1,443 (maili 896) kutoka Ziwa Albert magharibi mwa Uganda hadi kwenye bandari ya Tanga nchini Tanzania kwenye bahari ya Hindi.